Sijawahi kufikia wala kuvuka uzito kg 60!

Sijawahi kufikia wala kuvuka uzito kg 60!

Mkongwe, hiki nacho kinanitafakarisha, nawaza hivi ikitokea nimepigwa homa iliyochangamka, ile mfululizo itakuwaje.
Ni hatari sana ,piga msosi mkuu mwili upate virutubisho ,piga msosi kisha uwe unafanya mazoezi ili mwili usikuzidi...Wembamba ni hatari kwa afya...ukipigwa na kihoma kidogo kinaweza kukupeleka ICU.
 
Ulicho nacho wewe (uzito mdogo) tupo tunaokitafuta kwa jasho na damu na tusikipate,shukuru upo hivyo uzito mkubwa siyo afya ni mateso.

Mimi miaka 13 nyuma nilikuwa nakomea 67 kirudi 65 but majuzi hapa nikajikuta nipo 86+ nimejiwekea ratiba ya mazoezi kwa week nimezikata shida uzito umesimama kwenye 74 nimepambana navyopambana hata 70 nimeshindwa kuigusa.
Mkongwe, wewe ulikuwa pazuri, hizo kilo 67 ni ulimwengu wa peponi katika mwili wangu.

Mimi hapa naitamani 60 tu kamili, yaani nipate tu hata 60 tu.

Urefu wangu ni futi 6 mzee, kilo 58 kwa urefu wangu sio sawa kabisa.
 
Familia, hii kitu kuna wakati inanikera. Kiasi kwamba siku hizi nikiona mzani mbele yangu nahisi kama nimeona adui.

Iko hivi, urefu wangu ni 182cm, uzito wangu sasa...58kg.

Aisee, maisha yangu yote sijawahi kuvuka hiyo kilo 58, sanasana kuna wakati nashuka mpaka kilo 56.

Natamani sana kuongezeka uzito, angalau na mimi niwe na hata kilo 60. Nini nifanye kuongeza uzito!?

NOTE: Sina ugonjwa sugu wowote, siumwi mara kwa mara, ni zaidi ya miaka mitatu sasa sijakanyaga hospitali.
Mkuu Achana na mikopo ya kausha damu
 
Back
Top Bottom