Mkuu wa mkoa awataka wanafunzi vyuo vikuu kuachana na ndoa za miaka mitatu

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego amewataka Wanafunzi wa Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu Mkoani Iringa kuacha tabia ya kuanzisha ndoa zinazodumu miaka mitatu ya masomo yao na pindi wanapomaliza masomo ndoa hizo huishia hapo jambo ambalo linapelekea Wanashuka hao kushuka kitaaluma.

Dendego ameyasema hayo akiwa Mgeni rasmi katika kongamano la la wasomi lililofanyika katika ukumbi wa kichangani Manispaa ya Iringa ambapo amesema ni vyema Wanafunzi hao wakasoma na wakaachana na hizo ndoa au mahusiano ya miaka mitatu na baadae kuja kupata magonjwa .

“Ni vizuri Vijana mkajitambua na Vijana ndio nguvu kazi ya Taifa ili liweze kusonga mbele na kuwa na maendeleo linahitaji Vijana wenye nguvu na Wazalendo kula nanasi kunahitaji nafasi , niwaase mmeletwa huku kusoma na sio kuanzisha ndoa zenu za miaka mitatu niwaombe msome kwa bidii ili muipate A na sio AIDS “


Sent from my 21061119AG using JamiiForums mobile app
 
Haiwezekani Kwa sababu wanawake wanazitumia kupata Msaada wa kimasomo na pesa Kwa Wanaume/Vijana wa kiume
 
Tatizo lingine hawa wanachuo wanajua kujiremba hasa mabinti Yani bint anajiremba mpaka boys na baadhi ya lecturers wanawakula kama chips kuku wapunguze kujiremba angalau wavae maguo ya ajabu wasivutie.
 
Nikae na Dem miaka mitatu amekuwa digrii?

Au nikae na Dem semista amekuwa kozi,?

Hit and run
 
Back
Top Bottom