Kumkopesha ndugu ni kuua undugu wenu

Bravo247

Senior Member
Sep 14, 2013
108
229
Nimejifunza ni bora lawama kuliko fedheha.

Ndugu yangu alikuwa na mahusiano mazuri sana na mimi tuliweza kuwasiliana na kutembeleana mara kwa mara, lakini mambo yalibadilika baada ya yeye kupata matatizo fulani na kuomba nimuazime kiasi fulani cha pesa (kikubwa tu), nikamsihi nami niko vibaya basi ajitahidi arejeshe kwa wakati kama alivyoahidi.

Cha ajabu muda ulivyokuwa unakaribia nilimkumbusha na akakejeli hiyo pesa ataitafuta ndani ya siku tatu karibu na deadline. Nilikaa kimya nikiwaza kama aliona ni kiasi ni cha kutafuta kwa siku tatu kwanini alikuja kuazima?

Siku ikawadia nkamkumbusha naomba ile fund maajabu jamaa akasema jioni, mara nimpe siku kadhaa. Ikawa week na sasa miezi. Nashindwa kuwasiliana naye maana meseji hajibu simu hapokei.

Nilichojifunza ni heri kutokumkopesha ndugu upate lawama kuliko kumkopesha na kuua undugu.
 
NDUGU hakopeshwi, anapewa, anasaidiwa ila mipaka iwepo, sio wote wanakopeshwa, wanapewa, wanasaidiwa. Wengine wanaachwa wapambane na hali zao.

Mkopeshe kiasi ambacho uko radhi kukipoteza.
 
Nimejifunza ni bora lawama kuliko fedheha.
Ndugu yangu alikuwa na mahusiano mazuri sana na mimi tuliweza kuwasiliana na kutembeleana mara kwa mara.
Lakini mambo yalibadilika baada ya yeye kupata matatizo fulani na kuomba nimuazime kiasi fulani cha pesa (kikubwa tu) nikamsihi nami niko vibaya basi ajitahidi arejeshe kwa wakati kama alivyoahidi.
Cha ajabu muda ulivyokuwa unakaribia nilimkumbusha na akakejeli hiyo pesa ataitafuta ndani ya siku tatu karibu na deadline. Nilikaa kimya nikiwaza kama aliona ni kiasi ni cha kutafuta kwa siku tatu kwanini alikuja kuazima??

Siku ikawadia nkamkumbusha naomba ile fund maajabu jamaa akasema jioni, mara nimpe siku kadhaa. Ikawa week na sasa miezi. Nashindwa kuwasiliana naye maana meseji hajibu simu hapokei.

Nilichojifunza ni heri kuto kumkopesha ndugu upate lawama kuliko kumkopesha na kuua undugu.
Ndugu uwa akopeshwi bali huwa anapewa mtu anashida pengine anadaiwa au anauguliwa wewe hela unayo kwanini usimpe kiasi kadiri ya uwezo wako?anatumia neno kukopa sababu anajua akikuomba umpi tuache ubakhiri
 
Unapomuazima pesa mtu kindugu/kirafiki toa kile tu ambacho upo tayari kukipoteza. Usitoe kiasi ambacho huwezi kusamehe na kupotezea.
 
Sikubaliani na wewe kama unataka kukopa KOPA kama unataka kuomba OMBA!!!
 
Unapomuazima pesa mtu kindugu/kirafiki toa kile tu ambacho upo tayari kukipoteza. Usitoe kiasi ambacho huwezi kusamehe na kupotezea.
Bora nisimpe tu kabisa!! Huo ni utapeli na kukoseana heshima!!! Sasa anafanya hata wengine wakipata tatizo wasiweze kusaidiwa!!!
 
Back
Top Bottom