Siku hizi undugu ni ‘overrated’

Yaani acha kabisa mpango wangu mwakani nibaki na wanangu wawili tu ndugu tupa kulee!!!kwanza wanaafiki watupu unawasaidia halafu wanakusemanga!big up nyote mnaoishi na watoto wenu tu! Nuclear family ndugu kulostishana tu.
Ndugú(wa damu) mnàsengenyana? Au una maana ya extended ndugu?
 
Kwa taarifa yako tu nchi zilizoendelea wanathamini sana hizi siku ambazo nyny mnasherehekea kwa kupost juu juu tu happy mothers day wazungu wanajumuika pamoja nyumbani kwa mama au bibi siku za watoto wanajumuika pia pamoja hawana undugu wa kushinda kwa ndugu kuvizia chakula ila wanakumbukana mara kwa mara katka zile siku za maadhimisho
Mkuu kwani undugu tunaozungumzia ni wa kushinda kuvizia chakula?? Hahahaa inaonekana una uchoyo. Ndio huohuo wa kujumuika pamoja na kusaidiana wakati w shida. Wenzetu wazungu wanainuana sana. Sisi huku ukijaliwa kupata basi unataka uonekane wewe ndio mwamba ili ndugu wakupigie magoti. Sio hivyo.
 
Imenikuta hiyo mkuu! Unahangaika na ndugu alafu wanakunafikia...tupa kule . Ndugu zako ni wanao tu
Pole mkuu inaonkeana ndugu zako wamekumiza sana. Lakini pia huenda tatizo sio ndugu zako likawa liko kwako. Mfano unaweza ukawa Kaka kwenye familia let say wewe ndio mtoto wa kwanza na ukawa unategemewa kila kitu. Ukajitoa kimasomaso kuhangaika sana ili kuwasaidia wadogo zako na ndugu wengine.

Ukahakikisha mpaka unakwama kimaendeleo yako kwa ajili ya ndugu zako. Wakati ukifanya hivyo at the end ukaoa mke au ukabadilika kitabia. Ndugu wale uliowasaidia wakakushauri jambo fulani au la kubadilisha tabia zako. Kwakuwa wewe ndio uliwasaidia ukawa mkaidi na hisikilizi na baadae ukaanguka uchumi wako ukafa au kushuka sana. Mke wako akawa mbogo kushambulia ndugu.

Hapa ndipo utaanza kujuta na kulalamika ooh ndigu zangu niliwasaidia lakini wao wamenitupa na kunisengenya. Unasahau kuwa ulianza vizuri kwa moyo wa upendo ukamaliza vibaya mno. Yanapokukuta inataka kuwaunganisha na wao kisa tu uliwasaidia. Kisa tu ulijitoa hadi uhai wako kwa ajilo yao. Lakini ukasahau ni wapi ulipoanguka na ndugu zako hawahusiki. Mifano ni mingi huku Uraiani
 
Huu ndio ujinga hapo huoni kama ulioa mzigo
Yaani kijitu mmekutana at 20's ndio aje kunigombanisha na chalii yangu niliyedokoa nae mboga utotoni

Haitokaa ikatokea kamwe
Kwa kweli haipaswi kuw hivyo. Mke anabaki kuwa mke na ndugu wanabaki na nafasi yao.
 
Aisee tunapokuja kuzungumzia dada kaka mama baba nk
Hawa ni ndugu zangu na yote nnayopambania ni ili tuje kupata faraja ya mbeleni.
Napenda sana ndugu zangu.
Sahihi kabisa mimi binafsi bado najuta hadi leo kwa kuwa ilipita fursa sikuweza kumsaidi mdogo wangu wa kike. Alimaliza form four wakati huo mimi niko chuo na nilikuwa nasomesha wagmdogi zangu wengine wengi hivi kama watano hivi. Wakati huo kipato changu kilikuwa kidogo. Nilimweleza kuwa anisubirie kama mwaka hivi ili hali yangu ikiwa nzuri nitampeleka shule. Dogo wangu wa kike akanisikiliza akaendea kumsaidia mama kulima huko kijijini.

At the end miaka miwili ikapita mambo yangu bado tight na huku nina mzigo mwingine wa madogo. Mwisho wa siku mdogo wangu yule akapata mchumba. Akaniambia kaka nimesubiri sana msaada wako lakini naona bado naomba uniruhusu nieolewe. Basi nikamruhusu kwa uchungu sana. Hadi leo ana watoto watatu . Furaha yangu ilikuwa nimsomeshe apate maisha mazuri kwenye maisha yake.

Watu wanaona Ulaya ndugu wana maisha mazuri wanadhani yalijitengeneza. Hapana wanainuana. Undugu ni kusaidiana.kutokana na Choyo ya waafrika sasa wanasingizia Ulaya ya wazungu eti hakuna undugu ili wawatenge ndugu zao.

Wazungu wanapendana mno.
 
Tatizo ni ubinafsi. Siku hizi watu ni wabinafsi sana. Na ukijifanya eti wewe ndio unajali undugu, basi utakiona. Ni kuacha mambo yawe hivyo hivyo tu. Sababu ndg hawakusaidii ila wanakuridisha nyuma tu na ubinafsi wao.
Hii nayo inasikitisha yaani wewe uliyetoka kimaisha kushirikiana na ndugu zako unaona kama wanakurudisha nyuma??🤣

Aliyekuwa bado na maisha magumu matuamaini yake yako kwa ndugu zake wenye nafuu ya maisha. Hata ungekuwa wewe imungekuwa katika nafasi hiyo.
 
Mimi mbona ndugu yangu ndo aliyeninyanyua pale nilipojua mimi ni mgeni sana hapa duniani. Au kisa tupo wachache tu(3)!!!

Hao ndugu zenu inabidi mkapime DNA,labda bi'mkubwa alimpiga changa la macho mzee. Ndugu yako ni yule mliyetoka naye tumbo moja tu.
Tumbo moja lakini vipi iwapo baba mbalimbali? Undugu hapo utakuwa wa mashaka.
 
Mm Niko na miaka 2 no communication na ndugu yangu na hata tukikutana katika matukio no story na huyo mwingne akikupigia simu ana shida Ni tabu tuputupu

Nimeamua kuish life langu full stop namshukuru mungu vibiashara vyangu vinaenda
 
Sio
Hii nayo inasikitisha yaani wewe uliyetoka kimaisha kushirikiana na ndugu zako unaona kama wanakurudisha nyuma??🤣

Aliyekuwa bado na maisha magumu matuamaini yake yako kwa ndugu zake wenye nafuu ya maisha. Hata ungekuwa wewe imungekuwa katika nafasi hiyo.
Sio naona. Nimejaribu kuwa karibu nao lakini walichofanya ni kuniibia mamilioni wengine malaki, wengine utapeli. Wengine hata siku moja hawajali kuhusu mambo yako wanakutafuta kukuomba hela tu.

Nilikuwa nawasaidia ila ndio ikawa hivyo na mambo yangu yakawa yanazorota. Baadaye nikaamua kuachana nao na mambo ndio yamekuwa yanaenda vizuri mno kibiashara na kimaendeleo tokea nifanye uamuzi huo mgumu. Pia mafanikio yangu hakuna aliyenisaidia zaidi ya mama.

Walinitupa kabisa hata kipindi nashungulikia issue ya kwenda abroad. Wakaniona mimi takataka. Nilipotoboa ndio wakajileta. Niliwasamehe, ila ndio ikawa ni mambo ya ujambazi na utapeli, ikabidi niachane nao. Leo ndugu zangu ni wafanyakazi wangu sababu wanajitolea sana kuchapa kazi na kampuni inasonga mbele vizuri sana sababu ya juhudi zao
 
Natoka job jioni nakuta majirani wamejaa sebuleni wanaangalia TV
Na wanakaa Hadi saa 6 Usiku wakati mwingine..
Sasa hao majirani ni wasimbe au wasela nini! Maana mtu unafamilia ukakae kwa jirani mpaka saa6 mambo yake afanye saangapi duu maisha hayo hapana, itakuwa nawewe umezoea kwenda makwao mpaka usiku wa manane
 
Huu ndio ujinga hapo huoni kama ulioa mzigo
Yaani kijitu mmekutana at 20's ndio aje kunigombanisha na chalii yangu niliyedokoa nae mboga utotoni

Haitokaa ikatokea kamwe
Hujaelewa hivi kama hauna chakusaidia au hali imebadilika mkeo ndiyo analaumiwe? Au wewe na mama na Baba yako si waliweka umoja wao ndiyo nyie mkazaliwa na kupata ndugu kwanini umuone yeye ndiye sababu hata kama hakipo? Hivi kama awamu hii unaweza kumlaumu ndugu hasaidii wakati wewe mwenyewe ukicheza vibaya unalala njaa?
 
Extended ndugu zangu hawana shida hao siwahesabii maana ni jukumu langu.Hawa wa simenti na mchanga hawa ndo taabu
Haaa haaa akiomba hela hauna unaambiwa unaringa nashukuru Mungu sina ndugu wa hivyo tuna ambiana ukweli sina sina kweli
 
Back
Top Bottom