Salaam, Shalom,
Ilikuwa yapata kama majira ya saa tatu hivi usiku, tulikuwa tumemaliza kupata chakula Cha usiku, tulikuwa tukijiandaa kufanya Ibada kabla ya kwenda kulala. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 10.
Tukiwa katika kusubiri kuanza Kwa Ibada, nilisikia kishindo kikubwa, yaani nilisikia mlio mkubwa wa kitu kama ubao ukitua sehemu Fulani paaaaaa!!👀, mlio Ule ulitufanya wote kutahamaki kusikilizia Ule mlio na kishindo kile kilitokana na nini,
Baada ya sekunde kadhaa, tulisikia sauti kubwa ya KILIO Cha mwanamke aliyekuwa akilia KILIO Cha uchungu mkubwa, Kwa kuwa mshindo na kelele Ile ya ubao flat uliotua juu ya kitu tusichokijua ulifuatana na sauti ya kulia mwanamke yule, wote tulijua kuwa mwanamke yule ndiye aliyeangukiwa na kitu kile kizito.
Tukiwa katika kuhamaki nini kimetokea, yalisikika maneno ya mwanamke akimlalamikia mumewe kwanini amempiga vile, Mwanaume alisikika akisema nitakuonyesha, Rudi hapa.
Kumbe, Jirani yetu Mr Rwechungura,wa tatu Kutoka ilipokuwa nyumba yetu, aliyekuwa amemuoa mwanamke Kutoka mikoa ya kaskazini mashariki alikuwa akitoa somo la kawaida Kwa mkewe. Nilijiuliza hivi Kweli mwanamke anaweza kupigwa vile na mtu aitwaye mume na maisha yakiendelea?
Mwanamke yule Jirani alikimbilia kwao, na baada ya siku kadhaa ya kuuguza maumivu, alirudi Kwa mumewe na waliendelea na maisha kama kawaida, na vipigo havikukoma ndani ya familia Ile.
Leo Mimi ni mtu mzima, nimeshavuka umri wa Ujana, Bado najiuliza,
Wanaume mnaopiga wake zenu Huwa mnawapiga wapi?
Huwa mnakuwa mmetumia kilevi Gani?
Maana Kwa Utafiti nilioufanya, sijaona sehemu yoyote katika mwili wa mke wangu inayofaa kupigwa.
Kumpiga mke ni kukosa kujiamini, ni kushindwa kuongoza Kwa akili na BUSARA.
Mungu atusaidie.
Karibuni 🙏