Siku saba za uchunguzi wa moto sokoni Kariakoo zinaanza kuhesabiwa lini?

walimuomba tena siku saba nadhani,alilisema hili juzi alipoenda kuswali swala ya Eid pale kariakoo msikiti wa mtoro.
 
Waziri Mkuu kawaongezea siku saba tena. Amesema jana alipokuwa kwenye Msikiti wa Mtoro.
Halafu elewa historia ya Msikiti wa Mtoro,hotbed of revolution.
 
haifahamiki walianza lini kuhesabu ila taarifa iliyopo ni kwamba waliomba waongezewe muda ili wale posho zaidi.
 
Mkuu zingatia mtu alietoa hizo siku saba ni nani. Huyu ni yule yule ambae aliongea na marehemu na kutuaminisha kuwa ni mzima wa afya.
Hii nchi ni ya mhemko na maigizo. Keshapata kiki aliyoitaka kwa kipindi husika sasa maisha yanaendelea.
Na siku wakikosa pa kupigia hela za bia watakuja tena na kuunda tume mpya ya kuichunguza tume ya sasa inayochunguza moto wa kariakoo, wakilipana mabilioni ya pesa kuchunguza wachunguzi wanaochunguza sasa. Only in Tanzania.
 
Hivi ile ripoti ya uchunguzi wa ajali ya lori la mafuta kuwaka moto morogoro 2019 ilitolewaga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…