Siku kama ya leo, Mwaka...

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,490
4,774
Galam galam Aptii...
awali ya yote napenda kuitambulisha thread hii itakayokuwa inatukumbusha na kutupatia habari za Nyota mbali mbali wenye hadhi hapa Ulimwenguni, ama wawe wamefariki au laa wapo hai.

Thread hii itakuwa inatukumbusha yaliopita ama kwa kufanywa ama kwa kusemwa na Famous, Celebrities, Popular na Super Stars mbali mbali ulimwenguni.
katika Thread hii tutakumbushana matukio ya siku husika.

karibuni enyi nyoote...
 
siku kama ya leo Mwaka 1995, huku akiwa kaachia kibao cha "Me Against the World" Tupac Shakur hatimae anakuwa msanii wa kwanza ulimwenguni kushika chati namba 1 za Billboard ile hali yeye akiwa Gerezani.
 
siku kama ya leo miaka 11 iliopita Nas aliachia albam yake iliokwenda kwa jina la “Street’s Disciple”.
 
siku kama ya leo mwaka 2009, Super Pippo Filippo Inzaghi alifunga goli lake la 300 tangu alipoanza kuvizia na kuzifumania nyavu. Goli hilo aliifungia AC Milan ilioibamiza Siena 5-1.

Inzaghi pia ndie mshambuliaji aliefunga goli ktk kila mashindano aliopata kushiriki.

forza Milan
Sempre Pipo
 
Blake Griffin nyota wa NBA ambae ameshapata kushinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi mwaka 2011 ambae kwa sasa anakipiga Los Angeles Clippers leo ni kumbukumbu yake ya siku ya kuzaliwa. alizaliwa tarehe kama ya leo na mwezi kama huu mwaka 1989.

Griffin alichaguliwa kuingia NBA kama mchezaji namba 1 kutoka Chuo mwaka 2009.

anakumbukwa kwa balaa lake alilolifanya pale alipoliruka gari aina ya KIA na kupiga Dunk la khatari
 
siku kama ya leo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Theo Walcott mwanariadha ambae pia ni mshambulia wa Arsenal ambayo leo inaingia kkt Dimba la Nou Camp kupambana na Barca.

ametimiza miaka 27 akiwa na kombe 1 tu
 
siku kama ya leo mwaka 1872 ndio ilichezwa fainali ya kwanza ya kombe la FA nchini uingereza.
katika fainali hio iliozikutanisha Wanderers dhidi ya Royal Enginiers ilishuhudia Wanderers ikiibuka na ushindi wa 1-0 katika Dimba la Kennington Oval mjini London.
 
1996 siku kama ya leo ulimwengu ulishuhudia bingwa wa masumbwi wa uzito wa juu Mike "iron" Tyson akimchakaza kwa TKOs
Frank Bruno ktk round ya 3 na kufanikiwa kutetea mkanda wake.

Aboubakar Mike Iron Tyson kwa sasa anatamba ktk movie alioshirikishwa ya IP Man 3
 
Siku kama ya leo mwaka 2002 mechi dhidi ya aheffield United na West Brom ilivunjika baada ya dakika 82 zilizoshuhudia kadi 3 nyekundu.

balaa lilianza mapema tu dakika ya 9 pale kipa wa United alipotoka nje ya Box na kudaka mpira.
tukio hilo liliwalazimu United kufanya mabafiliko ili kukava nafasi ya mlinda mlango huyo.

West Brom waiutumia mwanya huo baada ya mshambuliaji Scott Dobie kutia kamba mnamo dakika ya 18.

Captain Derek McInnes alitupia kamba ya pili mnamo dakika 63.
manager Neil Warnock alifanya mabadiliko ya wachezaji wawili mnamo dakika ya 64 kiungo Georges Santos na mshambuliaji Patrick Suffo, lakini Santon hakudumu muda mrefu uwanjani. Santos alilambwa kadi nyekundu 65th bada ya kumrukia miguu miwili Andy Johnson. dakika moja baadae Suffo nae akapokea ya kwake.

United wakapoteza wachezaji wawili zaidi baada ya kupata majeruhi.
wakiwa tayari wanekwisha maliza nafasi 3 za wachezaji wa akiba na wamepoteza wachezaji watatu, hivyo wakawa pungufu wachezaji 6, kitu kilicho mwamuru mwamuzi Eddie Wolstenholme kumaliza mchezo.
 
tarehe kama ya leo mwaka 2007 Mkongwe
Kobe Bryant aliifungia LA Lakers points 65 katika ushindi wa 116-111 dhidi ya Portland Trail Blazers
 
hatimae Los Angeles Lakers' rekodi yao ya kushinda mechi zake za NBA ilisimamishwa katika mchezo wa 19 baada ya kukubali kipigo cha pointi 109-102 toka kwa Washington.

rekodi hio ya kucheza game 19 ikawa ktk nafasi ya tatu ya rekodi za timu zilizocheza game nyingi pasipo kupoteza.

hio ilikuwa siku kama ya leo mwaka 2000
 
siku kama ya leo vikosi vya waasi vilifanikiwa kuuteka mji wa Kisangani uliopo Zaire.

majeshi hayo yalifanikiwa kuuteka mji huo muhimu nchini humo na kuelekea kabisa kupata ushindi na kumng'oa raisi wa kipindi hicho Mzee Mobutu Sese Seko.

hii ilikuwa ni mwaka 1997
 
siku kama hii mwaka 1827 gazeti la kwanza la mtu mweusi hatimae likachapishwa.

gazeti hilo lililoitwa Freedom's Journal,
liliingia mitaani kwa mara ya kwanza ktk mji wa New York.
 
Kareem Abdul-Jabbar mchezaji mrefu zaidi wa wakati huo, pengine na sasa ktk NBA aliifungia timu yake ya Milwaukee Bucks pointi 50.

lakini hio haikutosha, kwani walipokea kichapo cha pointi 123-107 toka kwa Los Angeles Lakers.

hio ilikuwa ni siku kama ya leo
 
siku kama ya leo Kobe Bryant nguli wa Los Angeles Lakers anaifungia imu yake hio pointi 50 katika ushindi wa 109 dhidi ya 102 toka kwa Minnesota Timberwolves.

hii ilikuwa mwaka 2007
 
hii ilikuwa mwaka 1988.
siku kama ya leo Michael Jordan alifungia Chicago Bulls jumla ya pointi 50 baada ya kuwaadabisha Boston Celtic jumla ya vikapu 113-103 .
 
Back
Top Bottom