Sikiliza Mabishano yaliyoibuka kati ya Msemaji wa Bavicha na Mwenyekiti Kamati ya Bunge wakati wa uwasilishaji

Hii ndiyo CHADEMA NA BAVICHA YETU ilivyo imara katika Haki, Uhuru na Maendeleo ya Watu kuwa katiba mpya ndiyo mama wa kila kitu ili watu na nchi kwa pamoja tupate maendeleo.

Tunataka sheria na katiba inayozingatia kuwa leo ipo CCM, kesho CHADEMA au UDP n.k hivyo mabadiliko hayo yaone miaka mingi mbele.

Hivyo si sawa Rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama fulani cha siasa kilicho chama tawala kuhodhi na kuteka nyara mjadala kwa ajili ya kutetea uwepo wa chama chake madarakani badala ya kuangalia haki kwa wote waliopo katika serikali kwa sasa wa chama tawala.
 
..huyu Dada wa Chadema kwanza yuko very confident and composed.

..kitu cha ajabu ni kwamba maoni aliyokuwa akiyatoa Mwakilishi wa Bavicha yanafanana na yaliyotolewa na watoa maoni wengine kama CCT, na TEC. Tatizo limekuja baada ya maoni hayo kutolewa na Bavicha na Mwenyekiti akaanza kubishana na muwasilishaji.


View: https://www.youtube.com/watch?v=9dj-7i7DXb8

Mwenyekiti ni nani? si amuache atoe mapendekezo yake? hana mamlaka ya kumvchagulia ni mapendekezo yapi ya kutoa
 
Tayari Kamati ya Kudumu ya bunge ya utawala, sheria na katiba llililo la chama kimoja kupitia uchaguzi ulioporwa 2020 limefeli kuwa sikivu kusikiliza maoni ya vyama na wadau.

Hivyo kamati hii kukosa uhalali wa kusimamia muswada wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi na sheria za Tume ya Uchaguzi.

TOKA MAKTABA :

TUNDU LISSU - SABABU YA MIKOA YENYE IDADI KUBWA YA WATU KUWA NA MAJIMBO MACHACHE YA UBUNGE

1704902093726.png

Picha maktaba: Mh. Tundu Lissu katika moja ya mikutano, akitoa elimu ya uraia na katiba
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishwi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya watu waliofikia umri wa kupiga kura.

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo ya ubunge umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia.

Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
 
..huyu Dada wa Chadema kwanza yuko very confident and composed.

..kitu cha ajabu ni kwamba maoni aliyokuwa akiyatoa Mwakilishi wa Bavicha yanafanana na yaliyotolewa na watoa maoni wengine kama CCT, na TEC. Tatizo limekuja baada ya maoni hayo kutolewa na Bavicha na Mwenyekiti akaanza kubishana na muwasilishaji.


View: https://www.youtube.com/watch?v=9dj-7i7DXb8

Nilikuwepo, kiukweli huyu binti yuko vizuri!
P
 
Back
Top Bottom