Sawa mkuu nimekueleza hayo sababu nakumbuka hata mzee wangu aliagiza akifa akazikwe kijijini alikozikwa mama yake mzazi, lakini baada ya kifo chake kamati ya mazishi iliamua tofauti na akazikwa palepale mkoa alipofiwa na hayo yalikuwa maombi ya mkewe kuwa awe jirani na kaburi la mumewe.
Pia mzee aliacha wosia na mgawanyo wa mali, lakini suala la mirathi lilipofikishwa mahakamani, mahakama iliukataa wosia wake na kuagiza kitu tofauti na maagizo yake japo mahakama yenyewe inakiri kuwa wosia wa marehemu unawakilisha kauli yake halisi!
Mimi binafsi ningependa nikifa nizikwe tu kwa taratibu za kawaida kama walivyozikwa marehemu wengine walionitangulia, Lakini zaidi ningependa kila anayenifahamu popote alipo akinikumbuka aseme neno lolote kuniombea pumziko la amani huko nitakakokuwa sababu mimi pia nina utamaduni wa kuwaombea marehemu wote popote kila ninapohudhuria misiba au ibada makanisani!