Haya ni matatizo ya jamii masikini. Zaidi ya jamii masikini, mentality ya kimasikini. Maana unaweza kukutana na mtu masikini lakini hana mentality ya kimasikini.
Kuna siku, miaka ya nyuma sana, nilikuwa namtongoza dada mmoja, dada Mmarekani mweusi. Mtoto mkali, katulia.Nikasema ngoja nimchokoze huyu kwenye mtoko wa weekend.
Nikamtupia ndoano ya maneno matamu, tukawa tunaelewana.
Nikamwambia vipi weekend, una mpango gani? Ningependa tutoke. Akasema kutoka ningependa, ila kwa sasa nimechalala, mambo yangu si mazuri.
Sasa mimi mwanamme wa Kiafrika nikasema hapa si ndo penyewe pa kutoka kidedea mwanamme. Nikamwambia wewe usijali, mimi nitakuja kukuchukua nyumbani, tutakwenda restaurant ya maana, tutabarizi vizuri, halafu nitakurudisha.
Bidada akashukuru sana kwa ukarimu wangu, lakini akaniambia kwamba, yeye hata kama mwanamme atamlipia kila kitu, hawezi kufanya mtoko bila ya yeye kuwa na hela zake pia.
Nikamuangalia yule bibie, nikasema dada ningeweza kukurekodi tutoe somo kwa dada zetu wengine wa kibongo ningefanya hivyo.
Huko kwetu unaweza kuombwa mpaka nauli, ukatuma nauli na ya kutolea, halafu mtu asije!