Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Leo ndio Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Habari, ambapo kwa hapa Tanzania, siku hii imeadhimishwa kwa siku mbili, jana na leo, katika hoteli ya Nashera mjini Morogoro.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absolom Kibanda, amezungumza kwa ukali na kwa uchungu jinsi utawala wa JK ilivyo kandamizi kwa uhuru wa habari kuliko utawala mwingine wowote Tanzania!.
Huku akielezea kwa uchungu kuhusu kifo cha Mwanahabari Daidi Mwangisi, na kuelezea madhila yaliyomkuta yeye ya kungolewa kucha, meno na jicho!, kumbe serikali ya Tanzania iliulizwa rasmi na Jumuiya ya Kimataifa kuhusu matokeo haya, Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe, alitoa taarifa ya uongo kuwa madhila yaliyomkuta Kibanda, ni mambo binafsi!.
Kibanda ametoa hoja za msingi sana, nafanya utaratibu kuipata video yake niwawekee, msikilize wenyewe!.
Baada ya kumaliza ukumbi mzima ulisimama na kumpigia makofi ya Standing Ovation!.
Pasco

OFFICIAL OPENING Moderator: Prof. Penina Mlama (UDSM) / Edda Sanga (SJMC) MC's of the event: Jane Mihanji/ Usia Nkhoma-Ledama
|