Moto wa Kariakoo mwenye kituo cha Big Bon achunguzwe

rushanju

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
3,131
4,620
Mimi katika uchunguzi wangu, ningeanza na mwenye kituo Cha Bigbon cha KARIAKOO.

Yeye alihisi nini mpaka kufunga kituo hiki siku chache kabla ya moto kuteketeza hilo eneo?

Kwa haraka mtu wa kawaida anaweza kumhusisha mwenye hicho kituo na huo moto.
 
Muda mrefu huyo jamaa alikua anatransform hilo eneo toka sheli hadi frame za biashara, upande wa Mkunguni tayari alishtoa Frame za kutosha na upande wa Mafia kulikua na frame mpya zinajengwa, pia upande wa sheli alikua anajenga Ghorofa.

Viframe vidogo tu anakodisha milioni 2 kwa mwezi hilo eneo Hot, kuliko Kupambana na Mafuta ambayo Dola ikiadimika tu ni matatizo jamaa kaamua atoe frame, kavijaza kibao pengine hata milioni 50 na zaidi anapata kwa mwezi.

Labda na wewe utuambie anafaidika nini akiunguza frame zake mwenyewe?
 
Mchongo tu huo baada ya kituo Cha mafuta kuhamishwa ndo umetokea. Mipango ni kuwa matajiri wanalitaka eneo la mnadani lililopo nyuma ya big bon ni eneo ambalo liko hot Kwa biashara.
Refer soko la Kariakoo lilivyoungua wengi humu mulipiga kelele ni michongo ya matajiri kuondoa watu ili walitumie hilo eneo. Sasa hivi soko lina karibia kuisha kujengwa tena, Soko zima limejaa meza za Nyanya na Vitunguu hakuna Cha Tajiri wala mdogo wake tajiri, wanarudishiwa wale wale walio kuwepo na waraongezwa wengine hao hao wauza Nyanya.

Hapo Bigbon kuna Frame kwa mania hakuna ataesimamisha biashara yake kipuuzi tu kisa eneo, yaani mabilioni ya hela yasimame kisa tu kiwanja.
 
Haya matukio ya moto wa kariakoo yamelivua nguo na kuonesha uhalisia wa jeshi la zima moto, sasa kama moto unatokea hapo ambako ni pua na mdomo kufika kwenye ofisi zao na shida imekua hivi, vipi kama moto ukitokea koromije au kigoma huko mwisho wa dunia kitapona kitu kweli 🤔🤔 serikali iweke pesa ya kutosha kwenye hii idara ili kuitengeneza upya na kisasa zaidi inatia aibu
 
Mimi katika uchunguzi wangu, ningeanza na mwenye kituo Cha Bigbon cha KARIAKOO.

Yeye alihisi nini mpaka kufunga kituo hiki siku chache kabla ya moto kuteketeza hilo eneo?

Kwa haraka mtu wa kawaida anaweza kumhusisha mwenye hicho kituo na huo moto.
 
Mimi katika uchunguzi wangu, ningeanza na mwenye kituo Cha Bigbon cha KARIAKOO.

Yeye alihisi nini mpaka kufunga kituo hiki siku chache kabla ya moto kuteketeza hilo eneo?

Kwa haraka mtu wa kawaida anaweza kumhusisha mwenye hicho kituo na huo moto.
Mi kuna kitu nahic ila nakaa kimya
 
Back
Top Bottom