Siku ya Kifo Changu

Siku ya Kifo Changu

Kifo ni tukio kama matukio mengine, mimi nasubiria kifo kama ninavyopokea mwaka mpya au X - mas. Nizikwe mahali popote kwa gharama ndogo, nizikwe kwa jadi yangu ya mila sio hizi dini zilizokuja kwa meli.
Nifahamishe mkuu huwa kwa jadi yako ya mila mnazikwaje??
 
Ni kweli kila mmoja wetu atakufa na kwa mtu yeyote aliye makini ni lazima siku moja utajaribu kuimagine siku hiyo ya kifo chako itakuwaje na huku nyuma mambo yatabaki vipi? Lakini ni ukweli usiopingika kwamba marehemu huwa hana mamlaka na mwili wake bali wafiwa ndio wenye mamlaka, hivyo kuna mambo unaweza kuagiza lakini yasitekelezwe!

Mfano: Huwezizuia watu wasikulilie pindi utakapokufa, kilio huja kutokana na hisia za huzuni pale watu wanajaribu kukumbuka katika umuhimu na uwepo wako!

Pia huweziamrisha watu watawanyike masaa 7 tu baada ya kifo chako maana huwezijua utakufa lini na utafia wapi na wakati unakufa je wale ndugu muhimu kama Mama, Baba, kaka,dada, mke, watoto watakuwa karibu nawe? Hawa ndio wataamua uzikwe wapi na uzikwe lini!

Hiyo pesa uloanza kujiwekea nashauri usiiweke bali kama unaishi katika nyumba yako mwenyewe basi tenga chumba maalum, kanunulie sanduku unalotaka kuziwa nalo na vingine vyote uhifadhi humo ili siku ya kifo chako wavichukue na kuvitumia, lakini ukiacha pesa zitachukuliwa na hazitatumika bali michango ya watu ndo hutumika kufanikisha hilo suala, kwanza siku hiyo hata mkeo tu hawezi kabisa kuwa na nguvu hata ya kuinuka kwenda huko benk, chezea kufiwa na mtu wa tegemeo kwa familia kama baba wa familia huwa si mchezo!
Kwenye huu uzi nimeona comment nyingi ambazo walio-comment wanaonekana kuwa si wajuzi wa mambo
 
Unajitabiria kufa kifo kitakufuata badala ya kumuomba Mungu uishi kwa lile dhumuni lake la kutuleta duniani ili tumuabudu . tunaishi kwa imani na imeandikwa Zab 118:17 sitakufa bali nitaishi ......Muombe Mungu uishi maisha marefu na mazuri umtukuze huku ukisifu matendo yake makuu .

Hata ukiishi maisha marefu kiasi gani, mwisho wa safari uko pale pale kifo.
Ni vizuri kupata muda wa kuitafakari na ikiwezekana kujiandaa na kyandaa mazingira ya hiyo siku iweje.

Kuogopa haisaidii.
 
Siku ya KIFO Changu

5. Kaburi langu lisijengewe wala kuandikwa jina.

6. Nisivikwe nguo yoyote zaidi ya kitambaa kitakachohifadhi tupu zangu.

7. Pombe na Ulevi haviruhusiwi kwenye maziko yangu. Wala sitotaka watu wavae nguo nyeusi. What the hell na nguo nyeusi. Watu wavae mavazi waliyoyazoea na yakawaida

8. Sitopenda nyimbo zozote zipigwe wala mtu yeyote kuimba. It is the moment of silence to honor my existence.

Nimekukubali! Ila hapo namba 5-8 kwangu, aa! Iwe kinyume na unavyo taka wewe!
 
Kuwahoji nini ? Huo upepo unafuata Bendera ya Tanzania au ya Kenya ? Be specific
Hayo mliyo kuwa mnaelezwa kuhusu kifo kwa akili unaona hamkupaswa kuhoji ?

Pili, ama kuhusu bendera na kufata upepo,ulichokiandika hapa kimeonyesha ni kwa namna gani ulivyo kilaza ndiyo hata kuhoji uwezo hukuwa nao. Ni bendera ni bendera yoyote na upepo ni upepo wowote, yaani jambo la ujumla unaliza kwa jambo khasa ? Nyinyi wa kupigwa makofi kabisa kwa ujinga mlio nao.
 
Maisha hayana maana kabisa. Eti unazaliwa kisha unakufa.
Kitu chenye maana una kipimaje ? Hivi hizi akili huwa mnazitumia kwenye nini ? Yaani unahitimisha ya kuwa maisha hayana maana kwa kifo wakati kifo ndiyo kinaonyesha maana halisi ya kifo.
 
Siku mzee wangu alipofariki. Wakati wa kwenda kuchukua mwili niliingia monchwari kwenda kusaini. Pembeni kulikua na meza mbili juu wamelazwa maiti nadhan walikua wanataka kuwasafisha. Niliwaangalia kwa kweri nilinyong'onyea sana. Kifo kinatisha hata kukiongelea
nimeshindwa kwenda kumuosha mzee huko mortuary,nilichoweza ni kumtoa kwenye fridge basi,nimetoka nje nakutana na huu uzi. Kifo cha kisenge kinoma
 
Sasa ukifa halafu shemeji akaolewa na mwanaume mwingine, na mauti yakamkuta huko... Unadhani mumewe atakubali mkewe azikwe kwenye 'kitanda' chako..?!
Si ndio nikasema comment nyingi zinaonyesha namna ambavyo watoaji wa comment hizo wasivyo waelewa wa mambo
 
Inabidi nicheke kwanza. Usikute unae comment hata kuandika mistari mitatu kwa kutumia English hujui.

Kwa bahati mbaya hata kiswahili hujui, katika kiswahili hakuna neno kiinglishi LoL
Tujikite kwenye Hoja ya 'Kiinglishi' chako chenye Tege😛
 
kifo kipo na hakikwepeki, ingawaje akili zetu hatujazilazimisha kukubali kwamba hii dunia si yetu na kinachofany mwanadam asikubali kifo ni ile hali ya kusahau tu, mtu anakumbuka mambo ya kifo pale panapotokea msiba tu au anapoona mada za kifo kama hapa laiti tungelikuwa tunawaza kifo kla dakika basi uenda akili zetu zingezoea kuwa kifo ni kitu cha kawaida.

Mm insha Allah namuomba Mwenyezi Mungu anichukue akiwa radhi nami (Mwsho mwema) , pili mazishi yangu yafanywe kwa taratibu za dini yangu ya kiislamu, tatu kama ntaaacha watoto basi waniombee dua kwani amali zangu ztakuwa zmekatika isipokuwa wao wanaweza nifaa kwa kuniombea dua.

"Yaa Rabb tujaalie mapenzi ya kufanya matendo mazuri yanayokuridhisha wewe ,tujaalie tuwe ni wenye kutoa sadaka ambazo zitatufaa baada ya kufa kwetu, tujaalie vizazi vilivyovyema vitakavyokuwa msaada kwetu baada ya vifo vyetu."
 
Ni kukubaliana nacho hamna namna...ila maiti inatisha na kutukumbusha madhumuni ya sisi kuishi hapa duniani kwa kila mwanadamu,kwa Mara ya kwanza nilikaa chini na kutafakari kwa kina kabisaaa dhumuni La sisi kuishi duniani baada ya kuanza kuosha maiti za watu wangu wa karibu ambao ni marehemu,inaogopesha mno na pia kukurudisha ktk tafakuri Kali juu ya maisha ya duniani kama utakuwa ni timamu akilini kwako...
 
Hayo mliyo kuwa mnaelezwa kuhusu kifo kwa akili unaona hamkupaswa kuhoji ?

Pili, ama kuhusu bendera na kufata upepo,ulichokiandika hapa kimeonyesha ni kwa namna gani ulivyo kilaza ndiyo hata kuhoji uwezo hukuwa nao. Ni bendera ni bendera yoyote na upepo ni upepo wowote, yaani jambo la ujumla unaliza kwa jambo khasa ? Nyinyi wa kupigwa makofi kabisa kwa ujinga mlio nao.

Sasa kwanini upige watu makofi kaka
 
Ni kukubaliana nacho hamna namna...ila maiti inatisha na kutukumbusha madhumuni ya sisi kuishi hapa duniani kwa kila mwanadamu,kwa Mara ya kwanza nilikaa chini na kutafakari kwa kina kabisaaa dhumuni La sisi kuishi duniani baada ya kuanza kuosha maiti za watu wangu wa karibu ambao ni marehemu,inaogopesha mno na pia kukurudisha ktk tafakuri Kali juu ya maisha ya duniani kama utakuwa ni timamu akilini kwako...

Ina ogopesha nini , would you please elaborate
 
kifo kipo na hakikwepeki, ingawaje akili zetu hatujazilazimisha kukubali kwamba hii dunia si yetu na kinachofany mwanadam asikubali kifo ni ile hali ya kusahau tu, mtu anakumbuka mambo ya kifo pale panapotokea msiba tu au anapoona mada za kifo kama hapa laiti tungelikuwa tunawaza kifo kla dakika basi uenda akili zetu zingezoea kuwa kifo ni kitu cha kawaida.

Mm insha Allah namuomba Mwenyezi Mungu anichukue akiwa radhi nami (Mwsho mwema) , pili mazishi yangu yafanywe kwa taratibu za dini yangu ya kiislamu, tatu kama ntaaacha watoto basi waniombee dua kwani amali zangu ztakuwa zmekatika isipokuwa wao wanaweza nifaa kwa kuniombea dua.

"Yaa Rabb tujaalie mapenzi ya kufanya matendo mazuri yanayokuridhisha wewe ,tujaalie tuwe ni wenye kutoa sadaka ambazo zitatufaa baada ya kufa kwetu, tujaalie vizazi vilivyovyema vitakavyokuwa msaada kwetu baada ya vifo vyetu."

Sawa Mkuu kila la kheri
 
Tujikite kwenye Hoja ya 'Kiinglishi' chako chenye Tege😛

Sina English yenye tege. I am sure hujui kuzungumza Kiingereza for as long as wewe ni MTANZANIA na hauna Exposure ya kutoka nje ya TZ.

Kama kweli wewe sio Local guy, nataka mawasiliano yako na Mimi hapa yawe in ENGLISH TU, otherwise utaendelea kubaki kuwa typical bongoman kama Dalali.

for as long as wewe ni MTZ , utaendelea kubaki mkosoaji kama wakosoaji wengine, lakini Nina uhakika wa , huna English ya kuzungumza au kuchat na mimi. Kama unayo, prove it, right here right now
 
nimeshindwa kwenda kumuosha mzee huko mortuary,nilichoweza ni kumtoa kwenye fridge basi,nimetoka nje nakutana na huu uzi. Kifo cha kisenge kinoma

Pole Sana. Niliandika huu uzi baada ya kupata Taarifa za Mama mwenye nyumba yangu aliyenipangisha huku ughaibuni.

Last Monday alinipigia simu kuniuliza kama Nina changamoto yoyote kwenye nyumba ili fundi aje kufanya maboresho kwakuwa mkataba wangu wa makazi ulikuwa umeisha na nika renew.

Nikamwambia AC moja naona imechoka naomba kubadilishiwa, na nipigiwe Rangi Upya sitting room yangu. Akafanya Hivyo, the following day akanicheki na akasema nikiwa na muda nikamsalimie.

Nikasema Mama I will come Jumapili maana this week imekuwa tait.

Ijumaa jioni naambiwa Mama anaumwa umwa , nikamcall kujua hali , she told me , najisikia vizuri kidogo, it gets better.

saa sita ya Usiku mtoto wake wa kike ananicheki, rarely kunicheki muda huo , kupokea simu ananiambia Mom is no more....

I was like what ... what the hell with this world , where are we going? I could not believe my ears.

Nimeumia snaa Na nikajutia as in why sikumsikiliza kwenda kumuona as she requested. Imeniuma sana na kwa majonzi nikaandika huu Uzi.

Huwa nasema kama ningepewa fursa ya kuchagua whether nizaliwe duniani au la ; mm nisingekubali kuzaliwa kwa maana matokeo ya kuzaliwa ni kifo, kama najua matokeo ni kifo kwanini niishi kwa fantasy then nije kuacha watu wangu kwa majonzi.

Naikumbuka sana nyimbo ya R KELLY aliyomtumia Michael Jackson kuiimba. R Kelly aliandika ile nyimbo based on true story ya yeye kuondokewa na mpenzi wake.

You are not alone by MJ,

Rest In Peace Michael Jackson the prophet of our time. Pole sana Michael Jackson
 
Back
Top Bottom