DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,319
Ndio brother 😂😂😂😂😂ukaamua ujivue gamba
Ndio brother 😂😂😂😂😂ukaamua ujivue gamba
Kiukweli ndugu wengine ni wavivu. Au wamefanya maamuzi mabaya ya maisha kama kuzembea shuleni au kuchezea fursa. Mfano aliamua kuzaa watoto 7 na hana uwezo au Alipata hela ya maana akaichezea kwa starehe. Mimi nimepambana na kufanya maamuzi ya ku-sacrifice hadi nikatoboa. Halafu wao wale dezo.Hii nayo inasikitisha yaani wewe uliyetoka kimaisha kushirikiana na ndugu zako unaona kama wanakurudisha nyuma??🤣
Aliyekuwa bado na maisha magumu matuamaini yake yako kwa ndugu zake wenye nafuu ya maisha. Hata ungekuwa wewe imungekuwa katika nafasi hiyo.
Hongera aseeHaaa haaa akiomba hela hauna unaambiwa unaringa nashukuru Mungu sina ndugu wa hivyo tuna ambiana ukweli sina sina kweli
Hao wazungu unaosema sijui ni wazungu wa wapi. Wacha kujificha kwa wazungu kwa kuwa wanandugu zako wana roho za kutu. Nina marafiki zangu wamekuja kuwekeza miradi ya hotel. Jamaa alipofika mahali fedha ikamuishia alinambia ana kaka yake mtoto wa baba yake mdogo atamuazima kama dolar elfu 30 hivi amalizie mradi wake. Binafsi nimeweza kukaa na watu hawa wanapendana mno.
Tazama wahindi walivyo na upendo wao kwa wao. Yaani unaenda kwa familia ya muhindi unakuta nyumba ya vyumba vitano kuna ishi humo mtu kama 50 hivi. Wote ni ndugu na mwenye kipato( mhindi mwenye duka lake kariakoo) ni mmoja tu. Na anawalea wote na kuwatunza.
Twende kwa Warabu sasa. Yaanu haw ani noma. Mmoja akikosa mtaji wanamchangia na yeye anafanya biashara. Yaani hukuti kuna boya kwenye familia. Hata kama hakusoma lakini utakuta ana japo banda la spare za pikipiki.
Huku kwa waafrika sasa. Duuh ndio kama hayo. Ambayo na weww unayaendeleza kwa kisingizio kilekile.
Na haiji wealth ya kuja kurithisha jamaa zako badae haiji hivi hivi lazima kuwe na coorperation. Inaanza taratibu lakini kwa mawazo haya tunayoona ya umimi bado hatutafika popote. Hata hao wanaopeana dola elfu 30 usizani waliziokota chini wamehangaikia pia.Huwezi ukafananisha maisha ya Mwafrika na za wazungu, waarabu, wahindi nk. bila kuongelea generational wealth (kizazi kurithi mali na pesa toka kwa mababu/mabibi) na Black Tax.
View attachment 1466161
Huyo mwenye uwezo wa kumpa mwenzake dola elfu 30,000 unafikiri ni mtu anaetegemea mshahara wa kazi ya kawaida?? Minimum wage ya huko marekani kwa mfano ni chini ya dola $8 kwa saa na bado hajakatwa taxes. Hawa watu pia hawalipii shule mpaka labda chuo au kama wanatake mtoto aende private school. Huku kwetu ni kuanzia primary.
Huko marekani kwa mfano, watu weusi walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali/ardhi, kwahiyo tunaona matokeo yake sasa bado wanajitahidi kujinyanyua kutoka kwenye umaskini. Hapa Afrika kwa mfano kama Babu alikuwa mkulima ana wake wawili, kila mke akazaa watoto 8 kipindi hicho kilikuwa kitu cha kawaida; watoto wanazaliwa wengi , wanaenda kulima, maisha yanaendelea. Hakuna cha shule wala nini, kama ni shule mradi ujue kusoma na kuandika. Sasa maisha yakabadilika, na kwasababu first born kaenda shule, ndugu zake woooote 15 wanamuangalia wawasaidie, na hapo hapo kuna wazee wengine wanne wakutunza wakizeeka. Hii ndio tunaita Black Tax. Kipato chako kinarudi kusaidia wengine, mambo yako unashindwa kuyafanyia kazi sababu umeelemewa na majukumu .
Kwahiyo sidhani kwamba undugu ni overrated, bali tumegundua kuwa ukitaka kuishi maisha mazuri bila kuelemewa, inabidi kuwa selective, saidia ndugu zako . Jamaa watasaidiana na ndugu zao, kila mtu apambane na hali yake.
Hapo kwenye kuzaa sana bila mpango naungana na wewe kwa 100%. Imechangia umaskini na utegemezi usio wa lazima. Baba mwenye kipato cha mfano laki nne kwa mwezi na yuko kijijini au mkoani kwenye maisha nafuu. Anaweza kuweka akiba kila mwezi na kukuza mtaji au mali. Lakini kutokana unakuta ana wake wawili na watoto nane hiyo laki nne si kitu si lolote. Anatarajia watoto wakue ndio wasaidiane kulisha na kusomesha wenzao. Umaskini unarudi pale pale generatio after generation. Inakuwa vicious cycle.Huwezi ukafananisha maisha ya Mwafrika na za wazungu, waarabu, wahindi nk. bila kuongelea generational wealth (kizazi kurithi mali na pesa toka kwa mababu/mabibi) na Black Tax.
View attachment 1466161
Huyo mwenye uwezo wa kumpa mwenzake dola elfu 30,000 unafikiri ni mtu anaetegemea mshahara wa kazi ya kawaida?? Minimum wage ya huko marekani kwa mfano ni chini ya dola $8 kwa saa na bado hajakatwa taxes. Hawa watu pia hawalipii shule mpaka labda chuo au kama wanatake mtoto aende private school. Huku kwetu ni kuanzia primary.
Huko marekani kwa mfano, watu weusi walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali/ardhi, kwahiyo tunaona matokeo yake sasa bado wanajitahidi kujinyanyua kutoka kwenye umaskini. Hapa Afrika kwa mfano kama Babu alikuwa mkulima ana wake wawili, kila mke akazaa watoto 8 kipindi hicho kilikuwa kitu cha kawaida; watoto wanazaliwa wengi , wanaenda kulima, maisha yanaendelea. Hakuna cha shule wala nini, kama ni shule mradi ujue kusoma na kuandika. Sasa maisha yakabadilika, na kwasababu first born kaenda shule, ndugu zake woooote 15 wanamuangalia wawasaidie, na hapo hapo kuna wazee wengine wanne wakutunza wakizeeka. Hii ndio tunaita Black Tax. Kipato chako kinarudi kusaidia wengine, mambo yako unashindwa kuyafanyia kazi sababu umeelemewa na majukumu .
Kwahiyo sidhani kwamba undugu ni overrated, bali tumegundua kuwa ukitaka kuishi maisha mazuri bila kuelemewa, inabidi kuwa selective, saidia ndugu zako . Jamaa watasaidiana na ndugu zao, kila mtu apambane na hali yake.
PointNdugu mliokulia nyumba 1 au eneo moja, mara nyingi mna vitu vya kushea, memories.
Nakumbuka zamani wengi walikuwa wanatokea kijiji kimoja, watu wameoleana, bond ilikuwa strong!
Siku hizi mfumo wa maisha watu wamezaliwa maeneo tofauti, wamesoma maeneo tofauti, wakaajiriwa maeneo tofauti, wakaoa maeneo tofauti..huo ukaribu wa undugu utaupataje??
Lazima popote ulipo hata ugenini uwe na jirani, rafiki na watu wa karibu..uko U.S. mfano au Nanjilinjili, kwenu asili Bukoba, ukipata tatizo hadi mtu wa Bukoba akusaidie ni ngumu.
Ndugu tutazidi kutakutana kwenye misiba na harusi..
Undugu siyo kufanana bali kufaana!
Everyday is Saturday..........................
May be mpo wachache ndo maana mnathaminiana sana ktk nyakati hizi,kwangu mimi yote aliyoorodhesha mtoa mada yanaakisi maisha yangu na ndugu zangu.Mimi mbona ndugu yangu ndo aliyeninyanyua pale nilipojua mimi ni mgeni sana hapa duniani. Au kisa tupo wachache tu (3)!
Hao ndugu zenu inabidi mkapime DNA, labda bi'mkubwa alimpiga changa la macho mzee. Ndugu yako ni yule mliyetoka naye tumbo moja tu.
Sure,unapofeli ktk mambo yako utachekwa na kusemwa vibaya kinyama utadhani hata msaada walikupatia na kama walikupa msaada ukajisahau kuto fadhira basi utasimangwa mpaka ukajuta kwanini walikusaidia.Walichobakiza ndugu wa sasa ni kunafikiana na kuchekana, inasikitisha sana.
ia mifumo ya kijamaaTambua:
Siku hizi sio kama zamani ambapo undugu ulikuwa na thamani, damu ilikuwa nzito kuliko maji.
Siku hizi unaweza ukawa na braza hapa mjini msionane miaka miwili na msipigiane simu.
Siku hizi kila mtu ana time zake tu wanaita 'kuendana na kasi ya mheshimiwa'
Siku hizi rafiki na mchepuko wana nafasi kubwa kuliko ndugu.
Zamani matatizo ya ndugu yako ni matatizo yako lakini sikuizi kila mtu 'anapambana na hali yake'Undugu uliobaki ni mke, mume na watoto.
Lakini Kaka, Dada, Mjomba, Shangazi, Binamu imeshapitwa na wakati.
Maisha sasa hivi kila mtu yuko bize na maisha yake kutafuta vya kwake tu.
In short teknolojia ilileta ustaarabu na ndiyo inayouondoa.
Nyie ndio ndugu sasa.Hivi mki'share baba sio ndugu eti?
Hii imenitoa chozi...hali yake uko alikoolewa vip?Sahihi kabisa mimi binafsi bado najuta hadi leo kwa kuwa ilipita fursa sikuweza kumsaidi mdogo wangu wa kike. Alimaliza form four wakati huo mimi niko chuo na nilikuwa nasomesha wagmdogi zangu wengine wengi hivi kama watano hivi. Wakati huo kipato changu kilikuwa kidogo. Nilimweleza kuwa anisubirie kama mwaka hivi ili hali yangu ikiwa nzuri nitampeleka shule. Dogo wangu wa kike akanisikiliza akaendea kumsaidia mama kulima huko kijijini.
At the end miaka miwili ikapita mambo yangu bado tight na huku nina mzigo mwingine wa madogo. Mwisho wa siku mdogo wangu yule akapata mchumba. Akaniambia kaka nimesubiri sana msaada wako lakini naona bado naomba uniruhusu nieolewe. Basi nikamruhusu kwa uchungu sana. Hadi leo ana watoto watatu . Furaha yangu ilikuwa nimsomeshe apate maisha mazuri kwenye maisha yake.
Watu wanaona Ulaya ndugu wana maisha mazuri wanadhani yalijitengeneza. Hapana wanainuana. Undugu ni kusaidiana.kutokana na Choyo ya waafrika sasa wanasingizia Ulaya ya wazungu eti hakuna undugu ili wawatenge ndugu zao.
Wazungu wanapendana mno.