joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kitendo cha UK & USA kuamua kuiwekea vikwazo Zimbabwe'(Targeted sanctions), kumezua tafrani katika bara la Africa, hasa katika nchi za SADC.
Nimejaribu kufikiria sana ili niweze kujiridhisha kama kweli waafrika tunapaswa kulalamika na wengine hata kufikia hatua ya kuzitishia hizi nchi, lakini sijapata sababu yoyote ya msingi.
Hakuna sheria yoyote katika umoja wa kimataifa inayolazimisha nchi kufanya biashara au kuwa na mahusiano ya kidiplomasia na nchi yoyote, hayo ni maamuzi ya nchi wenyewe, UK na USA wameamua kukata mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na Zimbabwe, sasa sisi nchi zingine tunahusikaje katika hilo hata tuanze kutoa vitisho?.
Wakati wa ukombozi kusini mwa Africa, nchi nyingi za Ulaya ziliamua kukata uhusiano na Tanzania, na zingine kama vile Ujerumani Magharibi na Uingereza, Nyerere alizifukuza na kuwarudishia baadhi ya pesa zao ambazo walizitoa kama misaada, kutokana na kutoelewana, kwanini Nyerere hakulalamika na kuwaambia waondoe vikwazo vyao.
Kwangu mimi ninaona hatua hii ya kuwalalamikia ili waondoe vikwazo, ni dalili ya udhahifu mkubwa wa nchi za Afrika, hii ni dalili kwamba, bila hizi nchi, Africa haiwezi kufanya lolote lile, kubwa ninaloliona ni kwamba uchumi wa nchi za Afrika unategemea sana wazungu.
Badala ya kutoa vitisho ambavyo ninajua wala haviwezi kuwatikisa hawa wakubwa, bora tungegangamala kama alivyofanya Nyerere ili kupunguza hathari ya vikwazo kwa Zimbabwe, au tungekuwa wanyonge na kuwaomba kwa upole ili waviondoe.