Fr. Kitima na TEC mnalijua hili? Msaidieni huyu binti apate haki yake

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,948
"Mdogo wangu anaitwa Teresia Rubeni Mrimi. Ana cheti chake Cha kidato Cha nne kinachoshikiliwa katika Shule aliyosomea iitwayo Mother Theresa of Calcutta Secondary School nayomilikiwa na Kanisa Catholic Jimbo la Same.

Mwaka 2014 Fr. (Padre) Emmanuel Yatera alimtembelea Fr. Valentino Luvara Paroko wa parokia ya Vudee juu.

Katika ugeni huo Fr. Emmanuel Yatera kwa kushirikiana na Fr. Luvara walimuomba Mtoto Teresia Rubeni Mrimi kwa Wazazi wake aliyekuwa anasoma kidato Cha pili katika Shule ya Secondary Masheko (government) kuwa wanamtaftia mfadhili hivyo kumbeba na kumwingiza kwenye Shule yao ya Jimbo Mother Theresa Secondary School mwaka 2014.

Binti huyu alikuwa akifanya vizuri katika Shule hiyo ya kata kitu kichomvutia Paroko wa parokia ya Vudee Juu na Fr. Yatera ambaye alikuwa Mkuu wa Shule ya Mother Teresa kwa kipindi hicho.

Walimchukuwa Mtoto huyu anayetoka Familia ya kimaskini na kwenda kumwanzisha kidato Cha kwanza mwaka 2014-2018. Yaani walimrudisha nyuma. Baada ya kuhitimu, Shule hiyo sasa imeshikilia Cheti chake na kudai kuwa wanamdai Tsh. Milioni nne na laki mbili. (4,200,000).

Tangia mwaka 2018 hadi leo 2024 binti huyu anaranda randa mtaani akililia haki yake ambayo imepokwa na watumishi wa Mungu.

Familia ya Mzee Mrimi imetoa kila aina ya machozi kwa makasisi hawa lakini hakuna matumaini yoyote, wanajiuliza kuwa Wana nia gani na binti yao.

Walikuja wenyewe kumuomba kwa kigezo kuwa ni binti mzuri mwenye akili pevu yenye kung'amua mambo kwa urahisi pia angeweza kuwa mwanafunzi bora kwenye Shule yao, yaani kuitangaza Shule . Lakini mwishowe wameshikilia cheti Chake na kumtwisha mzigo wa deni mzazi huyu ambapo angesoma shule ya serikali aliyokuwa akisoma asingedaiwa pesa hiyo wala kushikiliwa cheti chake.

Familia ya Mzee Mrimi Tunaomba msaada wako bwana Yericko utufikishie kwa serikali ituokolee binti yetu apate cheti aendelee na masomo.

Namba ya Baba Mzazi wa Teresia Mrimi ni +255 783 841 577.

Namba ya Mkuu wa Shule ya Mother Theresa ni 0758 372 121.

Namba ya Meneja wa Shule Padre Fr. Mbaga +255 715 930 537

Number ya Simu ya Padre Emmanuel Yatera +255 767 066 701."CC...

@wizara_elimuTz

@ummymwalimu

@Dr_DGwajima
1705670964084.png
1705670978785.png
 
Amepata division ngapi? Kama alikuwa anafanya vizuri kwanini yupo mtaani? Ina maana hajafanya vyema form 4 yake.
Rudi kaongee na masister wamtolee copy au aliondoka na indiscipline cases?
Maana hii dunia ya wanawake inakuaje mtu mliye mfadhili Mumbai? Inafikilisha kidogo
 
View attachment 2876554View attachment 2876555
warangi bana kwa kulalamika 🐒

hiyo shule inasimamiwa na shirika, jimbo au TEC🐒

I think shida ni kwamba you are missing the target, jambo hili ni rahisi na jepesi mno, yapo mambo mmeficha....

kuweni wa kweli,
jueni hiarakia ya usimamizi wa hiyo shule, itasaidia na kumsaidia mtoto kuliko kuchonganisha na kutafuta huruma isiyostahili
 
Amepata division ngapi? Kama alikuwa anafanya vizuri kwanini yupo mtaani? Ina maana hajafanya vyema form 4 yake.
Rudi kaongee na masister wamtolee copy au aliondoka na indiscipline cases?
Maana hii dunia ya wanawake inakuaje mtu mliye mfadhili Mumbai? Inafikilisha kidogo
Wampe vyeti vyake
 
Apewe cheti chake

Nyie mtakitumia wapi

huyo bwege kakariri
cheti hawez pewa bila utaratibu labda sio kanisani katoliki my friend....

kwa utaratibu hawa jamaa huwez kuwayumbisha hata nukta....

Hawawezi kuhurumia mtu eti wakavunja utaratibu never ever.....

Hiyo familia wawe wakweli, wajuue shule inasimamiwa na nani shirika Fulani, Jimbo katoliki au TEC otherwise watapuuzwa tu 🐒

eti watakitumia wap 🤣🐒
 
Kwanza nikiri simfaham mwanafunzi huyu wala wazazi wake na hata hiyo shule siifahamu. Lakini pia nikiri kuwa habari yako haina ukweli kwa 💯,kwa sababu zifuatazo
1) haiwezekani km kweli alikuwa na akili unazosema akae mtaani, maan yake ni kuwa alishindwa mtihani. Km angekuwa amefaulu angechaguliwa na SERIKALI kujiunga kidato Cha TANO, na hapo ndo ukweli ungedhihiri maana hata mtendaji tu wa kijiji km angeambiwa juu ya kushikilwa cheti chake angefuatilia na suluhu ingepatikana maana huyu bado ni mali ya SERIKALI na lazima aendelee na shule.
2) km angekuwa amefaulu angetakiwa kupeleka result slip, kitu ambacho ingekuwa rahisi kupewa kuliko cheti halisi.
3) unasema hao ma Father walimuomba wamfadhili. Elewa ufadhili na msaada ni vitu 2 tofauti. Hapo lazima kuna makubaliano (mashariti) waliingia ndo maana wakaita ufadhili. Mfano, wanafunzi wa Tz wa vyuo vikuu wanafadhiliwa na SERIKALI kupitia HESELB. Manake ni kuwa kuna conditions and terms kati ya SERIKALI na mnufaika.
4) hao ma Father siyo vichaa kushikilia cheti Cha mwanafunzi waliemchukuwa kutoka mazingira ya kimaskini halafu waje wadai mamilioni ya fedha. Sidhani km ni wanyama kiasi hicho. Huu Ni uongo.
5) Unasema hao ma Father walimuomba na kumhamisha shule, walimjuaje maana familia masikini ni nyingi. Huu nao Ni uongo, hapa ukweli ni kuwa wazaz ndiyo waliwafuata ma Father shuleni kwao, na hapo ndo conditions and terms zilipoafikiwa baina yao.
6) tangu amalize, huyo mwanafunzi alichukuwa hatua gani ili kupata msaada wa kupata cheti chake maana kuna uongozi wa SERIKALI kuanzia kwenye shina hadi taifa, eti hadi wewe leo ndio unakuja kutoa habari yake. Hii inatia shaka.

NB:
wewe nenda shuleni hapo ulete taarifa sahihi. Usipende ya kuambiwa, vinginevyo za kuambiwa changanya na za kwako
 
Apewe vyeti vyake waache uduanzi wa kigalatia. No matter what vyeti ni haki yake na ni mali yake si ya Shule.
 
warangi bana kwa kulalamika

hiyo shule inasimamiwa na shirika, jimbo au TEC

I think shida ni kwamba you are missing the target, jambo hili ni rahisi na jepesi mno, yapo mambo mmeficha....

kuweni wa kweli,
jueni hiarakia ya usimamizi wa hiyo shule, itasaidia na kumsaidia mtoto kuliko kuchonganisha na kutafuta huruma isiyostahili
..utakuwa umevuta bangi weye! mrimi ni mrangi?
 
Back
Top Bottom