Sijala toka jana nilipohakikisha sijachaguliwa uhamiaji

Makaura

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
892
293
Wana JF, jana mlitupa taarifa ya kuitwa kazini kwa wale 70, baada ya kuona hayo, nilikimbilia kwa muuza magezeti, nkanunua gazeti la uhuru, kuangalia jina langu halipo.

Sikukata tamaa nkanunua daily news pia jina halipo, nikaamua kulipia 200 kwa kila gazeti, kuangalia mengi hayana majina, nilichukua hatua ya kutembelea website yao, pia jina langu halikuonekana.

Hatimaye nikawauliza marafiki kama jina langu lipo, wakaniambia herufi ya kwanza ya jina lako haipo kabisa kwenye list. Ndugu zangu nimekata tamaa na sikula tokea jana mpaka leo, sina hata hamu ya chakula! Maombi yenu ndugu zangu!
 
Pole usikate tamaa mungu yupo

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Duh pole sana ila we nae ulikuwa na moyo yaani kati ya watu 10000 wanataka 70 we nar ukaenda.
Pole sana ndio maisha haya
 
Wana jf, jana mlitupa taarifa ya kuitwa kazini kwa wale 70, baada ya kuona hayo, nilikimbilia kwa muuza magezeti, nkanunua gazeti la uhuru, kuangalia jina langu halipo, sikukata tamaa nkanunua daily news pia jna halipo, nikaamua kulipia 200 kwa kila gazeti, kuangalia mengi hayana majina, nilichukua hatua ya kutembelea website yao, pia jina langu halikuonekana. Hatimaya nikawauliza marafiki kama jina lango lipo, wakaniambia herufi ya kwanza ya jina lako haipo kabisa kwenye list. Ndugu zangu nimekata tamaa na sikula tokea jana mpaka leo, sina hata hamu ya chakula! Maombi yenu ndugu zangu!

Kaka usikate tamaa Maisha yana milango mingi, sio lazima upitee mlango wa Uhamiaji. Me nashukuru niliapply nikijua nitakosa. Ukiwa una apply kazi zenye kuhitaji watu wachache na applicants wako wengi jiwekee kuwa utakosa alafu ukienda kwenye interview fanya kama kazi inakuja mikononi mwako.
 
Asanteni ndugu zangu, kiukweli nakumbuka oral nilifanya vizuri sana, hata wao wenyewe walinikubali sana, sijajua nini kimetokea hapa katikati!
 
Kwani ulijihakikishia vipi kama utapata hadi ufikie hali yakutokula chakula zaidi ya masaa 24?

Usikate tamaa mkuu. Kikubwa kama huna kazi endelea kufight, na kama unayo, endelea kufanya hapo hapo kazi mzee.
 
poor you! kwa nn ulie kwa kukosa kazi uhamiaji? mm ata sikupi pole
komaaa na sehemu nyingine,think outside the box maisha ni zaidi ya uhamiaji
 
Asanteni ndugu zangu, kiukweli nakumbuka oral nilifanya vizuri sana, hata wao wenyewe walinikubali sana, sijajua nini kimetokea hapa katikati!

Hii huwatokea wale ambao hawajiamini au wanaleta stories zisizohusika kwenye interview interviewer ataonyesha gestures za kukufanya uwe na confidence zaidi au kufetch ujinga wako zaidi sorry mkuu usikate tamaa
 
Huyu jamaa aliweka hela kwa watu wa uhamiaji, hela wakala wakimuahidi kazi, kakosa anaanza kulia. Baki njia kuu
 
Tangu awali nilisema humu ndani kwamba zile nafasi zina wenyewe watu hawakutaka kuamini,leo wamejionea wenyewe.Uhamiaji ni zaidi ya uijuavyo
 
watu walishapangwa kitambo interview ilikuwa mbwembwe tu. Tanzania unaijua wewe!
chakushangaza kunawatu ata ile interview ya uwanja wa taifa hawakufanya ila wameitwa. bora kuwa jambazi kuliko kusubiria ajira za bongo
 
Kama ulitizama uhuru jina lako litakuwepo sema tu uhuru wanachuki binafsi kwa vijana jaribu kufuatilia
 
Uhamiaji ni shida kwa kweli watu wanabebana sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom