Siku mbaya JF

Sijawahi kuwa na siku mbaya mimi, mtu akileta ubaya nakwenda nae hivyo hivyo muhimu kutocheza rafu ndani ya 18 na kusababisha penati ( ban).
Nikiona vipi naenda zangu kushinda instagram huko au sportpesa.
 
Hivi ni kipi kinachokusukuma mpaka unamtupia mtu lugha mbaya?
 
Huwa namjibu mtu kulingana na hoja husika tofauti na hapo nikiona anakoelekea sio kuzuri huwa sijibu chochote.
Huo ndiyo ustaraabu.

Nilichojifunza hapa jf, kuna memba wengi hasa jukwaa la siasa wana uwezo mdogo wa kujibu hoja.

Wengi wanasukumwa na mapenzi yao kisiasa.
Wanajisahaulisha kuwa JMIIFORUMS ni uwanja wa hoja.
 
Ignore list yangu ina watu 28.
Nikiona nimekerana na mtu kwa kiasi cha kutoleana maneno makali basi ignore inahusika. Ili nisije kukutana nae tena siku nyingine.
Punguza hasira mkuu.
Penye wengi pana mengi, kikubwa ni subra.
Ukiwa na moyo wa subira utawavumilia tu.
 
Huo ndiyo ustaraabu.

Nilichojifunza hapa jf, kuna memba wengi hasa jukwaa la siasa wana uwezo mdogo wa kujibu hoja.

Wengi wanasukumwa na mapenzi yao kisiasa.
Wanajisahaulisha kuwa JMIIFORUMS ni uwanja wa hoja.
Upo sahihi kabisa maana hilo jukwaa ndio linaongoza kwa watu kutofautiana kila mara
 
Ndivyo nilivyo na siwezi badilika.
Subira ni sifa ya kwanza ya uongozi.

Viongozi wengi waliokosa subira na uvumilivu wameangukia kwenye ubabe na udikteta.

Kiongozi mzuri ni yule anayeweza kuzikabili kauli za ovyo za watu wake.
Nina imani kuna siku unaweza kuwa kiongozi wa ngazi ya mtaa, kata, wilaya hata taifa.

Kama itashindikana huko basi utakuwa kiongozi mzuri wa familia ukiwa na subira.
 
Mwanaume ndo kiongozi wa familia.
 
Mwanaume ndo kiongozi wa familia.
Uongozi ni daraja/madaraja.
Kuna maeneo baba anakuwa kiongozi.

Lakini kiongozi mzuri anakuwa na wasaidizi.
Kwahiyo mama anafuata baada ya baba.
Ukiwa na subira utawachukulia watoto ni kama watoto tu.
Ukikosa subira kila kinachofanywa na mtoto utamtandika.
Maana utamchukulia yeye ana akili kama za mtu mzima.
Subira ndiyo dira ya maisha yetu kila mahali.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…