Saikolojia ya mwanamke - Fahamu kuhusu mtoto wa kike

Travis Walker

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
323
332
Saikolojia ya Mwanamke
Maelezo haya yanatoa mafunzo kuhusu tabia na akili ya mwanamke wakati anapoingia katika mapenzi na mwanaume. Na hasa mwanamke anapokuwa mrembo, fahamu atakujaribu bila hata ya yeye mwenyewe kujifahamu. Ukiweza kufaulu kwenye majaribu hayo, she feels like wow na anaanza kupenda na kukupa heshima. Lakini ukishindwa kukabiliana na majaribio hayo kinachotokea ni kwamba wewe mwanaume unakua chini yake na yeye mwanamke anakuwa juu. Na hayo ndio matakwa ya mwanamke kwa uhalisia.

Saikolojia 01 : Upendo na Uhitaji
Mwanamke huwa na kawaida ya kuangalia uhitaji wa mwanaume. Anapenda kufahamu ni kwa kiasi gani mwanaume huyu ananipenda na kwa kiasi gani ananihitaji kiasi ya kuwa anashindwa kunikosa. Anapofahamu ya kuwa wewe unahitaji sana kutoka kwake, huanza kutumia udhaifu huo kukamilisha matakwa yake binafsi kama vile kufanya vitu kwa uhuru n.k. Hivyo huanza kuchukua mamlaka tataribu na kujaribu kukudhibiti kupitia huo upendo unao-muonesha. Ili kufaulu hapa unatakiwa kuonesha ya kwamba unamjali lakini na unampenda lakini ujaribu kumfanya akubali ya kuwa sio muhitaji sana kwake. Kwa mfano kama umetaka kitu kutoka kwake na yeye amekunyima usioneshe kuwa ulikuwa unahitaji sana. Nyamaza kimya na wala usirudie kumuomba kila wakati kitu hicho. Ukifanya hivyo, mwanamke hufikria wewe hauna thamani. Lakini unapo onesha ya kwamba huna haja naye sana, kile ulichokitaka utapewa kwa upendo zaidi kuliko kama ungeliendelea kusisitiza. Ukitaka kitu kutoka mwanamke jifanye kama huna haja nacho, atakupa zaidi ya ulivyotaka.

Saikolojia 02: Kusoma mazingira.
Mwanamke huwa na kawaida ya kukusoma tabia zako wewe mwanaume pale munapokuwa katika mahusiano. Wakati unahitaji mapenzi na kutimiza hisia zako, yeye huangalia kwenye tabia zako, jinsi ulivyo, mkarimu, mkatili, mwenye hasira, mpole n.k Yote hayo humsaidia kukufahamu wewe na kuanza kutumia sehemu yenye udhaifu kama ushindi kwake. Hii ni kwasababu mwanamke anapenda sana uhuru wake lakini wakati huo huo anahitaji upendo pia. Kwa mfano, siku za mwanzo mwanzo kwenye ndoa na mahusiano anaweza kutoka bila ya kupata ruhusa, anakuangalia jee utafanyaje? Utakemea au utanyamaza kimya au utachukulia ni jambo la kawaida tu. Hapo huangalia jinsi utavopokea, anapofahamu ya kuwa kitu fulani hakijakukera na wala hukuonesha hisia yoyote katika jambo anaendelea kufanya kitu hicho kwa mara nyingine mpaka anathibitisha ya kuwa hujali kwenye hilo. Sasa siku ambayo utahitaji kumzuia, ndipo hapo ugomvi unaanza. Ili kufaulu hapa, kama kitu chochote hujapenda kutoka kwake ni bora uwe muwazi tokea mwanzo. Watu wengi huharibu hapa, kwasababu mwanamke unampenda sana na labda unahisi kama utaongea chochote anaweza kukuacha unaamua kukaa kimya, fahamu ya kuwa unampa uhuru amabo utakuharimu baadae. Unaposema kitu fulani hukipendi tokea mwanzo mwanamke anatengeza heshima anajua ya kuwa unampenda lakini wakati huo huo unamfanya afahamu ya kuwa maisha yako yana thamani zaidi kuliko mahusiano.

SAIKOLOJIA 03: Vice Versa
Hii ni tabia nyengine ya mwanamke, anaposema kitu fulani atafanya aidha kwa kumuomba au kwa kutaka mwenye, fahamu kuwa kwa 90% hatofanya kitu hicho. Usitie tamaa kabisa kama atafanya, chukulia kama vile hajawahi kukuahidi chochote. Na anaposema kitu fulani hatofanya basi kwa 75% atafanya kitu hicho. Hivyo zikitokezea hali kama hizi usikurupuke wewe mchukulie kama alivyo. Hii ni kwasabau akili ya mwanamke inapoingia kwenye huwa kama mtoto.

SAIKOLOJIA 04: Kudeka au Kujibebisha

Mwanamke hupenda sana kudeka au wanaita kujibebisha, hii ndio asili ya mwanamke na kama utamuona mwanamke hana tabia hiyo aidha ameshaumizwa sana au amerithi tabia za kiume. Hivyo anapojibebisha unatakiwa kuenda nae vizuri. Wanaume wengi pia huharibu hapa, wanapomuona mwanamke anajidekeza wao hukemea tabia hiyo. Kitendo hiki kwa 60% kinapunguza mapenzi kutoka kwake mwanamke. Kauli kama “hemu, niache nipo busy” utazisikia kutoka kwa mwanaume.

SAIKOLOJIA 05: Maamuzi
Hii ni sehemu muhimu sana ambayo mwanaume unatakiwa kufaulu. Mwanamke huwa na kawaida ya kuangalia uamuzi wako. Kwa mfano, tuchukulie mkeo anakwambia baba fulani leo nahitaji ubakie nyumbani usiende kazini. Huenda hapo hakusema hivyo kwasababu ana hamu na wewe, pengine alikuwa anaangalia utachukua uamuzi gani? Ukikubali haraka na mara moja itakuwa umempa thamani na hiyo itamfanya yeye kupoteza mvuto kwako, Ukikataa moja kwa moja unatengeneza picha ya kutomjali. Sasa unafanyaje? Unatakiwa usikubali lakini utafute sababu au sharti. Kwa mfano, unaweza kusema hivi, sawa ukitaka nibakie basi nipige busu au nikumbatie. Mwanaume wa design hizi anavutia sana kwa mwanamke yoyote yule.

SAIKOLOJIA 06: Kuepuka au Kupunguza upendo
Mwanamke pia anakuwa na tabia ya kukuepuka au kuonesha hakupendi tena au kuonesha upendo wake umepungua, na hii inatokea baada ya kuishi nae kwa muda mrefu. Ingawa kwa uhalisia anakuwa anakupenda tena sana lakini hufanya hivyo ili kujua udhaifu wako. Kuangalia jee kwa kutumia silaha hiyo anaweza kukuburuza. Kwasababu matakwa makubwa ya mwanamke ni kumuendesha mwanaume vile anavyotaka yeye. Sasa ili kufaulu jaribio hili, usikurupuke isipokuwa muoneshe wewe upo sawa na hali yoyote hile hata kama kumkosa ikibidi. Wapo wanaume wengine katika hali kama hiyo, huanza kuzalisha mashaka kwenye uhusiano na kummuliza mwanamke unanipenda au kwanini umepungua upendo wako. Unapofanya hivyo tu, kaka unafeli.

SAIKOLOJIA 07: Hofu ya kuachwa.
Mwanamke anapojihakikishia ya kuwa anampenda mtu fulani inakuwa ni kweli kabisa tofauti na mwanaume. Ndio maana mwanamke hawezi kugawa penzi lake, hata kama atakuwa na wanaume 2 au zaidi ya hapo, kuna mmoja anampenda kweli na wengine waliobakia anawadanganya. Sasa, mwanamke huogopa sana kuachwa na mtu anaempenda kwa dhati, jambo hilo humtia hofu sana. Hivyo epuka tabia za kutania kuwa unataka kumuacha mwenza wako. Kwani kufanya hivyo, hupelekea kupunguza mapenzi ya mwanamke na kumfanya ajenge chuki taratibu dhidi yako.

SAIKOLOJIA 08 : Kuweka Refrence
Sijapata kuona sehemu ambayo wanawake wapo vyema kama hapa. Wapo vizuri sana kwenye kuhifadhi mambo. Wewe unaweza kupandisha hasira na kuongea mbovu vya kutosha halafu baada ya muda ukasahau na ukasamehe pia. Lakini mwanamke chochote utachokisema yeye hunakili na kukiweka akilini. Na sio hapo tu, bali hutengeneza tafsiri. Hivyo ni jambo zuri kama ukipandisha hasira kubakia kimya na kutoa maamuzi baadae. Lakini pia unapoweka ahadi kwa mwanamke jikubalishe ya kuwa utatimiza ahadi yako. kwasababu hata iweje ujue mwanamke kitu hicho atakuwa na kumbukumbu nacho. Ni bora usi-ahidi kama huwezi kutekeleza, kwanini? Kwasababu kwa kitu kidogo kama hiko tu, kwa mwanamke kumtia uchungu sana mpaka pale utakapotimiza.

SAIKOLOJIA 09: Hakubali kushindwa
Wanawake wana kitu kinaitwa “Complex Superiority Psychology”. Kisaikolojia hali hii inamfanya mtu kujiona yeye yupo sahihi zaidi au anaweza kufanya kitu kwa ufanisi zaidi kuliko mwengine. Hivyo kwa mwanamke ni bora afe lakini anapoamua kusimamisha misimamo yake huonesha yupo bora sana.
 
Mtoa mada Hii ni chai,
Huu Uzi wako wote haufiki hata kurasa 5 TU ya kilichoandikwa kwenye iki kitabu chote
JamiiForums-204902884.jpg
JamiiForums308654683.jpg
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom