Siku ya kwanza kijiweni kama dereva bodaboda

Screenshot_20210620-130852.jpg
 
Uhalisia upi unaotaka ww wakati mm mwenyewe nafanya mishe hiyo so naongea kitu ambacho nakielewa 100% usiwe na roho ya uchawi ya kukatisha watu tamaa wakati ktk bolt kulaza hiyo pesa ni jambo la kawaida na endelea kutembeza bahasha katika maofisi ya watu kila siku huku ukipewa tumaini hewa
Hao ndo wale ma last born wachagua kazi
 
Kama upo kigamboni uwe unawahi pale uhasibu kuanzia saa 10 alfajiri pale pesa hatari ,mida hiyo hakuna kabisa bodaboda

Pili na muhimu Sana ,vaa helmet muda wote na usiwe na haraka barabani na jitahidi Sana ufwate sheria

Kingine Kama pikipiki Ni mpya uwe makini kupakia abria wa kuingia vichochoroni
 
Ni matumaini yangu mpo salama wote. Baada ya kusota mtaani kwa miaka miwili tokea kumaliza degree yangu nimefanikiwa kujikusanya na kupata kapesa kidogo.

Baada ya kuwaza sana nimeona ninunue pikipiki kwaajili ya biashara ya bodaboda ambayo nataka niifanye mimi mwenyewe.

Hatimaye kila kitu kimekamilika naomba msaada wa mawazo siku ya kwanza kwenda kijiweni, je unaenda kijiwe chochote unachoona kinafaa au kuna utaratibu wa kufuata ili uwe member wa kijiwe fulani?

Karibuni kwa mawazo na ushauri wenu.

Asante.
Hongera, itapata pia mademu wa kugonga...
 
Mkuu kama upo Dar kajisajili bolt hakika utaona mambo mqazuri wala huna haja ya kwenda kuomba kijiwe abiria unapata online swala la kulaza 30k au 40k na kuendelea ni jambo la kawaida cha muhimu pkpk yako iwe na bima,kadi,pleti namba nyeupe,latra zamani ilikuwa inaitwa Sumatra na leseni hai ya kuendesha chombo husika then nenda ofisini kwao pale jengo la victoria place unasajiliwa bure kabisa
Mkuu nimeku PM
 
Yaah nipo Dar mkuu Kigamboni
Nakushauri ukiweza unaweza ku-park kariakoo

Kama una ndugu au jamaa yako (mwenye biashara kkoo) anaweza kukudhamini madukani ongea nae halafu mpite madukani akutambulishe ukipatikana mzigo unapigiwa simu unawapelekea wateja

Ukifanya mizigo inaweza kukulipa zaidi
Mf:kutoka kkoo kupeleka mzigo fire 5,000
Mbezi stendi ni 12,000
Kwa siku ukipata mizigo hata 6 inatosha



Ni uaminifu tu.
 
Back
Top Bottom