Sijavutiwa na muonekano wake ila anataka kunioa

Sijavutiwa na muonekano wake ila anataka kunioa

nime shuudia mabinti wengi wazuri kwa mtindo huo huo kuchagua muonekano na mwisho wake wamebaki kama vimada,kuzalishwa aka single mama,umri usha kwenda na hakuna hatakaye mtaka.
Kuna wakati akili zetu bongo zake hugeuka makamasi labda unatamani mtu umchape tunayaona kila siku mitaani lkn hatusikii kaka kakupenda unaleta nyodo aisee km haamini Mungu basi amtose huyo kaka ataona rangi zote za dunia Hii atalia mpk akauke
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?
Subiri mwenye muonekano anakuja
Unataka muonekano wakati we mwenyewe gaka tuu.
Nyie wadada vip nyie
 
Kumpenda mtu huwa anajifunza na kama mtu anakupenda hana shida nyingine yoyote what else do you want? Be thankful mshukuru Mungu hata kwa huyo aliyekuletea, sababu hiyo sura au muonekano unaouhitaj mwisho wa siku hauna mchango wowote ktk maisha yako ya ndoa.

Na mwisho jifunze kuridhika sababu hii ndio sifa kubwa anayotakiwa kuwa nayo mwanamke.
 
Utakuja kumsumbua bure jomba bira utavute aina zako. Mwanamke huanza kupenda ndio mengine yafuate
 
Love him for who he is and not for what he has...
 
Uwezekano mkubwa wa kumpenda upo sana ukiwa karibu na mtu lazima utamzoee na kumpenda kikubwa angalia vile moyo wako unapenda usije ukaenda kumsumbua mkaka wa watu bure

Doooooooh Nenda dada kapate stara yako ukipendwa shikamana ooooohoo.Atakupenda huyo na utasahau hata hao wazuri tena hao ndo wanaume sasa

Mungu hakupi vyote hivyo huyo kapewa mali na upendo kanyimwa vingine nendaaaa tu
Muumbaji ni mmoja

Mhh. Hili ndio tatizo letu baadhi ya wanawake. Ila kabla ya kufanya unayoyataka kuyafanya angalia kwanza umri unaruhusu kuwa na hayo maringo uliyo nayo sababu usije jikuta wakati unafika wa kutaka ndoa na hata wa kukupa habari gani asipatikane.

We angalia vile moyo wako unataka.

Pia wacha dharau sababu hakuna aliyejiumba.
Nadhani kila mmoja kapata like yake[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
 
Habari zenu wapendwa,

Nimekutana na mkaka ambaye tunafahamiana kitambo kidogo kiukweli amejaaliwa mali na ana upendo na mimi na yupo tayari kunioa tatizo sasa linakuja mimi ninachompendea anatabia nzuri ila kama mnavyojua Mungu ametuumba tofauti kila mtu na sura yake na kila mtu macho yake anavyoona hivyo kwenye swala la muonekano kiukweli hajanivutia kabisa yaani daah.

Ila tabia ni njema sana sasa nawaza nikimkubali anioe hivi inawezekana kweli kuja kumpenda huyu mtu baadae nikiwa kwenye ndoa maana wengine wananiambia nitampenda mbele kwa mbele uwezekano huu upo kweli?
Endelea kusubiri hadi umpate mwenye muonekano mzuri , hata kama hana tabia nzuri ama ni lofa wewe usijali ili mradi ana muonekano mzuri
 
Una natanata usikute ww mwenyewe libaya lakini hujioni maana mijitu mibaya ndo inaonaga wengine wabaya we muache endelea kusubiria wapiga chuma
 
Hill ndio tatizo la wanawake na wakiingia uhengani wanatamani kuolewa hata na mentally unfitted.
 
Back
Top Bottom