Hata kama umeoa au kuolewa ila kuna yule mpenzi ambaye huwezi msahau

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Nimewakumbuka sana,

Husika na kichwa cha habari hapo juu, umeoa au kuolewa ila Kuna yule mpenzi usiyeweza msahau.

Kama kuna jinamizi linalowatesa wengi waliopo kwenye ndoa ni lile jinamizi la yule mwanamke au mwanaume ambaye Huwa hasauliki kabisa Yani.

Yani huyo mpenzi Wala anaweza akawa hana maajabu kwa kitanda ila ndio hivyo sura yake na hisia naye za mapenzi haziishi kwa muhusika.

Utakuta mlengwa ana mke au mume ambaye yaani anajali anamahaba mvua ila wapi jininamizi la huyo mwanaume au mwanamke linamjia.

Wakati mwingine wakiwa na mumewe au mkewe wanafanya yao hisia zinahama na kwenda kwa huyo mpenzi wa zamani.

Mioyo ingefunguliwa wanandoa wangekimbiana kabisa, maana Siri zilizojoficha ni kubwa mno.

Anasema mwanamke mmoja kuwa tokea ameolewa na mumewe mpenzi walipendana sana.

Mahaba yalikuwa moto moto ila anadai kuwa kulikuwa na tatizo kwake la kumkumbuka mwamba mmoja.

Anadai mwamba mwenyewe si kwamba alikuwa na maajabu six kwa six ila alikuwa akimkumbuka sana.

Nimerudi kwa ufupi...

Donatila
 
Hili ni jinamizi kubwa sana, ambalo linatafuna gen Z na millenial's marriages kwakweli. Ndo maana da maua kule kawasilisha regrets zake juu ya body counts and all. Tujaribu kuassume average ya wanaume, mwanamke anaokuwa ametembea nao kabla ya kuolewa ni watano, though kuna pipo ni mara 10,100 labda...humo ndani inakuaje?. Sawa braza msaf atasema "hayana muongozo" lakini ni very likely kuwa, kuna ambaye atakumbukwa tu pindi mwanamke huyu atakapoingia kwenye maisha ya ndoa, ama familia. Tena hasa kwenye zile nyakati za kiangazi cha ndoa, migogoro etal. Aisee hiki kizazi chetu, Mungu atusaidie tu, bila yeye hatutoboi....HAKIKA!!
 
Asante sana mkuu kwa andiko lako
 
Ndo maana mwenyezi mungu aliharamisha uzinzi kabla ya ndoa ili kuepusha mambo kama hayo.

Huwezi kuwa umeolewa alafu wakati huo uwe unamkumbuka mwanaume uliye kuwa unafanya uzinzi naye ,alafu utegemee kuwa na furaha na hiyo ndoa na huyo aliye kuoa.
 
Back
Top Bottom