Siku hizi wanaume ndio wanaolia msibani

Siku hizi wanaume ndio wanaolia msibani

Hivi unategemea nn mwanaume kaenda msibani kasuka rasta mpaka kiunoni na hereni Juu hasilie???....nimeshangaa wema kavaa sket na mtandio na full black glass kaja msibani kasaini kitabu kabaki anakodoa tu....vijianume vya dar kamasi kisado
Hahahahahaaaaaaaa mbona kamasi KISADO!!!!
 
Mwanaume katika msiba(baba, kaka,mjomba,binamu wa marehemu) kwa jinsi nilivyolelewa ndiye mleta faraja wa kwanza kwenye msiba. Yeye (akishirikiana na kamati zitakazoundwa kufanikisha mazishi) ndiye anaijua nyumba na atatoa maelekezo mwili wa marehemu uhifadhiwe wapi, chakula kitaandaliwaje na kwa watu wangapi, wageni watapokelewaje,marehemu atazikwa wapi, nani ataandaa risala ya marehemu (eulogy) n.k. Wanaume wengine kutoka nje ya familia watakuja kutoa support ya kujenga mahema, kuandaa jiko la muda, kuandaa wachimba kaburi, kununua jeneza na kufanya taratibu za kuutoa mwili hospitali n.k.

Kwa yote hayo niliyotaja hapo juu mwanaume anakuwa na muda mdogo wa kulia ila simaanishi hauzuniki bali anahuzunika na anaomboleza kwa majonzi. Ila akilia kuanzia asubuhi mpaka usiku anakata matumaini hata kwa wale waliotamani asimame imara katika wakati huo mgumu nikimaanisha watoto, mke na hata ndugu wengine.

NB: Ikumbukwe pia wakati wa misiba maeneo mengi ndiyo vibaka huiba kiurahisi hivyo jukumu la ulinzi wa nyumba bado lipo kwa mwanaume haijalishi una njaa, msiba ama harusi. Na wanaume wanaokuja kufariji nao wana jukumu hilo la kumsaidia mwenzao ili majukumu yasimlemee. Mwanaume lia ila usisahau yote hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka miaka mi5 nyuma wakati mzee wangu amefariki my girlfriend aliniambia usionyeshe udhaifu wako mbele za watu ukitaka kulia lia sana ukiwa kifuani kwangu au mabega yangu lakini mbele za watu be strong wewe ni mwanaume.
Asee nilijikaza lakini the time wamefunua jeneza nikajikuta machozi hayo bila taarifa. [emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaaa mbona kwanzia hilo jina lako Ni langu.. Na story yako Ni yangu kabisaaaaaaaa yani nilikaza kabisa mpka nafika pale kusogea karibu Zaid nasema it's ouk, fine, it's OK, fine.. Aaaaargh sijui hata machozi na mafua yalitokea wapi.. Kwakweli chozi halikuniacha salama..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ilinikuta mm baba yangu mlezi anafariki ndyo natoka depo mzee nimeshavaa kivazi wazeee mmeelewa nilipofika msibani msiba ndyo ukazidi kiukwel baba yangu mdogo ndyo alinilea nilipofika pale nikakumbuka wema aliyonitendea kamanda pale pale nilishidwa vumilia niliangua kilio sana ase hii inatokea ata mm sikuamini.R.I.P ba mdogo wangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jinsi ya kulia KIUME!
Mwanaume unatakiwa uji control. Unaweza usiweze kuzuia machozi, ila unaweza kabisa kujizuia usigalegale chini au usipige ukunga na pia unaweza kuzuia makamasi yasikujae usoni kama mtoto wa chekechea..! Ukishindwa kabisa, sogea pembeni jifiche sehemu lia weee.. then jiweke fresh rudi kwenye kadamnasi.
 
Sisi wa mikoani bado hizo shughuli tunaendelea kuzifanya mpaka kesho. Ila hadi muda huu bado tumeshikwa na mshangao tunapowaangalia huko Dar kupitia runinga, namna wanaume wanavyolia kwenye huo msiba wa Ruge!

Tunawaona wengine hata kutembea wanashindwa! Eti wanasaidiwa kama wanavyofanyiwa wake za marehemu huku mikoani tuliko
Kumbe alikuwa na mke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We jamaaa mbona kwanzia hilo jina lako Ni langu.. Na story yako Ni yangu kabisaaaaaaaa yani nilikaza kabisa mpka nafika pale kusogea karibu Zaid nasema it's ouk, fine, it's OK, fine.. Aaaaargh sijui hata machozi na mafua yalitokea wapi.. Kwakweli chozi halikuniacha salama..

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuvumilia kumuona mtu wako wa karibu mle ni ngumu sana mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi unategemea nn mwanaume kaenda msibani kasuka rasta mpaka kiunoni na hereni Juu hasilie???....nimeshangaa wema kavaa sket na mtandio na full black glass kaja msibani kasaini kitabu kabaki anakodoa tu....vijianume vya dar kamasi kisado

Hahaaa mkuu we ukishaona mwanaume anadiriki kukaa kwenye kiti anaweka miguu kwenye beseni halafu mwanaume mwenzie anamuosha miguu, anamsugua na kumkata kucha, anampaka mafuta mpaka kwenye mapaja... Hapo kuna mwanaume kweli?
 
Kuna jinsi ya kulia KIUME!
Mwanaume unatakiwa uji control. Unaweza usiweze kuzuia machozi, ila unaweza kabisa kujizuia usigalegale chini au usipige ukunga na pia unaweza kuzuia makamasi yasikujae usoni kama mtoto wa chekechea..! Ukishindwa kabisa, sogea pembeni jifiche sehemu lia weee.. then jiweke fresh rudi kwenye kadamnasi.
Umenikumbusha petro alivyomlilia Yesu alijificha ukutani akaliaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom