Siku ambayo askari MP alipojitayarisha kumpiga risasi askari Sajenti kwa amri ya Mkuu wa Kambi ya Mgambo JKT

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni (nimekumbushwa kwamba alikuwa Luteni mmoja bongebonge sio Sajenti na mtu aliekuwapo Mgambo) huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamanda, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya Luteni kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi Luteni angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri Luteni apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Mkuu nje ya mada, kwahiyo alichofanya sabaya ni sawa baada ya kupokea amri kutoka juu?
Swali zuri sana. Unajua Mkuu, tukiwa jeshini, tulikuwa tukiambiwa askari anapaswa kutii amri wakati wote, ili mradi iwe wazi ni amri halali.

Kwa hiyo Sabaya alijua wazi alikuwa anapewa amri isiyo halali, hivyo hakupaswa kutii. Lakini hata hivyo, inawezekana kabisa amri halali ya Magufuli ilikuwa ni Sabaya kwenda kuwakamata wale watu. Lakini unadhani aliambiwa utakapoenda kuwakamata uwapige na kuwaumiza? Hata hivyo bado kuna maswali kama, kwa nini Magufuli akamtumia Sabaya na sio vyombo halali vya usalama kama TISS na Polisi? Ni wazi basi Magufuli na Sabaya walijua wazi walikuwa wanafanya uhalifu.

Sasa Sabaya akijua alikuwa anatekeleza amri ya kihalifu, utetezi wake haupaswi kuwa alitumwa, kwa sababu anajua hupaswi kutii amri isiyo halali. Ukiwa mhasibu huwezi kujitetea niliiba fedha za kampuni kwa kuwa meneja wangu aliniambia niibe. Utetezezi wa Sabaya unapaswa kujikita kwamba alifanya vile kwa kuwa kwa alivyomjua Magufuli, asingetekeleza maisha yake yangekuwa hatarini.

Na labda Sabaya awe na ushahidi kwamba fulani aliamriwa kutekeleza jambo la kihalifu na Magufuli na alipokataa aliuwawa katika mazingira tatanishi. Na pia anaweza kuweka ushahidi ambao unamwonyesh kuwa Magufuli alikuwa anaua watu waliompinga. Hapo ndipo anaweza kujiokoa na hii kesi.
 
kissa anyigulile

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
1,214
2,000
Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.

Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.

Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)

Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of course pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked, maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!

Operation nidhamu!!
 
St Lunatics

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
6,669
2,000
Swali zuri sana. Unajua Mkuu, tukiwa jeshini, tulikuwa tukiambiwa askari anapaswa kutii amri wakati wote, ili mradi iwe wazi ni amri halali.

Kwa hiyo Sabaya alijua wazi alikuwa anapewa amri isiyo halali, hivyo hakupaswa kutii. Lakini hata hivyo, inawezekana kabisa amri halali ya Magufuli ilikuwa ni Sabaya kwenda kuwakamata wale watu. Lakini unadhani aliambiwa utakapoenda kuwakamata uwapige na kuwaumiza? Hata hivyo bado kuna maswali kama, kwa nini Magufuli akamtumia Sabaya na sio vyombo halali vya usalama kama TISS na Polisi? Ni wazi basi Magufuli na Sabaya walijua wazi walikuwa wanafanya uhalifu.

Sasa Sabaya akijua alikuwa anatekeleza amri ya kihalifu, utetezi wake haupaswi kuwa alitumwa, kwa sababu anajua hupaswi kutii amri isiyo halali. Ukiwa mhasibu huwezi kujitetea niliiba fedha za kampuni kwa kuwa meneja wangu aliniambia niibe. Uteteze wa Sabaya unapaswa kujikita kwamba alifanya vile kwa kuwa kwa alivyomjua Magufuli, asingetekeleza maisha yake yangekuwa hatarini.

Na labda Sabaya awe na ushahidi kwamba fulani aliamriwa kutekeleza jambo la kihalifu na Magufuli na alipokataa aliuwawa katika mazingira tatanishi. Na pia anaweza kuweka ushahidi ambao unamwonyesh kuwa Magufuli alikuwa anaua watu waliompinga. Hapo ndipo anaweza kujiokoa na hii kesi.

Ikiwa Ndungai alipewa maelekezo kuwafukuza wapinzani bungeni nae Magu awashuhulikie uraiani tumeona kilichomfika Lissu. Sabaya angekaidi amri kibarua kingeota mbawa

lunatic
 
Mnyatiaji

JF-Expert Member
Dec 13, 2018
3,203
2,000
Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.
Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.
Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)
Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of cause pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked,maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!
Operation nidhamu!!
HATimae mmekutana na mtoa mada
 
kalonji

JF-Expert Member
Feb 17, 2021
6,317
2,000
Swali zuri sana. Unajua Mkuu, tukiwa jeshini, tulikuwa tukiambiwa askari anapaswa kutii amri wakati wote, ili mradi iwe wazi ni amri halali.

Kwa hiyo Sabaya alijua wazi alikuwa anapewa amri isiyo halali, hivyo hakupaswa kutii. Lakini hata hivyo, inawezekana kabisa amri halali ya Magufuli ilikuwa ni Sabaya kwenda kuwakamata wale watu. Lakini unadhani aliambiwa utakapoenda kuwakamata uwapige na kuwaumiza? Hata hivyo bado kuna maswali kama, kwa nini Magufuli akamtumia Sabaya na sio vyombo halali vya usalama kama TISS na Polisi? Ni wazi basi Magufuli na Sabaya walijua wazi walikuwa wanafanya uhalifu.

Sasa Sabaya akijua alikuwa anatekeleza amri ya kihalifu, utetezi wake haupaswi kuwa alitumwa, kwa sababu anajua hupaswi kutii amri isiyo halali. Ukiwa mhasibu huwezi kujitetea niliiba fedha za kampuni kwa kuwa meneja wangu aliniambia niibe. Uteteze wa Sabaya unapaswa kujikita kwamba alifanya vile kwa kuwa kwa alivyomjua Magufuli, asingetekeleza maisha yake yangekuwa hatarini.

Na labda Sabaya awe na ushahidi kwamba fulani aliamriwa kutekeleza jambo la kihalifu na Magufuli na alipokataa aliuwawa katika mazingira tatanishi. Na pia anaweza kuweka ushahidi ambao unamwonyesh kuwa Magufuli alikuwa anaua watu waliompinga. Hapo ndipo anaweza kujiokoa na hii kesi.
Askari upokea maagizo yeyeto ya mwanasiasa haruhusiwi kuhoji.
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
10,055
2,000
Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.
Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.
Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)
Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of cause pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked,maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!
Operation nidhamu!!
Aaah, kumbe na wewe! Haya, ngoja nirekebishe. Lakini ile bunduki ilikuwa SMG, ilikuwa SAR kweli?
 
Genecandy

JF-Expert Member
Dec 13, 2017
465
1,000
Ni jambo ambalo sintalisahau maishani mwangu, japo lilitokea zaidi ya miaka 20 iliyopita. Leo nimeamua kulisimulia kwa kuwa nadhani kwa sasa limefikia hatua ya kuwa "declassified" hata kama lilikuwa ni siri, ila sintataja majina ya wahusika.

Ilikiua usiku mmoja katika kambi ya JKT Mgambo, katika sehemu moja ya starehe watu walikuwa wakinywa na kuburudika kwa vinywaji mbalimbali pamoja na bia, wakihudumiwa na wasichana warembo service girls. Katika sehemu hii, alikuwapo pia Mkuu wa Kambi, ama CO kama tulivyowaita mara nyingi.

Sasa tunajua kwamba pombe sio chai, na baada ya bia mbili au tatu watu hubadilika katika kufikiri kwao na hata kutenda. Katika harakati za kuhudumia watu, service girl moja alipokuwa akipita katikati ya meza za wateja wake, aliangusha chupa ya bia ya askari Luteni ikapasuka na bia kumwagika. Luteni huyu alikuja juu kama vile amepoteza maji yake ya uzima! Alianza kumfokea yule service girl kwa uzembe kwa sauti ya juu.

Sasa Mkuu wa Kikosi alipoona hivyo alitoa amri kwa Luteni, "kamanda acha kelele! Service girl, mpe bia nyingine kamanda kufidia iliyovunjika"

Basi yule service girl alienda kumletea Luteni bia nyingine. Sasa jambo la ajabu ni kwamba yule Luteni alipoletewa bia kufidia iliyovunjia, bado akaendelea kumbwatukia yule service girl. Kitendo hiki kikamuudhi sana Mkuu wa Kikosi, akasema kwa hasira, "Kamanda, umerudishiwa bia yako na bado unapiga kelele, haya inuka nenda mahabusu sasa hivi"

Kwa ujasiri wa ajabu yule Luteni hakuinuka. Mkuu wa Kikosi akarudia tena, "Kamanda nakuamuru jipeleke mwenyewe mahabusu". Yule Luteni aliendelea kukaa pale kwenye kiti huku akigumia kwamba huo ulikuwa uonevu, kwa sababu bia yake ilivunjwa kwa uzembe.

Sasa Mkuu wa kikosi alikuwa na dereva wake MP nje ambaye alikuwa na SMG. Aliitwa ndani na Mkuu wa Kikosi akaambiwa "askari, koki silaha, mlenge sajenti". SMG ilitoa mlio wa vyuma kugongana wakati ikikokiwa, sauti ambayo wale wanaozijua bunduki watakuwa wanaifahamu vizuri. Ni mlio wa pekee sana.

Kisha Mkuu wa Kikosi akasema, "Kamada, nakuamuru kwa mara ya mwisho inuka jipeleke mwenyewe mahabusu"

Watu wote pale ukumbini wakawa kimya, ungeweza hata kusikia kishindo cha sisimizi wakitembea!

Yule Luteni aligeuka akaona SMG imeelekezwa kwake, na akajiinua taratibu na kuanza kuondoka kwenda mahabusu huku akisema kwa chini chini hii sio sawa.

Baada ya sajenti kuondoka, kulikuwa bado na kimya cha kama sekunde 30 hivi, na Mkuu wa Kikosi akasema "tuendelee kuburudika na kufurahi"

Lilikuwa na gumzo lililotawala kikosini kwa muda mrefu, watu wakijiuliza hivi sajenti angekataa kuinuka Mkuu wa Kikosi angemwambia dereva mpige risasi? Dereva angetii? Mimi niliamini kwa dhati kwamba Mkuu wa Kikosi angetoa amri sajenti apigwe risasi na dereva angetii, kwa sababu tu ya Mkuu wa Kikosi kulinda heshima yake.

Lakini jambo moja lilikuwa wazi kwangu, kwamba wote Luteni na Mkuu wa kikosi walifikia hatua ile kutokana na kwamba walikuwa wamekunywa bia. Na kwa mara nyingine niliona wazi kwamba kweli pombe sio chai!
Napenda hizi mambo
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,394
2,000
Sajenti miyeyusho.. Pombe haiwezi anafosi, hawa ndio wakija bar za uraiani wanasumbua watu kibwege bwege.
Sajenti mpuuzi sana ameleta mambo ya kitoto mno.

Ndio yale ya pipi imeanguka bahati mbaya halafu mtoto anafosi nataka kama ile akipewa pipi mpya hataki anataka ile ile iloanguka chini chafu!

Utoto kama huu ningemfumua ubongo huyo sajenti.
 
Peril22

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
553
1,000
Story ninaipata vizuri sana. Ila aliyeleta story ameikosea sana.
Kwanza Sargent hawezi kukaa sehemu moja ya vinywaji na Mkuu wa Kikosi, therefore ile ilikuwa officer's mess.
Unayemtaja kukokiwa bunduki alikuwa na Cheo cha Lieutenant. Msukuma mmoja bongebonge.
Yule CO alikuwa bonge la Kamanda. Alipenda sana seriousness katika kila kazi hasa training mnapokuwa "uwanja wa damu". (R.I.P)
Lakini kwenye burudani alipenda sana jokes (of cause pale baada ya kuona jamaa amelewa na hataki kutii amri, alimnong'oneza mtu fulani na kikafanyika kilichofanyika. Ilitumika SRA na si SMG (haikuwa na risasi), maana SRA inalia sana ikikokiwa, na good enough it worked,maana jamaa alisimama juu bila shuruti " paaap".) Ilikuwa burudani tosha!!
Operation nidhamu!!
Mleta mada ni miongoni mwa mananga wanaozalishwa jeshini kwa kupiga zile kozi za mtoto wa binamu anafundishwa na mtoto wa nmmjomba. Kuna cheo kinaitwa askari luteni kweli katika jeshi lolote!!, huyu askari luteni bia yake inamwagwa na kuambiwa aende mahabusu baada ya kugoma bunduki anaelekezewa sajenti.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom