Siku hizi hakuna maisha ya mapenzi! Ni maisha ya maslahi!

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,167
11,491
Yale mambo ya kuonyesha unampenda kwa dhati kiasi gani mpenzi wako, au mke wako, au bosi wako au rafiki yako hayapo tena!

Kila mtu anaangalia maslahi ya kutoka kimaisha au kupata unafuu fulani wa changamoto za maisha au kwa jinsi gani uwepo wako utampa unafuu wa changamoto za kila siku!

Ukijizima data ukaweka matumaini na mategemeo makubwa kwa huyo mtu wako wa karibu utaishia kwenye maumivu!.

Jipe kipaumbele wewe mwenyewe na wale wanaokutegemea ambao bila wewe hawana maisha kama watoto (tegemezi chini ya miaka 18) na wazazi (kama kuna ulazima).

Mapenzi hayapo tena! Ukimtongoza mwanamke, huyo mwanamke anachokiona kwako ni fursa/pesa na ndani ya dakika/lisaa utaanza kupigwa mizinga! Unaona!

Hata mwanaume anawinda hako katundu tu basi! Nimeona jamaa yangu kafukuzwa kazi kachanganyikiwa! Nikamuuliza hiyo kazi ulidhani umepewa na babaako?

Kalaghabao! Juzi jirani yangu baada ya maokoto kupiga chenga, karudi nyumbani kakuta mke na watoto hawapo kakimbiwa na familia yake karudi kwao kadai utawaua kwa njaa! Jamaa kamkopesha rafiki yake pesa kashindwa kurudisha sasa maadui wa kutupwa! Hii dunia sio!
 
Tunawaambiaga msitafute pesa bali pateni pesa maana hakunaga mkate mgumu mbele ya chai, kiko wapi sasa? Me tumekuwa vilalamishi kila siku kwa Ke.
Jamaa anajilia mema ya nchi tu kwa Ke zote 3 alizooa kwa pamoja
Screenshot_2023-07-12-18-17-17-85_73617a28b0d3e7e6a04848a88f233e6b.jpg
 
Back
Top Bottom