Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,162
- 18,841
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.
Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.
Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.
Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"
Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"
Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.
Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.
Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"
Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!
Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.
Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"
Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.
Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!