Siku hizi wanaume ndio wanaolia msibani

Siku hizi wanaume ndio wanaolia msibani

Sisi wa mikoani bado hizo shughuli tunaendelea kuzifanya mpaka kesho. Ila hadi muda huu bado tumeshikwa na mshangao tunapowaangalia huko Dar kupitia runinga, namna wanaume wanavyolia kwenye huo msiba wa Ruge!

Tunawaona wengine hata kutembea wanashindwa! Eti wanasaidiwa kama wanavyofanyiwa wake za marehemu huku mikoani tuliko
Wanaume kwenye runinga tunangalia mpira. Wewe unaangalia tamthilia na mazishi
 
Wanaume kwenye runinga tunangalia mpira. Wewe unaangalia tamthilia na mazishi

Mgosi asubuhi karibia midia zote zilikua mubashara kurusha taarifa za huo msiba hivyo kuangalia hiyo habari ya kumuaga Ruge ilikua haikwepeki. Hii jioni kama kawa wengi tulihamia Azam sports 2 kuingalia timu ya wananchi ikicheza na timu ya wanafunzi wa Alliance academy.
 
Mgosi asubuhi karibia midia zote zilikua mubashara kurusha taarifa za huo msiba hivyo kuangalia hiyo habari ya kumuaga Ruge ilikua haikwepeki. Hii jioni kama kawa wengi tulihamia Azam sports 2 kuingalia timu ya wananchi ikicheza na timu ya wanafunzi wa Alliance academy.
Kumbe upo timu ya Wananchi. Big up!
 
Nakumbuka miaka mi5 nyuma wakati mzee wangu amefariki my girlfriend aliniambia usionyeshe udhaifu wako mbele za watu ukitaka kulia lia sana ukiwa kifuani kwangu au mabega yangu lakini mbele za watu be strong wewe ni mwanaume.
Asee nilijikaza lakini the time wamefunua jeneza nikajikuta machozi hayo bila taarifa.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dunia inaenda kasi sana ,zamani wanaume kazi yao kubwa msibani ilikuwa ni kuchimba kabuli,kumstili marehemu kumbemba na kwenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya Milele ,

Kulia,kupika ,kuchota maji Na inshu ndogo ndogo ilikuwa ni kazi ya kina Mama,


ila siku hizi sasa wanaume kazi yao ni kulia Na kulegea Na wanawake kuja kutoa pole.

Wanaume wamekuwa soft sana siku hizi hivi mwanaume Yule anaelia msibani siku akifiwa ata Na mwanae ataweza kwenda kumstili marehemu,kumuosha,kumvika Na kumuweka kwenye jeneza.


Wanaume we are under attack ipo siku isiyo Na jina wanawake watatupokea kazi hizi.

Zero IQ
Wanaume wa dar ndio wanadhalilisha wanaume. Unamvalisha pete mwanamke unapiga magoti na kulia alafu mwanamke anakuangalia downwards, uko msibani unalia wanawake ndio wanakubembeleza. Hovyo sana wanaume wa dar.
 
Kama kufiwa na rafiki tu mtu analia hadi anatepeta je akifiwa na mzazi sindo mtu naye atakufa kabisa.kwasababu sidhani kama rafiki au boss ata kama ana mchango vip kwenye maisha yako anaweza kufikia hadhi ya mzazi.Hao wanaume wanaolia hadharani hadi kutepeta huo ni uzwazwa.
Mmmh kwa mtazamo wangu swala la kulia msibani sio swala la kuwa mwanaume wa mkoani au wa Dar hii ni jinsi gani kifo cha marehemu kimekugusA. Ruge alisaidia wengi mno hiyo itabaki kuwa privacy yao na marehemu quote toka kweny familia " Ruge cared much about the society around him than his family." Sasa familia imeona matundA yake. So hii inaonyesha jinsi gani watu walio fanya nae kazi Akatoa misaada ya dhati kwa jamii yake leo hii Ruge hayupo kwanini kama kwel una moyo wa kiuana damu usilie kwa kifo chake? Kwa mtu baki ata ona ni mtu wa kawaida ila kwa mtu anaye tambua mchango wa Ruge lazima utaliA mno labda usiwe na Moyo huu wa damu na nyama.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Back
Top Bottom