Naomba kutoa changamoto kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini
Naamini wenye changamoto ya kucheleweshewa mikopo hawakuwa wanafunzi wa UDSM peke yao. Huenda vyuo vingi tu havijapewa mikopo yao ila UDSM kupitia uongozi wao walikuwa wa kwanza kuja hadharani na kudai haki yao
Matokeo ya kudai haki yao hiyo imewagharimu baadhi ya wanafunzi wa UDSM kwa kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana
Wito wangu kwa wanafunzi wote, huu ndo muda wa kuungana kwa pamoja ili kuwatetea wenzenu waliosimamishwa masomo
Naamini viongozi wale hawakujituma na wala hawakuwa wanadai madai yao peke yao
Ilikuwa wao watoke mbele wadai haki za wengi waliokuwa nyuma yao
Huu ndio wakati sasa wa hao waliokuwa wanawakilishwa na viongozi wao kutoka hadharani na kudai madai mawili!
Dai la kwanza liwe viongozi hao wa UDSM kurudishwa chuoni bila masharti kwa sababu kimsingi hawana kosa! Saa 72 ni sawa na siku tatu muda unaotosha kabisa kwa taasisi makini kutoa majibu ya walichokuwa wanadai! Wangeamka na kuanzisha maandamano bila mpango wowote nadhani kila mtu asingewaelewa!
Dai la pili liwe kwa Bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa wahusika wote kama mkataba unavyosema! Hivi hao watumishi wa bodi wakikaa miezi miwili bila posho wala mshahara watajiskia vizuri? Familia zao hazitateteleka? Vipi kwa mwanafunzi anayetoka familia isiyokuwa na kipato?
Ifahamike kuwa endapo wanafunzi mtaacha viongozi wenu wakose masomo kwa adhabu hiyo waliyopewa jamii ya watu makini haitawaelewa!
Nyie kama wasomi ndio kioo cha Taifa! Nyie ndio mwelekeo halisi wa wasomi tulionao kwa sasa hivyo hamna budi kuudhibitishia umma kiwango cha weledi wenu
Note: Mimi sio mwanafunzi wa chuo chochote ila nafahamu shida ya wanafunzi wanapokosa mkopo kwa muda
Pia maoni yangu hayo juu yatakuwa na msingi endapo viongozi waliwashirikisha wenzao na tamko lao lilitokana na kikao halali cha serikali ya wanafunzi
Sent using Jamii Forums mobile app