Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 39,938
- 61,728
Vitu hivi akivifanya mpenzi wako wa kike jua ni wife material:-
- Anapokuja kukutembelea anakuwa amevaa nguo za heshima
- Akija kwako anaweza kukuletea vitu vya kupika,vya kutafuna tafuna n.k
- Akija kwako atafanya kazi mbalimbali mfano kufua,kupiga deki,kuosha vyombo,kukupikia n.k
- Akipika chakula anakuandalia mezani na anakukaribisha ule.
- Kama atalala kwako,ataamka asubuhi na mapema na atafanya usafi,atapika chai,atakuandalia maji ya kuoga n.k
- Mkiwa katika maongezi kwa asilimia kubwa atakuwa anaongea mambo ya msingi kuhusu maisha yenu ya baadaye mfano watoto,maendeleo,biashara n.k
- Pia anakuwa ni mtu asiyependa kutumia fedha zako hovyo atajitahidi kubana matumizi.
- Kila unapomhitaji anaitikia wito wako
- Anaonyesha unyenyekevu anapokuwa na wewe