Sifa nyingine ya Augustine Mahiga: Yeye ndiye "Shahidi Y" kwenye kesi ya Uhaini ya mwaka 1982/83

You are right, we would have been better off!! Unfortunately, those who have power have no ideas and those like the JF community who have very good ideas have no power!!!!

Precisely.
 
K alituponza, watu wakaona upole sio sifa.

Sikubaliani na wewe kuwa Jakaya alikuwa mpole; alikuwa ni mtu wa visasi na mnafiki aliyekuwa anatumia tabasamu lake kuficha uovu wake!!! Unlike Dr. Mahiga , Vasco Dagama hakuwa makini, mtu wa kubembea zaidi [ Boys to men!!]
 
Shukrani sana mkuu
Nyakati zimebadilika halafu vyombo vya kimataifa kama UN na AU zikikuwekea vikwazo hufiki popote. Hata nchi za West Africa hususan Nigeria na Ghana ambazo zilikuwa na matukio mengi ya mapinduzi toka majeshini ziliacha before mid 1990s.

Pili demokrasia ya vyama vingi ikiheshimiwa ndiyo suluhisho la kuutoa utawala mbovu usiokidhi matarajio ya raia kwenye uongozi. Ndiyo maana tunawashangaa hawa akina Pole Pole na Bashiru Ally wanapomsaidia Magufuli kuuua UPINZANI kwa kununua wabunge au akina **** Nkamia wanaposhabikia kuongeza muda wa Rais kutawala.

Hawa wote inabidi tuwachukie kama ugonjwa wa COVID19 kwa kuwa wanatupeleka kwenye nyakati za giza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikubaliani na wewe kuwa Jakaya alikuwa mpole; alikuwa ni mtu wa visasi na mnafiki aliyekuwa anatumia tabasamu lake kuficha uovu wake!!! Unlike Dr. Mahiga , Vasco Dagama hakuwa makini, mtu wa kubembea zaidi [ Boys to men!!]
JK had the weakest ego ndiyo maana tumefika hapa tulipo. Alishindwa kumanage power succession kwa kumg'ang'ania Bernard Membe na kumtosa hasimu wake wa kisiasa na mshirika wake wa zamani Edward Lowassa. Hatimaye tukadondokea kwa mtu asiyejuwa uongozi wa nchi zaidi ya kufanya visasi na kutekeleza miradi mikubwa bila mipango.
 
Mkuu Joka Kuu umenikumbusha mbali!

Tulikuwa tunaishi Drive In Estate, mafleti next to Banyikwas, nyumba zimeungana na kutenganushwa na ukuta. Mzee wa Kihangaza, mke Mhangaza, alikuwa na mabinti 4 bomba sana!, Hope, Daines, Betty na Ngola na kaka yao mmoja Mzomu. Hapo ndipo vikao vilipo fanyikia!.

Kesi hiyo ilikuwa na similarities nyingi na Kesi ya Mauaji Mwanza, Mzee wangu, Andrew Mayalla ndio alikuwa RSO wa Mwanza, Jaji alikuwa Nassor Mzavas, DPP alikuwa William Sekule, Mzee wangu alitetewa na wakili Murtaza Lakha, ndie pekee alichomoka, wengine wote walikula mvua nyingi!.

Murtaza Lakha alinifanya nitamani kuwa wakili, by then ukikosa 1st class forget law, ndio nika-opt journalism, he was the best na mpaka sasa bado sijaona wakili yoyote Tanzania aliye vaa viatu vyake!.
P

kwahiyo baada ya mzee wako kuchomoka kwenye kesi ya uhaini alirudishwa kazini na katika nafasi yake.?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Stuxnet,

Kwa maoni yangu, upande wa UTETEZI ndiyo uliotia fora ukiongozwa na Wakili MURTAZA LAKHA.

Kwa kweli Murtaza Lakha alikuwa na maswali ya kuwachachafya sana mashahidi wa upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka ulikuwa na wakili anaitwa William Sekule ambaye alifanya kazi nzuri sana ktk kuhitimisha kesi na kuchambua ushahidi na kuuunganisha na washtakiwa.

cc Nguruvi3, Pascal Mayalla
Mzee wangu ni mtu mkimya sana ila kuna siku aliamua kufunguka kuhusu hawa jamaa na mambo waliyoifanyia nchi kuanzia miaka ya 1975-1995 (The Golden Age of Tanzanian Intelligence), kiukweli mwili wangu ulisisimka maana kuna wazee nilikuwa nawafahamu lakini nilikuwa nawachukulia kawaida. Ila kilichonishangaza sana ni kwamba wengi wao kwenye ile orodha walikuwa ni watu wa Njombe na Iringa. Alinisimulia kidogo kuhusu Mzee wetu Comrade Mizengo Peter Pinda na sehemu alizotembelea huko Mashariki ya Kati akiwa na wenzake fulani hivi (Majina Kapuni) siku hizi ni mabalozi wastaafu.

Kuna mambo kafanya Mzee Mahiga ambayo binafsi baada ya kuyafahamu yalinifanya nitokee kumkubali sana yule Mzee wetu.
Japo kuna wengine ambao pia mchango wao ni mkubwa sana japo kutokana na kazi zao hawawezi kufahamika kirahisi, kuna watu kama marehemu wazee wetu wakina Peter Siyovelwa (mbali na ukauzu wake mchango wake ulikuwa mkubwa sana), Mzee Kaduma, Mzee Mayagila na wengine ambao siyo vyema kuwataja maana bado wapo hai.

Nilitamani sana kuandika kitabu kama kumbukizi ya haya matukio, maana kuna baadhi ya wahusika ambao ni rafiki wa mzee wangu walisema kwamba wangenisaidia lakini nikafikiri kwamba sheria zetu za nchi siyo rafiki na naweza kuandika kwa nia njema kabisa halafu nikaishia kuvurugwa tu au kupitiwa na kuandika mambo ambaya sikutakiwa kuyaandika.

Leo niko Iringa mjini na nilitamani sana kwenda Tosamaganga kumzika Mzee wangu Mahiga lakini nimeshindwa kwenda kwasababu kuna mambo hayajakaa sawa kidogo na vikwazo vimekuwa vingi sana. Lakini Mungu amlaze mahali pema sana huyu Mzee wetu na aipe faraja kubwa familia yake. Tanzania imepata pigo kubwa sana kwa kifo chake, yeye ni kati ya wa Tanzania wachache sana ambao ni wajenzi wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania (Architects of Tanzania's Foreign Policy) akiwa nyuma ya wanasiasa nguli kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Oscar Kambona, Mzee Job Lusinde, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Abdulrahaman Mohamed Babu, Mzee Mkapa na wazalendo wengine.....

Ambassador MAHIGA was The Man, The Myth and The Legend.........
 
Mkuu Joka Kuu umenikumbusha mbali!

Tulikuwa tunaishi Drive In Estate, mafleti next to Banyikwas, nyumba zimeungana na kutenganushwa na ukuta. Mzee wa Kihangaza, mke Mhangaza, alikuwa na mabinti 4 bomba sana!, Hope, Daines, Betty na Ngola na kaka yao mmoja Mzomu. Hapo ndipo vikao vilipo fanyikia!.

Kesi hiyo ilikuwa na similarities nyingi na Kesi ya Mauaji Mwanza, Mzee wangu, Andrew Mayalla ndio alikuwa RSO wa Mwanza, Jaji alikuwa Nassor Mzavas, DPP alikuwa William Sekule, Mzee wangu alitetewa na wakili Murtaza Lakha, ndie pekee alichomoka, wengine wote walikula mvua nyingi!.

Murtaza Lakha alinifanya nitamani kuwa wakili, by then ukikosa 1st class forget law, ndio nika-opt journalism, he was the best na mpaka sasa bado sijaona wakili yoyote Tanzania aliye vaa viatu vyake!.
P
Inasemekana Baba yako alikuwa mtu mwema na mwenye akili sana na hata mama yako pia naye alikuwa na uwezo mzuri sana kichwani (Hizi ni habari za wambea). Lakini mbona wewe umekuwa ni mtu wa ajabu na hovyo-hovyo kihivi, au vinasaba vya akili vya wazazi wako vimekuruka wewe na kwenda kwa wajukuu ? Man you're a disappointment.....

NO HARD FEELINGS...........
 
Inasemekana Baba yako alikuwa mtu mwena na mwenye akili sana na hata mama yako pia naye alikuwa na uwezo mzuri sana kichwani (Hizi ni habari za wambea). Lakini mbona wewe umekuwa ni mtu wa ajabu na hovyo-hovyo kihivi, au vinasaba vya akili vya wazazi wako vimekuruka wewe na kwenda kwa wajukuu ? Man you're a disappointment.....

NO HARD FEELINGS...........
Usipompenda mtu lazima atakudisapoint,

Mlimchukia tu kwani pachal na mkapa wanatofauti gani katika nyanja ya habari? Au kwa kuwa yeye alikuwa na back up ya Mzee N
Sawa bana maana kama ukuonekana form six basi jitafutie mwenyewe nafasi serikalini
 
Kwa taarifa yako, figure zote zenye kalba ya bashe na zaidi ni kitengo!
Si wapinzani wala watawala...
Mbatia, hakupewa ubunge na jk bure..

Sent from my iPhone using JamiiForums
Bashe huyu huyu na yeye kitengo?
 
Mzee wangu ni mtu mkimya sana ila kuna siku aliamua kufunguka kuhusu hawa jamaa na mambo waliyoifanyia nchi kuanzia miaka ya 1975-1995 (The Golden Age of Tanzanian Intelligence), kiukweli mwili wangu ulisisimka maana kuna wazee nilikuwa nawafahamu lakini nilikuwa nawachukulia kawaida. Ila kilichonishangaza sana ni kwamba wengi wao kwenye ile orodha walikuwa ni watu wa Njombe na Iringa. Alinisimulia kidogo kuhusu Mzee wetu Comrade Mizengo Peter Pinda na sehemu alizotembelea huko Mashariki ya Kati akiwa na wenzake fulani hivi (Majina Kapuni) siku hizi ni mabalozi wastaafu.

Kuna mambo kafanya Mzee Mahiga ambayo binafsi baada ya kuyafahamu yalinifanya nitokee kumkubali sana yule Mzee wetu.
Japo kuna wengine ambao pia mchango wao ni mkubwa sana japo kutokana na kazi zao hawawezi kufahamika kirahisi, kuna watu kama marehemu wazee wetu wakina Peter Siyovelwa (mbali na ukauzu wake mchango wake ulikuwa mkubwa sana), Mzee Kaduma, Mzee Mayagila na wengine ambao siyo vyema kuwataja maana bado wapo hai.

Nilitamani sana kuandika kitabu kama kumbukizi ya haya matukio, maana kuna baadhi ya wahusika ambao ni rafiki wa mzee wangu walisema kwamba wangenisaidia lakini nikafikiri kwamba sheria zetu za nchi siyo rafiki na naweza kuandika kwa nia njema kabisa halafu nikaishia kuvurugwa tu au kupitiwa na kuandika mambo ambaya sikutakiwa kuyaandika.

Leo niko Iringa mjini na nilitamani sana kwenda Tosamaganga kumzika Mzee wangu Mahiga lakini nimeshindwa kwenda kwasababu kuna mambo hayajakaa sawa kidogo na vikwazo vimekuwa vingi sana. Lakini Mungu amlaze mahali pema sana huyu Mzee wetu na aipe faraja kubwa familia yake. Tanzania imepata pigo kubwa sana kwa kifo chake, yeye ni kati ya wa Tanzania wachache sana ambao ni wajenzi wa sera ya mambo ya nje ya Tanzania (Architects of Tanzania's Foreign Policy) akiwa nyuma ya wanasiasa nguli kama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mzee Oscar Kambona, Mzee Job Lusinde, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Abdulrahaman Mohamed Babu, Mzee Mkapa na wazalendo wengine.....

Ambassador MAHIGA was The Man, The Myth and The Legend.........
Marehemu Mahiga vile vile ni architect wa Serikali ya Somali ya Kidemokrasia iliyopo sasa. Mwaka 1991 Ban Kin Moon alimteua Mahiga kuwa UN special envoy and head wa UN Political Office for Somalia (UNOPS). Alijudumu huko hadi 2013 na ndipo alishuhudia utiwaji mkataba wa amani kati ya makundi hasimu na kuanza kwa Serikali ya kwanza ya kiraia baada ya miaka kama 20. Hakika gwiji wa diplomasia za kimataifa amedondoka.
 
Kuna mambo kafanya Mzee Mahiga ambayo binafsi baada ya kuyafahamu yalinifanya nitokee kumkubali sana yule Mzee wetu.
Japo kuna wengine ambao pia mchango wao ni mkubwa sana japo kutokana na kazi zao hawawezi kufahamika kirahisi, kuna watu kama marehemu wazee wetu wakina Peter Siyovelwa (mbali na ukauzu wake mchango wake ulikuwa mkubwa sana), Mzee Kaduma, Mzee Mayagila na wengine ambao siyo vyema kuwataja maana bado wapo hai.

Achana na mazuri mengi niliyojifunza kwenye bandiko lako, jicho langu baya limetua kwenye huo tu mstari wa mwisho.... mbona kusubiri wafe.?
 
Back
Top Bottom