Sihamasishi vurugu, ila huu ndo wakati mzuri wa kufahamu ueledi wa wanafunzi wa vyuo vikuu

Well said mkuu, ingawa kuna situation zinafikia hadi watu wanakosa namna kabisa ya kufanya,
Mkuu nakubaliana nawe. Lakini kwa experience yangu, vijana wengi maisha yao ya chuo yamekuwa magumu kwa kujifanya manunda. Unawakumbuka wale ambao Mzee Mwinyi alidai walimtukana matusi ya nguoni? Kiongozi wao Matiku Matare mpaka leo hii is a failure!
 
Hivi na dunia hii ya leo bado mnatumia majukwaa kuongea ndani ya huu ukomunisti, mnacheza kweli ninyi wanafunzi. Nashauri uongozi wa Daruso watengeneze group la telegram la wanachuo wote tu, afu waongee mambovyao humo, hata kama ni mgomo utaanzia humo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
me natamani waandamane ili nione jinsi watakavo-chezea virungu.

jamani udsm andamaneni please please.
 
sweettablet, Nadhani hata madai yao huyaelewi vizuri na pengine hili swala ama umelikurupukia au umelisikia vibaya.

Madai ya wanafunzi hao si ya kukosa mikopo tu.

Wapo wanafunzi ambao kweli hawajapata mikopo kwa kutokidhi vigezo ambao ni mwaka wa kwanza. Hili sio dai lao kuu kwasabab u hapa kuna taratibu za kufuata

Dai lao kuu ni kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo tangu chuo kifunguliwe takribani miezi miwili sasa hawajapewa hela yao kinyume na makubaliano

Ilitegemewa wanapofungua chuo wanakutana na hela zao kwasababu hawa mkopo wanao tayari

Hao mwaka wa kwanza ambao rufaa zao zimekataliwa ni dai lililoingia katikati. Kifupi ni dai la mengineyo

Hivyo kabla hujajadili hoja jiridhishe kama unafahamu kweli na unachotaka kuchangia vinginevyo kuuliza ni jambo jema zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kingjr2,
Mkuu, taarifa ya Waziri Ndalichako iko humu humu JF. Hapo, tatizo ni mimi au wewe? Mmempotosha dogo mpaka akaondolewa chuoni. Na ninavyojua, hatapata msaada wowote kutoka kwenu zaidi ya serikali yenyewe kumhurumia na kumrudisha chuoni.
 
Mkuu, taarifa ya Waziri Ndalichako iko humu humu JF. Hapo, tatizo ni mimi au wewe? Mmempotosha dogo mpaka akaondolewa chuoni. Na ninavyojua, hatapata msaada wowote kutoka kwenu zaidi ya serikali yenyewe kumhurumia na kumrudisha chuoni.
Wanyime wanao (kama unao), mumeo au mkeo (kama unaye) chakula au haki yake kwa miezi miwili bila sababu za msingi halafu usubiri kujibiwa kwa adabu

Kinachofanyika ni ubabe tu! Na huu ubabe unaendekezwa na watu kama nyie.

Uoga ni dhambi na dhambi huleta mauti!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uoga ni dhambi na dhambi huleta mauti! Huku ndo kunaitwa kukosa weledi! Kwa hiyo tamko la kwanza lilitolewa na baadhi ya wahuni au ni huu huu uongozi uliotoa tamko hili tena?

Kwa hiyo kama Taifa tusiwashangae viongozi wetu wanapokuja na kauli tatanishi au wanapotoa maamuzi yanayokinzana na uhalisia! Ndivyo wanavyoandaliwa vyuoni huko

Leo watasema hivi na kesho watasema vingine! Hawana muda wa kufanya tafakuri ya impact ya wanachotarajia kuleta kwenye jamii

Screenshot_20191219-095212~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani hapo wanadai hali gani? Ili upate mkopo umeambiwa lazima ukidhi vigezo. Hujakidhi. Ukakata rufaa. Ukaahindwa. Unatetea haki gani hapo?

Maoni yangu; badala ya hao vijana kulilia mikopo kwa hoja dhaifu, waombe sheria ya utoaji mikopo ibadilishwe. Kwamba, badala ya kuwa na Bodies ya Mikopo, Admission Letter ya chuo anayopata mwanachuo ndio iwe sifa kuu ya kupata mkopo. Na mikopo itolewe na benki ambazo zitaingia mkataba na serikali ambayo ndio itakuwa mdhamini mkuu kwa kazi hiyo. Kwahiyo, mwanachuo anabeba barua yake anaenda ku bargain na afisa wa benki anataka kiasi gani kwa kila mwaka wake wa masomo. Halafu liwe jukumu la hizo benki kufuatilia marejesho. Hapo kutakuwa hakuna maandamano wala nini!
Bodies - Boards
 
Back
Top Bottom