Sikia kisa cha Binti huyu, Jinsi kinavyosikitisha! Anahitaji Msaada wako na jamii kwa ujumla kukaa sawa. Je, tumsaidiaje?

Bushmamy

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
8,848
15,252
Maisha ni fumbo kubwa sana, hayo sio maneno yangu bali ni ya binti huyu mwenye umri wa miaka 35 kwa Sasa,.
Binti huyu Ambaye ni yatima muda wake mwingi Anapandisha na kushusha na barabara za Kijijini Kwao pasipokuwa na mwelekeo Wowote Huku akionge Mwenyewe.

Kisa kinaanza hivi. Baada ya kumaliza elimu yake ya msingi Alifaulu vizuri na kupaangiwa special school. Ikumbukwe kuwa ni enzi hizo kabla ya Ujio wa shule za Kata.

Lakini kutokana na hali duni ya familia walishindwa kumnunulia mahitaji muhimu ya shule kama vile daftari uniform na Ada ya kuanzia na hivyo kulazimika kukaa nyumbani.

Baada ya muda shemeji yake ambae ni Mume wa dada yake aliamua kumtoa pale kijijini na kumpeleka Dar es Salaam kwa ahadi Kuwa atamsomesha au angemtafutia kazi lakin baada ya. Kumchukua mambo hayakuwa kama alivoahidiwa bali alibaki nyumbani kuangalia watoto.
Mwisho wa Siku shemeji yake alimrubuni na. Kumbaka
kumpatia mimba pamoja na ugonjwa wa Ukimwi

Binti akiwa mjamzito wakati wa mahudhurio ya Kliniki Ndipo anapogundua kuwa ana maambukizi.

Baada ya majibu hayo akili ya yule binti haikukaa sawa hadi leo hii . shemeji yake aliyempa mimba baada ya kuugua kwa muda mrefu Alifariki dunia na Kumuacha mkewe na binti huyo katika Mateso makuu ya kulea watoto wenyewe huku wakiwa hawana kitu.

Baada ya hali ya binti kuwa na Mental health alinyanganywa mtoto kwa usalama zaidi na sasa binti anaishi yeye na kaka yake ambae nae hajaoa kwenye mji wa mama na Baba yake,.

Maisha yake anaishi Kana kwamba amekata tamaa ya kuishi
Je serikali na asasi za kijamii zina mchango /nafasi gani kwa watu wa aina hii.?

Itaendelea....
 
Kwa TZ Hatuwah kuw na malez kwa watu wenye mentor issues
 
Back
Top Bottom