Siku muungano ukivunjika Tanganyika itapata hasara kubwa sana

Tanganyika ilikuwa na mipaka yake kabla ya muungano, muungano haujabadilisha mipaka, hizo hadithi za sijui tutapara hasara ni aina ya mazungumzo ya kipumbavu
 
Kwanza tuanze kwa kuzungumza kuhusu sheria za mambo ya bahari. Sheria za kimataifa zinasema kuwa kutoka Pwani ya nchi hadi nautical miles 12(22Km)kuingia baharini(1NM=1.85km). Ni eneo la bahari la nchi husika. Yaani hapo nchi inamiliki kila kitu. Hata meli haziruhusiwi kusafiri bila ruhusa.

Pia sheria inasema kuwa 200NM yaani 370Km kutoka Pwani kuingia baharini ni eneo la uchumi la nchi husika. Hilo linamaanisha kila kitu kilichopo chini ya bahari. Samaki, mafuta, gesi nk ni vya nchi husika. Lakini nchi haimiliki uso wa bahari hivyo meli zite zinaruhusiwa kusafiri juu ya bahari.

Kwa mujibu wa sheria hii, hata ukiwa na kisiwa ambacho hakifiki hata eka moja, basi kilomita 370 kuelekea kila upande kutoka kisiwani hapo ni eneo lako la bahari. Hii sheria ndiyo inafanya Ufarsansa kuwa nchi yenye eneo kubwa la bahari kuliko zote duniani sababu inamiliki visiwa vingi sana.

Sasa tuone Tanganyika na Znz zilivyokaa.


Kati ya Tanganyika na Zanzibari mpaka wa bahari utakuwa katikati yao. Yaani watachukuwa visiwa vya magharibi kabisa vya Zanzibari na vya mashariki kabisa vya Tanganyika na kuweka mpaka katikati. So kuanzia Mpaka na Kenya hadi kufika karibu na Mafia, Tanganyika watakuwa na bahari ambayo upana wake haifiki hata km 50. Zanzibar wao upande wa Mashariki bahari yao itaenda kwa kilomita 370, labda wakutane na eneo la bahari la visiwa vingine Sheria hii.

Kitu kingine. Unaona hako kadoti kabluu kati ya Zanzibar na Mafia. Hicho kinaitwa kisiwa cha Latham. Ni mwamba tu usiokaliwa ila una nguvu kuamua eneo la bahari la nchi. Zamani kisiwa hicho kilikuwa chini ya Tanganyika kama ilivyo Mafia. Maana yake mpaka wa bahari wa kusini kati ya Tanganyika na Zanzibar ungekuwa kati ya Unguja na kisiwa hicho. Lakini sasa kisiwa hicho kinamilikiwa na Zanzibar. Maana yake mpaka wa kusini wa bahari unakuwa kati ya Kisiwa hicho na Mafia na kuongeza eneo la bahari la Zanzibar kwa sehemu kubwa.

Pia kuna sehemu ndogo ya bahari ya Tanganyika itaenda Kenya. Sababu mipaka ta bahari inafuata angle ya jinsi mpaka wa nchi kavu unavyoingia baharini. Ndiyo maana huku kusini Msumbiji inaingia kwetu kwenye eneo la bahari sababu mpaka umeelekea Kaskazini Mpaka wetu na Kenya umeelekea kusini. Lakini sababu Pemba ipo pale inafanya mpaka ukifika baharini unyooke kuelekea mashariki. Lakini siku Zanzibar ikiwa nchi kamili, pale juu mpaka itabidi uchorwe upya na sehemu ya Tanganyika itachukuliwa ba Kenya. Labda Tanganyika iwe na visiwa kule Tanga vitakavyolinda eneo lake la bahari.

So kuvunjika kwa Muungano wetu kila mtu atapoteza, lakini Tanganyika itapoteza pakubwa sana.

Tuulinde Muungano kwa nguvu zote, maana nje ya muungano ni vurugu na hasara kwa kila mtu.

IMG_3570.jpg

sasa ww n wakili gan washetan huna akili??
 
Mwandishi Asibezwe ana Hoja!
Kwa kiasi kikubwa yupo sahihi!
Yupo sahihi Muungano ukivunjika Bara itaathirika Kiusalama na Kiuchumi.
Sheria ya Mipaka ya Bahari Kuu inatoa faida zaidi kwa zanzibar dhidi ya Bara, huo ni mkweli mchungu.
bandari ya Zanzibar itakuwa lulu, wakati Bandari za Tanga na Dar zitapoteza mvuto.
Hata hivyo Zanzibar nayo itaathirika Kiusalama na Kiuchumi kwani ni mtegemezi mkubwa wa chakula, nishati na Biashara wa Bara. bila Bara ZnZ haitakuwa na soko. Pia inaitegemea sana Bara kiusalama.
Hofu yangu kubwa ni kuwa Kisiwa kinaweza geuka kuwa pango la magendo na kila aina ya crimes za hatari jambo litakalofanya Bara nayo iathirike.

Kimsingi Muungano una tija nyingi kwa pande zote mbili. Kuvunjika kwake kutakula kwetu pande zote.
Cha muhimu ni uwazi na wananchi wapewe fursa ya kuainisha aina ya muungano wautakao, tusilazimishane.
 
Back
Top Bottom