Nimeshtushwa na hiki nilichoambiwa na huyu jamaa yangu ambae ni bodaboda

Black Walker

Senior Member
Oct 8, 2018
107
238
Habari za muda huu wanajamii? Ilikuwa ni usiku wa jana majira ya saa mbili hivi, nikiwa nje napunga kidogo upepo mara nikasikia muungurumo wa pikipiki.

Kumbe alikuwa ni jamaa yangu ambae tulisoma nae shule ya msingi huko kanda maalum, ukimuona ni mfupi lakini inaonekana kuwa na misuli ya kutosha yaani amejengeka kisawasawa.

Nilimkaribisha tukapata kikombe cha tangawizi kali na baada ya muda kidogo tukaletewa chakula cha usiku ugali(sembe + mhogo) na samaki aina ya sangara, jamaa alifurahi sana maana alijiona kama kafika kanda maalum.

Sasa baada ya msosi tukaendeleza story zetu na moja ya jambo nililomshirikisha ni kuhusu kuwa na mpango wa kununua pikipiki hapo baadae kwa ajili ya usafiri wa kazini na kuitumia kama bodaboda pale muda wa kazi unapisha ili kujiingizia kipato cha ziada!

Kiukweli jamaa yangu alionekana kutoafikiana na mimi, nilimuuliza kwa nini?

Kabla ya kujibu swali langu ghafla nilikuona anainuka kwenye kiti akawa kama anajinyoosha huku akipinda mgongo kwa nyuma akilalamika maumivu makali ya nyonga.

Alikaa huku akiendelea kuugulia maumivu mdogo mdogo, nikampa pole! Akaitikia akaniangalia usoni na kuniita Black walker umesema una mpango wa kununua pikipiki nikamjibu ndivyo! Akasema nakushauri utulie mambo yakikaa sawa tukae chini tusaidiane mawazo kitu kingine cha kufanya lakini sio kuendesha bodaboda.

Akadai kwamba maumivu ànayopata kwenye nyonga ni kutokana na kuendesha bodaboda kwa muda mrefu.

Kabla hajaendelea zaidi tukawa tumeingiza hoja ya wanawake hapa ndo nilipigwa na mshangao mkubwa, anadai kwamba pikipiki inachangia sana kuua nguvu za kiume na alinishangaa aliposikia namwambia mimi hata nilale na mwanamke kila siku yaani ni lazima kiwango cha chini niondoke round 2 yeye alidai amekuwa akiishia kimoko mara nyingi tena kwa tabu sana.

Yaani hiyo ndo habari ambayo kiukweli imenisikitisha zaidi na kuona kabisa kwamba kumbe wanaume mashababi wanapungua kwa kasi kubwa.

POLENI SANA WAENDESHA PIKIPIKI.
 
Bodaboda wa wapi anaowazungumzia..?

Maana deile tunasikia lawama kuhusu boda kutembea na wake hata mademu za watu

Kwa hyo mademu zetu wanashoboka na hcho kimoko 🤔
 
Nguvu za kutafuna wake za Watu na wanafunzi wanazipata wapi? Au pia huko pia ni kimoko?
 
Kweli wengi wanaumwa migongo ndio maana wanatafuta pozi la kukaa kwenye bodaboda.

Mara nyjngi wanaoindisha kiuno au kukaa tako moja kutafutia balance na pozi.

Mda mwingine pikipiki inatulia Road mda mwingi jua kali. Anakalia kiti pumbu zinawaka moto. Ukirudi nyumbani pumbu zimeiva sio poa
 
Research yako ndo imeishia hapo tuu?
Anyway tatizo kubwa ni tunajisahau sana lifestyle zetu.
We sa 10 alfajiri upo juu ya chuma, unaenda kulala saa 6 usiku. Hio nguvu ya kupiga viwili utatoa wapi?

Sio tu bodaboda, wengi waliojiajiri ndo wana lifestyle hii.. sa 12 mtu kafungua ofisi anakaa mpk sa 4 usiku hapo atakunywa chai na chapati, mchana chips, usiku wali, kulala saa 6 kuamka sa 11, hakuna muda wa kupumzika. Hakuna muda wa kufanya hata jogging.. WTF do you expect..
 
Kama anafanyiq kazi zake rafu road iyo lazima ila kama uku mjini kila sehem lami tatizo atakalopata labda ulemavu tu wa ajali na kifua
 
Back
Top Bottom