Sifa za mwanamke

Bak byzo I.T

JF-Expert Member
Jun 29, 2014
264
122
Mwanamke kabla hajaolewa huutunza usichana wake kwani ndio taji peke la heshima pale aolewapo. Ikitokea aliuharibu uschana wake basi hujutia na kutorudia kitendo kile kama mazoea kwake na huwa mbora zaidi akijutia.

Mwanamke huanza kujifunza kwao maisha kwani kwa mume huwa ni mechi lakini mazoezi yote mke hufanyia nyumbani mfano
mapishi, usafi, tabia na nzuri. Mwanamke mwema huwa mnyonge na hawezi shindana kwani sifa ya mwanamke ni utulivu sio ukorofi kama walivo simba jike porini.

Mwanamke anaejielewa hutumia upole kuwa ndio ngao yake kwani hakuna mwanaume anaeweza kushindana na mwanamke mpole asiejali mambo mabaya anayoletewa habari kuwa mumewe kafanya kile nje mwisho mwanaume hujishusha kwa upole wa mkewe.

Mwanamke hodari haambiwi kazi za kufanya na mumewe bali mume humpa pongezi kwa kuona mazuri ndani usafi ni jambo la msingi kabisa ndani. Mwanamke hutambua hali ya uchumi ya mumewe na humshauri katika maendeleo na humuhurumia mumewe hata kama kuna siku karudi hakupata.

Mwanamke anaejielewa humpokea mumewe katika furaha na huzuni hata kama aliokuja nayo mumewe ni masuali ya wazazi wa mume. Mwanamke huwajali wazazi pande zote mbili wengine hutumia ujanja wakawapenda zaidi wazazi wa mume.

Mwanamke sio kujipikilisha anatakiwa kutambua kuwa hilo hatolikwepa kama kifo kupika ukiolewa na jukumu la kusaidiana ambalo mke ni vizuri kujiweka vizuri katika idara ya kumpikia mume vizuri hata kama masikini na hali yao ya kimaisha lakini hupika kikaiva.

Mwanamke humkumbusha mumewe katika amri za MUNGU licha ya kuwa kupata wivu juu ya kuongeza mke hatolifurahia lakini hujitahidi katika kumuamrisha mumewe katika Sala na mambo ya kheri. Mwanamke huwa hatoki ovyo ovyo nyumbani kutoka kwake ni kama dharura iliomlazimu au anasaidiana na mumewe katika kutafuta.
 
Nasubiri part II, "Sifa za Mwanamume"

Wakati mwingine huwa najiuliza lengo la mleta mada naishia kukuna mvi tu....!!
 
Back
Top Bottom