Siku kama ya Leo mwaka 1804 huko Ufaransa bwana Napoleon Bonaparte alijivika Taji kama Kaisari wa Ufaransa

DIDAS TUMAINI

JF-Expert Member
Nov 11, 2014
232
653
Siku kama ya Leo mwaka 1804 huko Ufaransa bwana Napoleon Bonaparte alijivika Taji kama Kaisari wa Ufaransa. Mwaka uliofuata akapewa pia Taji la Mfalme wa Italia.

Vita ya Mapinduzi yake dhidi ya familia ya Kifalme, Huhesabika kama moja ya matukio 10 makuu ya Kihistoria Ulaya.

Mwaka 1805 Uingereza, Urusi na Austria walipatana kushindana pamoja dhidi ya Napoleon kwa sababu waliona mipango yake ilkuwa kutawala Ulaya yote. Jibu lake lilikuwa ni kuandaa jeshi kubwa na kuvamia Uingereza, Katika vita hiyo Ufaransa walichapika vibaya sana katika vita iliyopewa jina "mapigano ya bahari ya Trafalgar" na Ushindi huo ukawapa jina Uingereza kama Wababe wa Bahari zote Ulimwenguni.

Napoleon kwa Ulaya tu aliteka miji mingi kama Berlin, Vienna, Prussia. Mwaka 1907 Urusi wakakubali kuacha vita dhidi yake, hivyo akawa ndio Mtawala mkuu katika nchi zote za Ulaya isipokua Uingereza, Uswidi pamoja na Nchi za Scandinavia na Uturuki, nchi hizi zililazimishwa kusaini mikataba ya kusaidiana nae.


Picha ya pili ndio Kaburi la Bwana Napoleon Bonaparte lipo ndani ya kanisa linaloitwa "Dome des Invalides" huko Ufaransa.

Licha ya Ubabe wake na Akili zake, Jamaa mwisho wake ulikua mfupi sana, Unajua ilikuaje?

Jamaa katika utawala wake, Alizikataza kabisa nchi za ulaya ambazo zoko chini yake, Kufanya biashara na nchi ambazo hazipo chini yake, Moja wapo ni Uingereza.

Lakini mwaka 1810 Nchi ya Urusi ambayo ilikua chini yake ikaanza kufanya Biashara na Uingereza, haya yalikua ni maamuzi ya Kaisari Alexander wa Urusi.

Mwaka 1812 Napoleon hakutaka maneno mengi, aliivamia Urusi akiwa na Wanajeshi takriban 600,000 na Kuiteka Moscow, vita hii hakufaulu, Maana raia wa Moscow walichoma moto nyumba zote za mji huo, Na kipindi cha Baridi kilikua kimeshafika, hivyo Napoleon alikosa chakula na Mambo mengine muhimu.

Akaamua kuondoka na Kurudi Ufaransa, njiani alivamiwa na Jeshi la Urusi, akachakazwa vibaya na kubakia na wanajeshi 40,000 tu, alipofika Ufaransa, Paris Uingereza nao wakavamia mwaka 1813 yaliitwa "mapigano ya Leipzig" haya mapigano ndio yalimaliza nguvu ya Ufaransa.

Mwaka 1814 Napoleon alijiuzuru, Washindi wa Vita ambao ni Uingereza, Urusi, Austria na Prussia hawakutaka Kumfunga bali wakampa kisiwa cha Elba akae kwa Heshima huko, na akatawala kama mtemi, Mataifa yote ya ulaya yakakutana mjini Viena ili kujadili kurudisha Utawala na Mipaka kama ilivyokua mwanzo haijaharibiwa na Napoleon.

Lakini Napoleon hakuridhika, Alirudi tena Ufaransa na Kupigana na Kushinda tena, Akawa Mtawala kwa Siku 100 tu, Uingereza ilijipanga na Kumrudia, Vita ilipigwa huko Ubelgiji ya Leo, na Uingereza ikashinda.

Waingereza hawakutaka tena kumuona Napoleon Ulaya, wakampeleka kisiwa kinachopatikana pwani ya Africa kinachoitwa Saint Helena, na akafariki mwaka 1821 kwa kuwekewa sumu kwenye Chakula.

Miaka 20 baada ya kifo, maiti yake ilikuja kufukuliwa na Wafaransa Na kwenda kuzikwa kwa heshima, mahali hapa.

Polycarp Mdemu
FB_IMG_1701517134420.jpg
FB_IMG_1701517287420.jpg
 
Back
Top Bottom