Siku mbili za Halima Mdee rumande Oysterbay

Siku mbili za Halima Mdee rumande Oysterbay

SIKU MBILI ZA HALIMA MDEE RUMANDE OYSTERBAY
Usiku wa kuamkia leo tarehe 6 Julai, 2017 ni usiku wa pili wa kulala korokoroni Mwenyekiti wa BAWACHA taifa, Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Kawe CHADEMA Halima James Mdee.

Katika rumande ya Polisi Oysterbay wilayani Kinondoni, Mdee ameendelea kutumikia masaa 48 aliyopewa na Mkuu wa Awilaya ya Kinondoni Ally Hapi kwa kosa la kumdhihaki Mh. Rais Dr. John Magufuli na kutoa maneno machafu yanayoweza kuvunja amani.

MATAMSHI YA MDEE
Akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya CHADEMA Mdee ananukuliwa kudai kuwa Mh. Rais Magufuli amekua na "tabia ya hovyo...", "...ipo siku ataagiza watanzania (wake kwa waume) watembee vifua wazi...". Maneno mengine ni "...Rais lazima afungwe breki...",apewe semina elekezi n.k.

UCHOCHEZI
Halima Mdee anatajwa kutoa kauli za uchochezi kama vile "...woga wetu wananchi ndio unaotugharimu nchi hii..." "...watakaomfunga breki ni nyinyi wananchi...", maneno yanayotajwa kupandikiza na kuhamasisha chuki na vurugu kwa wananchi.

KUKAMATWA KWAKE
Baada ya amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mdee alianza harakati za kutoroka na kuruka mtego wa Polisi. Hata hivyo Jeshi la Polisi Kinondoni lilimkamata akiwa amejificha nyumbani kwa mama yake Kibamba wilayani Ubungo tayari kwa kutoroka.

RUMANDE
Halima Mdee anatajwa kuhifadhiwa katika rumande ya watuhumiwa wa uhalifu wa jinsia ya kike katika kituo cha Oysterbay Kinondoni.

BUNGE KUMUWAJIBISHA TENA
Akiwa bado anatumikia kifungo cha kutohudhuria Bunge hadi mwaka 2018, Halima Mdee ameingia tena matatani.

Kufuatia matamshi ya Mdee na waandishi wa habari Makao Makuu ya Chadema, Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza kamati ya Kinga na Madaraka ya Bunge kukutana haraka kujadili kitendo cha Mbunge huyo kutoa matashi ya kulifedhehesha Bunge. Akikutwa na hatia huenda akaongezewa adhabu nyingine.
Kulifedhehesha Bunge kwani aliongea kama Mbunge au kama Mwnyekiti wa BAWACHA? huyu redio sasa kachanganyikiwa
 
Mwanamke jembe sana huyu.Anaongea mambo ambayo wanaume na suruali zao wanaogopa.Wababaki kujichekesha chekesha tu..Bravo Halima
 
Kwani huwezi kukosoa au kupinga kwa staha? Mbona akina Zitto hawajawahi kukutana na heka heka kama akina Mdee..
Hukumbuki Kahama aliposema njaa tu utawala ulitaka kummeza?! Au Zitto yupi unamuongelea?!
 
Kwenye hayo maneno ya Mdee ni wapi alipomdhihaki Rais?
Kwasababu wewe ni shabiki ni vigumu kuelewa. Wangekuwa wanafanya siasa zenye ushindani na tija sizani kqma wangekuwa wanapitia hali hii. Lqkini upizani utasikia mara nimeoteshwa rais atakufa mara nitawahamasisha wanawake watembee kifua wazi. Ivi kweli kwa akili ya kawaida mwanamke gani hapa Tanzania anaweza kutembea kifua wazi kama Halima anavyoamanisha wengi. Lete sera mzuri ueleweke si bla bla na matusi.
 
Kwasababu wewe ni shabiki ni vigumu kuelewa. Wangekuwa wanafanya siasa zenye ushindani na tija sizani kqma wangekuwa wanapitia hali hii. Lqkini upizani utasikia mara nimeoteshwa rais atakufa mara nitawahamasisha wanawake watembee kifua wazi. Ivi kweli kwa akili ya kawaida mwanamke gani hapa Tanzania anaweza kutembea kifua wazi kama Halima anavyoamanisha wengi. Lete sera mzuri ueleweke si bla bla na matusi.

Siasa za ushindani? Hivi Rais si kazuia siasa? Huo ushindani unatoka wapi? Tatizo lenu mna uwezo wa kufikiri kama wa bata.
 
Siasa za ushindani? Hivi Rais si kazuia siasa? Huo ushindani unatoka wapi? Tatizo lenu mna uwezo wa kufikiri kama wa bata.
Bora ufikiri kama bata kuliko kuwa nyumbu. Raisi amekataza siasa wapi ni lini Mdee ameenda kwenye jimbo lake akakatazwa kuongea na wananchi wake? Tatizo nyumbu mnaishi kwa kukariri. Kuna nama nyingi sana za kutoa ujumbe mbona Zitto kila siku anaikosoa serikali lakini hajawahi kukamatwa? You have to think big my friend.
Siasa siyo matusi, ukitumia lugha za kistarabu ujumbe wako utafika to na utagusa watu wengi pia utajijengea heshima kwa wananchi wako hata taifa kwa ujumla. Lakini kwa sababu nyumbu wao wanachokijua ni matusi basi endeleeni na matusi tutakutana segerea na central
 
Ndio sheria kandamizi hizi ambazo makoloni aliziacha na bado magamba wanazikumbatia ili kiwakomboa wapinzani halafu wanasema huyu rais hana mfano ni wa kuigwa eti Africa.
Ni moja kati ya makosa yaliyoachwa maksudi ili kukifeva CCM na viongozi wake. Katiba mpya ya wananchi ni muhimu
 
Mwandishi wa habari Happiness Katabazi,aliwahi kubashiri anguko la Mdee kwa usela mavi wake,miaka mitatu nyuma
 
Sishangai wengi humu kuunga mkono upuuzi wa Mdee maana hata alivyomtusi Spika 'acha Ufala' mlishangilia sana.
Kuna kosa kubwa kma kujeruhi mtu kwa rungu la utosi,ila kwa vile yeye chama kijani wakapotezea... acha ushabiki maandazi mlangira
 
Kuna kosa kubwa kma kujeruhi mtu kwa rungu la utosi,ila kwa vile yeye chama kijani wakapotezea... acha ushabiki maandazi mlangira
Nimemuliza Swali gamba mmoja humu khsu hilo la kumshambulia mwenzake hyo spk mpaka sasa hajanijibu?
Kama jamaa ni clean kwann alimpiga mwenzake rungu hadi akazimia wao wanaona sawa

Ova
 
Umeweka mtiririko mzuri na binafsi sikujua kama alikamatiwa kwa mama yake na kitendo cha kuwa kwa mama yake ni namna mojawapo ya kutaka kutororka.
Jambo moja ni wazi nalo ni kuwa kila mtu anataka kumfurahisha Mheshimiwa Raisi kwa kadri inavyowezekana.Wateule wote wameshasoma ni kitu gani ambacho aliyewateua anataka na wanaitumia nafasi hiyo kiukamilifu,ni jambo jema kwani wanajihakikishia kula kwao na wapendwa wao.
Mkuu wa wilaya ametumia mamlaka yake kikatiba na tunaamini saa 48 zitaisha na atatoka sasa tuangalie huyu wa Dodoma naye kimemuumiza nini?Hivi kweli kwa matamshi hayo ukilinganisha na yule aliyesema bungeni watu wanalala tu ni nani kaliabisha bunge zaidi?
Binafsi naomba JPM asimame tena katika uchaguzi wa 2020 na upinzani wapate wabunge wachache mno na ikiwezekana wakosekane kabisa, si ajabu tukapiga hatua kubwa mno katika nchi hii.

....Kwa nini unahangaika kuzunguka mbuyu mara Rais gombea 2020, mara wabunge wa upinzani wawe wachache....Si na wewe uanzishe maandamano ya kutaka vyama vingi vifutwe ili tuone utavuna nini hasa?? Yaani mnavyohangaika it is as if since independence hii nchi iilikuwa inaongozwa na opposition.....
 
Ub
kisu cha ngariba: kama una ubavu, vua koti la hiyo ID, utoke hadharani uyasema maneno ambayo wewe unaamini ni sahihi kuyasema ukimshbulia Rais.
Ubabe, kutisha watu, uonevu, uongo, unafiki... ndio mambo mnayoweza tu! Pathetic!!
 
Halima Mdee lazima abadilike, watanzania sasa hivi hatutaki siasa za chuki. Hata kama Rais anakosea, kuna njia nzuri za kumpinga lakini sio kama wabunge wengi wa upinzani wanavyofanya.
Sema wewe n.a. si watanzania.
Hujawa msemaji wa wa-Tz
 
Hata kama Rais ana element za siasa za chuki lakini sio kwa kushambuliwa kwa namna wanavyofanya wapinzani. Rais ni taasisi kumbuka.
Anasahmbuliwa au anaambiwa ukweli.... hiv jaman kushambiliwa kukoje.... hapa tz wap wenye siasa za chuki kama ccm?.. sasa tunaelekea kua kenya au rwanda sidhan kama mnaliona ilo
 
Nimemuliza Swali gamba mmoja humu khsu hilo la kumshambulia mwenzake hyo spk mpaka sasa hajanijibu?
Kama jamaa ni clean kwann alimpiga mwenzake rungu hadi akazimia wao wanaona sawa

Ova
Huyu atakua ndgu wa mwijage yeye mfuata upepo,hela za rambirambi zilivyoliwa sikumuona akiongelea hpa,ukiwa gamba akili inakua matope
 
Back
Top Bottom