Sihamasishi vurugu, ila huu ndo wakati mzuri wa kufahamu ueledi wa wanafunzi wa vyuo vikuu

Kingjr2

JF-Expert Member
Sep 8, 2018
644
1,271
Naomba kutoa changamoto kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini

Naamini wenye changamoto ya kucheleweshewa mikopo hawakuwa wanafunzi wa UDSM peke yao. Huenda vyuo vingi tu havijapewa mikopo yao ila UDSM kupitia uongozi wao walikuwa wa kwanza kuja hadharani na kudai haki yao

Matokeo ya kudai haki yao hiyo imewagharimu baadhi ya wanafunzi wa UDSM kwa kusimamishwa masomo kwa muda usiojulikana

Wito wangu kwa wanafunzi wote, huu ndo muda wa kuungana kwa pamoja ili kuwatetea wenzenu waliosimamishwa masomo

Naamini viongozi wale hawakujituma na wala hawakuwa wanadai madai yao peke yao

Ilikuwa wao watoke mbele wadai haki za wengi waliokuwa nyuma yao

Huu ndio wakati sasa wa hao waliokuwa wanawakilishwa na viongozi wao kutoka hadharani na kudai madai mawili!

Dai la kwanza liwe viongozi hao wa UDSM kurudishwa chuoni bila masharti kwa sababu kimsingi hawana kosa! Saa 72 ni sawa na siku tatu muda unaotosha kabisa kwa taasisi makini kutoa majibu ya walichokuwa wanadai! Wangeamka na kuanzisha maandamano bila mpango wowote nadhani kila mtu asingewaelewa!

Dai la pili liwe kwa Bodi ya mikopo kutoa mikopo kwa wahusika wote kama mkataba unavyosema! Hivi hao watumishi wa bodi wakikaa miezi miwili bila posho wala mshahara watajiskia vizuri? Familia zao hazitateteleka? Vipi kwa mwanafunzi anayetoka familia isiyokuwa na kipato?

Ifahamike kuwa endapo wanafunzi mtaacha viongozi wenu wakose masomo kwa adhabu hiyo waliyopewa jamii ya watu makini haitawaelewa!

Nyie kama wasomi ndio kioo cha Taifa! Nyie ndio mwelekeo halisi wa wasomi tulionao kwa sasa hivyo hamna budi kuudhibitishia umma kiwango cha weledi wenu

Note: Mimi sio mwanafunzi wa chuo chochote ila nafahamu shida ya wanafunzi wanapokosa mkopo kwa muda

Pia maoni yangu hayo juu yatakuwa na msingi endapo viongozi waliwashirikisha wenzao na tamko lao lilitokana na kikao halali cha serikali ya wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha waendelee kuvuna matunda ya kura zao na za wazazi wao, tutawabembeleza mwakani mwezi wa kumi.
 
Sijawahi kuona mwanafunzi anayejifanya nunda chuoni akifanikiwa!
Tatizo sio kujifanya nunda na hakuna mtu timamu atasapoti manunda!

Mwanafunzi wa chuo anategemewa kujitambua, kufahamu haki zake, kufahamu njia za kudai haki zake pale zinapominywa na pia anatarajiwa kushauri na kusaidia jamii pale panapohitaji msaada

Kudai haki sio ununda! Kuongoza watu kudai haki zao sio ununda! Kuhamasisha watu kujitambua na kutambua haki zao sio ununda! Hizo ni baadhi ya faida zinazotarajiwa kwa mwanachuo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashtuka nikiskia watanzania wanaunga mkono wanafunzi wasiandmn kupt hak yao HUKU wakiacha kuikosoa serikali wanavyowatesa njaa watoto wa wenzenu"think about first year" inatia huruma
 
Mlimani City kupo shwari kabisa hakuna wavaa milegezo wakiwa na boxa chafu wala wadada watembea uchi. Leo ndiyo nimegundua kumbe ni wanafunzi udsm. Halafu kukopeshwa siyo lazima na mkiendelea na kelele kifutacho ni Fanya fujo uone. Ffu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingjr2,
Kwani hapo wanadai hali gani? Ili upate mkopo umeambiwa lazima ukidhi vigezo. Hujakidhi. Ukakata rufaa. Ukaahindwa. Unatetea haki gani hapo?

Maoni yangu; badala ya hao vijana kulilia mikopo kwa hoja dhaifu, waombe sheria ya utoaji mikopo ibadilishwe. Kwamba, badala ya kuwa na Bodies ya Mikopo, Admission Letter ya chuo anayopata mwanachuo ndio iwe sifa kuu ya kupata mkopo. Na mikopo itolewe na benki ambazo zitaingia mkataba na serikali ambayo ndio itakuwa mdhamini mkuu kwa kazi hiyo. Kwahiyo, mwanachuo anabeba barua yake anaenda ku bargain na afisa wa benki anataka kiasi gani kwa kila mwaka wake wa masomo. Halafu liwe jukumu la hizo benki kufuatilia marejesho. Hapo kutakuwa hakuna maandamano wala nini!
 
sweettablet, Umekimbilia kucoment bila kusoma. Wanafunzi wanaolalamika si waliokosa mikopo, bali walio kwenye orodha ya walio andikwa kuwa watapewa mikopo lakini bado hawajapewa hela. Kuna watu kazi ni kusifu serikali tu bila hata kujiuliza kulikoni. Vyuo vimefunguliwa tangu oct, hujiulizi kwa nini mpaka leo heslb hawajatekeleza wajibu wao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom