Siku Freeman Mbowe alipotumia ofisi za CCM kuwakwepa polisi

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,013
Nitakuwa naleta mfululizo wa story za madhila ambazo viongozi wa upinzani walikuwa wanapitia enzi za Awamu ya 5. Story hizi zinasimuliwa na aliyekuwa Meya wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, Boniface Jacob.

Je, wajua katika maandamano ya CHADEMA kutoka Mwananyamala kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaaa ya Kinondoni ni CCM Wilaya ya Kinondoni ndiyo waliwaokoa Mbowe, Mashinji na Viongozi wengine wa CHADEMA dhidi ya risasi na mabomu ya polisi?

Ni 16 February 2018, siku ya kufunga kampeni katika marudio ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni, kufuatia aliyekuwa Mbunge wa CUF Maulid Mtulia kujiudhuru nafasi yake na kuhamia CCM.

CCM walikuwa wanafunga kampeni zao katika viwanja vya Biafra na CHADEMA walikuwa Mwananyamala.

Baada ya mikutano ya kufunga kampeni siku hiyo ya tarehe 16 February 2018 kila chama walikuwa wanatoka kwa maandamano.

CCM walikuwa wanatoka viwanja vya Biafra kuja maeneo ya Mwananyamala

CHADEMA walikuwa wanatoka viwanja vya Mwinjuma Mwananyamala kwenda Magomeni ofisi za Manispaa.

Katika hali ya kushangaza, misafara ya vyama vyote viwili ilikutana barabara ya Mwananyamala maeneo ya vijana.

CCM wakiwa kushoto wanaenda mwananyamala na chadema wakiwa upande wa kulia wanaitafuta barabara ya kawawa washike njia ya kwenda magomeni.

Bila ugomvi wowote maandamano ya CHADEMA yalifanikiwa kufika katika stendi ya mwendo kasi Mkwajuni yalifanikiwa na amani kabisa.

Baadae gari za polisi zilikuwa na kuyapita maandamano ya CHADEMA kisha kuyazuia kwa mbele, kwa kupiga mabomu na risasi kuelekea upande wa waandamanaji.

Polisi waliendelea kupiga mabomu na risasi mfululizo kwa waandamanaji wa CHADEMA katika eneo la Mkwajuni.

Vijana na walinzi wa CHADEMA wali chukua jukumu la kutuokoa kwa kutuingiza katika geti la ofisi za CCM Wilaya Kinondoni baadhi ya Viongozi wa CHADEMa tukiwa na Mwenyekiti Mbowe.

Baada ya kuingia mle ndani ya geti,tulikuta wana CCM wakiwa wametoka kwenye kampeni Biafra ingawa hawakuwa wengi.

Walionyesha upendo kwanza walifunga geti ili polisi wasiweze kuingia ndani.

Pili wakatufungulia geti ya nyuma tukatokea mtaani, tukatembea kuelekea CHADEMA HQ.

Ndugu yangu Heche John alichelewa kuingia kwenye geti 😂 akapata akili ya kuingia katika maduka ya nguo nje ya fensi ya ofisi za CCM Wilaya ya Kinondoni.

Kwa bahati nzuri muuzaji akafunga duka ili kumficha kwa ndani asiweze kudhuriwa na polisi waliokuwa wanapiga mabomu na risasi.

Hata hivyo baadae tulisikitika kusikia kuwa wana CHADEMA zaidi ya 10 walikuwa wamejuruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za miili yao, na mwanafunzi mmoja aliye julikana kwa jina la Akwilina Akwilini mwanafunzi wa Chuo cha NIT ameuwawa kwa risasi katika eneo lile la Mkwajuni😭😭
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom