Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,439
- 166,898
Laiti ningekuwa rais, ningetenga siku moja rasmi ya kitaifa, watu wasiende kazini.
Niite siku ya kuondoa dukuduku, kila mtu aseme chochote, hata akitukana sawa tu, aandike, aongee au afanye vyovyote awezavyo, ili tu dukuduku limtoke, asiwe na kinyongo. Kinyongo ni sumu mbaya iuayo.
Maoni ya watu wangu yooote nitahakikisha yanakusanywa, yanachakatwa na mwisho yanatolewa taarifa, uongozi uboreshe wapi, umekosea wapi na ujirekebishe vipi.
Naamini ingekuwa njia nzuri sana ya kulilainisha taifa.
Watu wenye dukuduku lazima wawe na stress, huwezi kufurahia maisha ukiwa stressed, ndio maana Tanzania imo miongoni mwa mataifa ambayo watu wake hawana furaha kabisa.