Tusiache kufanya checkup mara kwa mara

Tusiache kufanya checkup mara kwa mara

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
378
Reaction score
741
Tusiache kufanya check up

Miaka kadhaa nilipompokea Yesu Kristo kama Bwana na Mokozi wa Maisha yangu, nakumbuka siku ile ilikuwa ni ya kipekee kiasi kwamba ndani yangu kuliingia pendo kubwa sana ambalo sikuwai kuwanalo. Sikujua kwamba kumbe Mungu anatupenda kiasi kile , upendo ule ulipoingia ndani yangu ulibadirisha maisha yangu nilitamani kila mtu ambaye nitakutana naye nimweleze juu ya upendo wa Mungu kwa wanadamu.

Ilikuwa no siku ya kipekee maisha Mwangu. Ndivyo inavyowatokea watu wengi wanapokubali kumpokea Yesu kama Bwana na mokozi wa Maisha yao.

Pendo lile la Mungu ndani yangu lilipelekea kuwa na kiu ya kuwa na mahusiano na Mungu binafsi kwa njia ya kusoma neno la Mungu yaani Biblia pamoja na kufanya maombi na kumwimbia Mungu na kumsifu na kutangaza habari zake.

Miaka ilianza kusogea na uhusiano wangu na Mungu ulizidi kuimarika, mara baaya ya kumaliza shule na kurudi nyumbani na kuanza maisha yangu binafsi, ndio nilipoona utofauti

Maandiko yanasema Mungu anapomwokoa mtu ni kama mkulima anayepanda mbegu, kuna ambazo zitaota juu ya miamba , zingine kwenye miiiba na zingine kwenye udongo mzuri.

Mara baada ya kumaliza shule ndipo nilipojua kumbe shughuli nyingi zinaweza kukupelekea kumwacha Yesu..Shughuli nyingi ni nini, ni mahangaiko ya dunia , yaani nile nini ni vae nini? Kutaka kujulikana ,na anasa za dunia

Miimba ni kule kupekea neno lakini hakuna mzizi yaani kama vile mbegu haiwezi kukua vizuri kwenye mwamba kadhalika mtu ambaye amepandwa katika Mwamba

Lakini Mungu akutiacha akatuambia njooni nyinyi nyote ambao mnasumbuliwa na kuelemewa na mizigo na yeye atatupumzisha, hiko mizigo ambayo katika safari ya wokozi tunaibeba kwa kujua au kutojua mizigo hiyo tusipokuwa makini nayo itatuelemea na kutufanya tusiingie mbinguni

Umuhimu wa check up kwa Mkristo, kwa kuwa maisha ndani ya Mungu ni safari basi ujue kwamba kama ni safari pasi sisi ni wasafari na kama niwasafiri ujue tunatumia usafiri hakuna usafiri wowote ambao unaweza kwenda safari pasipo kufanyiwa check up.

Ni kawaida kwa usafiri kufanyowa check up ndogo au kubwa kutokana na umbali wa safari, lakini cha kushangaza wasafari wengi ambao tunasafari ya kwenda mbinguni hatufanyi checkup juu mahusiano yetu na Mungu.

Biblia inasema njia ni nyembamba ielekeapo uzimani na njia ni pana ielekeapo upotevuni, kwa hiyo kama wasafari ni lazima kufanya checkup ya njia maana safari hii ni mpya na anayeongoza safari ni Yesu

Mara nyingi hatufanyi chechup ya maisha yetu, tunaishi kama tuko jana, Yuda alikuwa na Yesu kama sehemu ya wanafunzi wa Yesu lakini alikuwa anaiba sadaka, kitendo cha kuiba sadaka Yuda aliona ni cha kawaida hakutaka kukifanyia kazi, hakujua kwamba kitendo kile kadr i kinavyoendelea kunamtenga na Yesu alikuja kushtuka ni pale alipomuuza Yesu na wayahudi walipomuua ndipo akajua amefanya makosa

Petro alikuwa mwanafunzi wa Yesu alikuwa ni mtiifu kwa Yesu alikuwa ni mwanfunzi mwenye kieleele kwa Yesu, na ile kiu yake kwa Yesu ilimasaidia hata alipoteleza katika wokovu alijua wapi ameteleza na kuomba msamaha na Mungu alimsamehe

Ni kweli tumempa Yesu maisha ni kweli ni Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu, je ni kweli tunakwenda Mbinguni? Mbona dash bodi za mioyo yetu zimejaa taa nyekundu lakini hatutakia kufanya check up

Mtoto yoyote ambaye anajua gari anajua dashbord ya gari inatakiwa kuwasha taa zote na gari ikiwa safarini taa zinatakiwa kuzima , na kama taa zitaendelea kuwaka maana kuna shida katika gari na kama ni shida ya ingini na ni serious safari yako inaweza kuishia njiani

Lakini wakristo mioyo yetu imewaka taa na wengine taa zao zimezima maana ziliwaka wakaamua kuzizima kwa njia yao ilizisiwasumbue kama wanavyofanya wafanyabiashara wakitaka kukuuzia gari bovu.

Ziko ishara kadhaa ambazo zinaweza kukusaidia kufanya checkup, aidha tuwe na utamaduni kama gari linaweza kwena chechup baada ya kilometer 3000 na kuendelea kutokana na aina ya gari na matumizi yake, kwanini wakristo hatufanyi checkup za mara kwa mara hadi tunakufa kiroho?

Unapoyachukulia poa mambo madogo madogo kama vile ni kawaida kwako siku inakwisha haujasoma biblia hata mstari mmoja haujaomba hata dakika kadhaa, wakati huo umeingia kwenye mitandao ya kijamii umesoma kila aina ya habari, na kubishana pia ujue unaitaji kwenda checkup

Unapuuzia vitu vidogo vidogo unasoma habari za chombeza, habari za mambo ya ngono na connection , view onces na kadhalika na bado unasema umehokoka ndugu yangu rudu gereje kabla injini haijazima barabarani

Uongo, matumizi, mizaa nk unakuta umeokoka lakini uongo ni sawa tu , yaani unakuwa muongo hadi unajishtukia mwenyewe rudi gereje kwa checkup .

Mahusiano yenu na Mungu lazima yawe hai siku zote hatuju lini Yesu anakuja kutuchukua kwa hiyo ni lazima hatukute mioyo yetu ni safi, biblia ni kioo soms biblia

Kuna dhambi ambazo nilisoma kwenye biblia hadi nikashangaa Samweli anasema nisije kumkosa Mungu kwa sababu ya kutokuwaaombea, Paulo anatuambi lolote ambalo sio la haki ni dhambi , na Yohana anasema sote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, kadri dhambi unavyopata nafasi katika moyo wa Mkristo utukufu wa Mungu unaondoka , unajua faidia ya utukufu wa Mungu ni kuweka hofu ya Mungu ndani yako kiasi kwamba hata kutenda dhambi unaogopa sasa hiyo ikiondoka utatenda dhambi za kila aina.

Ni kweli tuko katika Neema lakini Yesu hakutengua torati sheria ziko kama uwezo kushizika kwa njia ya Roho unatakiwa kutubu maana Sheria ndizo zinazotuleta kwa Kristo kwamba sisi ni wenye dhambi

Fanya checkup leo wengine wanaweza kuwa na checkup ndogo ndogo kama za kumwaga oili na kubadorisha filter ila wengine wanaitaji kubadirisha injini, Yesu anaweza yote , we nenda kwa Yesu mwambie apeleleze moyo wako akague kama kuna njia za majuto., Daudi alikuwa ni mtu anayeupendeza moyo wa Mungu lakini daudi huyo alitembea na mke wa mtu, kwa nini Mungu alimpenda Daudi alikuwa ni mtu wa kutengeneza na Mungu akusubiri kuambiwa umemkosa Mungu alimtafuta Mungu akamweleza chunguza moyo wangu, kagua ndani yangu kama kuna njia ambayo sio nzuri ni tengeneze niumbie moyo safi moyo wa kukupendeza.

Unataka kuwa mtu ambaye unaupendeza moyo wa Mungu kuwa mtu wa toba usisubiri injini imekufa ndo uende kwa Mungu hapana nenda tu mwambie Mungu nimekuja kufanya checkup ya moyo wangu kama kuna makando kando ayaondoe tenga muda wa kukaa na Mungu na Mungu akusaidie
 
Jitahidi hii injili iwafikie zaidi Vijana, maana wao ndiyo wapo kwenye risks zaidi

Sisi Wazee kitambo miili yetu na nafasi ipo checkup

Ndiyo wakati ambao, tunauza tulivyonavyo ili kusaidia injili kusonga mbele
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom