Sifa za mke MWEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa za mke MWEMA

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Bujibuji, May 18, 2011.

 1. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,109
  Trophy Points: 280
  Kitabu cha mithali 31 kuanzia msitari wa 10
  hadi 31 kimeelezea sifa mbalimbali za mke
  mwema, tuangalie kwa uchache sifa hizo
  kwa kuzichambua katika maeneo tofauti.
  1. Imani
  Mithali 31:26, 29, 30
  Mke mwema anayashika na kuyafanyia kazi
  maneno ya Mungu na ni mtu ambaye
  anamtumikia Mungu kwa moyo wake wote
  na akili yake yote. Anatafuta makusudi ya
  Mungu katika maisha yake na kuyafuata.
  Zaburi 119;15
  2. Ndoa
  Mithali 31:11-12, 23, 28
  Mke mwema humuheshimu mume wake na
  anahakikisha anamtendea mambo mema
  siku zote za maisha yake. Ni wa kuaminika
  na msaidizi kwa mume wake. Efeso 5:22-24,
  1Petro 3
  3. Malezi
  Mithali 31: 26, 28
  Mke mwema anawafundisha watoto wake
  njia za Mungu na pia anawatunza kwa
  upendo. Huwafundisha kwa hekima na
  kuwaelekeza njia iwapasayo kuiendea.
  Mithali 22:6
  4. Huduma
  Mithali 31:12-15, 17, 20
  Mke mwema anamhudumia mume wake na
  familia yake yote kwa ukarimu na upendo.
  Anahakikisha wanapata chakula kilicho bora
  na chenye afya. Ni mtu mwenye huruma na
  ukarimu.
  5. Mali
  Mithali 31:14, 16, 18
  Mke mwema anatafuta kwanza ushauri wa
  mumewe kabla ya kutumia fedha na pia
  anafanya manunuzi kwa hekima. Ni
  muangalifu kununua bidhaa zenye ubora
  kulingana na mahitaji ya familia yake.Efeso
  5:23
  6. Nyumba
  Mithali 31:15, 20-22, 27
  Mke mwema ni mtu anayeifanya nyumba
  iwe mahali pa kuishi. Anatengeneza
  mazingira ya kuvutia kwa familia yake na
  wageni wote na anawahudumia watu wake
  wote kwa ukarimu. 1pet 4:9, Ebrania 13:2
  7. Muda
  Mithali 31:13, 19, 27
  Hutumia muda wake vizuri na kuhakikisha
  anakamilisha kazi zake za kila siku. Kamwe
  hapotezi muda katika kufanya mambo
  ambayo hayampendezi Mungu na yasiyo na
  faida.
  8. Uzuri / Urembo
  Mithali 31:10, 21-22, 24
  Ni mrembo na mwenye thamani, ana uzuri
  wa ndani unatoka kwa Yesu Kristo.
  Anatumia ubunifu wake na utanashati wake
  kuleta uzuri katika maisha yake na ya watu
  wake.
  Mungu atusaidie ili maisha yetu yaonyeshe
  kweli tunamjua na kumwamini yeye.
  Ubarikiwe na Bwana Yesu!
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseeeee....
  Kina kaka CHECK LIST ndo hiyo...mshindwe wenyewe!!
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,304
  Likes Received: 22,109
  Trophy Points: 280
  Wanao enda kusake wanawake kwa waganga imekula kwao, shetani kawapiga bao la kisigino
   
 4. O

  Ombeni Charles Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haaaa! Ubarikiwe sana kwa somo la leo. Kuanzia sasa kwa kufuata mtiririko huu nina uhakika ntampata mke mwema. Asante sana MUNGU akubariki wewe pamoja na familia yako yote. Ameeeeeee
   
 5. S

  Sharo hiphop JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wenye hizo sifa tutawatoa wapi? Wapo kweli?
   
 6. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nimekukubali kaka!!!
   
 7. M

  Marytina JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Naamini BF wangu akiisoma hii sredi atamshukuru mungu kukutana na mimi
   
 8. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />
  <br />


  I doubt It,Ww si ndiyo yule Mwanamke aliyekuwa anasema ana kiu na Mzungu? Nafikiri hakujui Vizuri,Embu pitia vizuri hiyo Mithali halafu uone kama una-qualify!
  Ukiniambia kwamba umejifunza kitu katika thread hii ya kiroho na kwamba unataka kuji-revamp ili uwe mke Mwema katika Viwango vya Muumba nitakuelewa,lakini dont suggest kwamba ww ni Mke Mwema ss hv,wewe ni Mwenza tu,upgrade urself now!!
  Please take ths as a challenge and not an insult,no hard feelings!!!
   
 9. I

  Ikunda JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Jul 12, 2010
  Messages: 722
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  dhu! mie ni mwanamke, ila kwa dunia ya sasa wa hivyo kama maandiko yanavyosema unaweza usimpate hata mmoja.
   
 10. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwan waume wenye sifa husika wapo?tutawatoa wap
   
 11. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Humu ndani leo wanandoa.... kweli kazi ipo....
   
 12. c

  chelenje JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu umesahau sifa moja awe na miguu mizuri
   
 13. bacha

  bacha JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 4,336
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135


  hapo kwenye bold nimejikuta nasoma sana na kuparudia rudia,
  kisha nahuisha na uhalisia wa maisha ya sasa,
  nachoka kabisa!!!

  ASANTE MTUMISHI WA BWANA!!!!!!
   
 14. Mtoka Mbali

  Mtoka Mbali JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 238
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Siku hizi kummpata mke mwema ni ndoto.
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  mulinieleza na nikawaelewa
  ule mpango nishaufutilia mbali.
   
 16. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,640
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nzuri sana hii checklist. Ila kwa maisha ya sasa watu kama hao ni wachache sana. Si wanaume au wanawake, wengi ndoa maana yake siyo hiyo uliyosema sababu ndoa zimegeuzwa kama ni ujasiliamali.
   
 17. A

  Aine JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ubarikiwe sana kwa mafundisho hayo
   
 18. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Wapo wengi tu, tatizo ni wapi unatarajia kumpata huyo mwenye sifa - ila kati ya hizo sifa mojawapo ni mcha Mungu kwahiyo tafuta katika wacha Mungu na utampata tu.
   
 19. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  What a useful post.
   
 20. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Asante1 ukimpata mwenye sifa hizi ndoa tamuuu.
   
Loading...