Sihamasishi vurugu, ila huu ndo wakati mzuri wa kufahamu ueledi wa wanafunzi wa vyuo vikuu

Wanyime wanao (kama unao), mumeo au mkeo (kama unaye) chakula au haki yake kwa miezi miwili bila sababu za msingi halafu usubiri kujibiwa kwa adabu

Kinachofanyika ni ubabe tu! Na huu ubabe unaendekezwa na watu kama nyie.

Uoga ni dhambi na dhambi huleta mauti!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi sio mtaalamu wa vitisho vya mtandaoni. MnavyoandikaGA kwa kujiamini mtandaoni mngekuwa ndivyo mnavyofanya mtaani, basi nchi hii ingefika mbali. Ngoja nikuulize, mbona huyo "Rais" kafukuzwa kama mbwa koko. Hao wanachuo aliokuwa anawatetea wako wapi? Si ajabu na wewe ni mwanachuo hapo Mlimani na umeufyata hasira na misimamo unamalizia mtandaoni! Pumbavu!!!!
 
me natamani waandamane ili nione jinsi watakavo-chezea virungu.

jamani udsm andamaneni please please.
Utafaidika na nini wakionewa? Ukweli ni wamba serikali inapaswa itimize wajibu wake, ikiwa waliwachuja wakawapata hao ambao kwa mujibu wa masharti na vigezo vyao wanastahili kupewa mikopo kwa kumaanisha kuwa bajeti ya kuwawezesha wanafunzi hao ipo.
 
Utafaidika na nini wakionewa? Ukweli ni wamba serikali inapaswa itimize wajibu wake, ikiwa waliwachuja wakawapata hao ambao kwa mujibu wa masharti na vigezo vyao wanastahili kupewa mikopo kwa kumaanisha kuwa bajeti ya kuwawezesha wanafunzi hao ipo.
sijasapoti wao kutokupewa mikopo waliyoahidiwa, ila me nawakosoa kutaka kutumia maandamano kama njia ya kupata wanachokihitaji.
 
Mimi sio mtaalamu wa vitisho vya mtandaoni. MnavyoandikaGA kwa kujiamini mtandaoni mngekuwa ndivyo mnavyofanya mtaani, basi nchi hii ingefika mbali. Ngoja nikuulize, mbona huyo "Rais" kafukuzwa kama mbwa koko. Hao wanachuo aliokuwa anawatetea wako wapi? Si ajabu na wewe ni mwanachuo hapo Mlimani na umeufyata hasira na misimamo unamalizia mtandaoni! Pumbavu!!!!
Soma original post niliyoweka hapa!

Lengo la post yangu ilikuwa kuwauliza hao wanachuo na si UDSM tu bali wa vyuo vyote, baada ya viongozi waliofukuzwa kwa kutetea haki zao wao wanachukua hatua gani?

Kuhusu kuwa mwanachuo nadhani ni ukosefu wako tu wa umakini maana nilishaliweka hapo juu tangu mwanzo!

Mimi sio mwanachuo tena, nilishapita huko miaka mingi tu iliyopita! Nimeliweka hivi hili swala kwasababu nayafahamu maumivu ya kukosa au kucheleweshewa mikopo!

Huyo Ndalichako akae miezi miwili tu bila mshahara, posho au marupu rupu tuone kama atapata amani ya moyo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
*MAISHA YA CHUO BILA MKOPO HIVI NDALICHAKO UNAYAFAHAMU*

Kalamu ya Miambili ya Mwl.Jonathan Kwizera aliyekuwa katibu Mkuu DARUSO 2017/2018.

Nikiwa mtaani baada ya muda kadhaa kutoka UDSM, nimeshangaa sana Maamzi yaliyofanywa na Waziri wa Elimu tena Profesa juu ya viongozi wa UDSM waliokua wanadai haki zao za Mkopo kama wanafunzi wanyonge.
Nikajiuliza, hivi uamzi wa NDALICHAKO, Waziri tena Profesa ameufanya akiwa na Figo zote mbili, mapafu, kichwa na pumzi ya uhai aliyopewa na Mungu?

Maisha ya kucheleweshewa Mkopo au kukosa Mkopo nayafahamu, na kila mtu mwenye kufikiria sawa sawa anaweza kuyafahamu bila hata kuyaishi na Rais Magufuli anayafahamu pia.

Kukosa Mkopo au kuchelewa kwa Mkopo tena ukiwa Chuo cha Dar es Salaam ni hatari sana.

Kukosa fedha na kucheleweshewa fedha imekua chanzo cha Dada zetu kujiuza Sinza na Maeneo mengine. Ndalichako hufahamu kweli?

Kukosa na kucheleweshewa fedha imekua chanzo cha vibaka kujaa kwenye viunga vya chuo . Profesa haelewi hili?

Kukosa na kucheleweshewa fedha imekua chanzo cha wanafunzi kuzunguka kwa mamantilie kula ukoko Lakini pia pale Maeneo ya Cafeteria wanaongea na wapishi wanawaibia ukoko ujulikanao kama *Nyengu au zigo pale UDSM* hili Ndalichako hawezi kulifahamu Lakini mimi nilikula ukoko sana nafahamu.

Kuchelewa kwa pesa imekua chanzo cha wasichana kujipeleka peleka kwa Ma Dkta na Ma Profesa. Hili nalo halijui Ndalichako kweli?

Kucheleweshewa fedha kumefanya wanafunzi wengi wanafunga virago kuelekea kwao na kuwaachia elimu watu wengine. Hili nalo hujui Ndalichako?


Mimi niseme tu;elimu ya Tanzania haina manufaa kwa mafanikio na maendeleo ya Mtanzania lakini elimu hiyo hiyo imejaa misukosuko kuipata. Tafadhali Profesa, hangaika na Mfumo wa Elimu ili uache Legacy. Usihangaike na watoto wasio na hatia.

Mwisho. Wanafunzi wote mliofukuzwa popote pale mlipo, Msiumie wala kufa moyo. Mtu yeyote asiye na hatia anapoadhibiwa, adhabu yake hugeuka baraka juu yake. I can guess kwamba, mafanikio mtakayopata kwasababu ya Adhabu ya Ndalichako ni makubwa kuliko elimu mliyokua mnapambania UDSM.

Mungu ni Mwaminifu kila wakati na kila saa. Utafanikiwa kwa kipaji chako wala si kwa elimu ya Ndalichako.
 
Back
Top Bottom