misasa
JF-Expert Member
- Feb 5, 2014
- 13,642
- 9,338
Duh! Na utajiri kautolea wapi wakati alikuwa mtumishi wa serikali? Na huyo Harry yupo hai?Hans Pope (senior) alikuwa Regional Police Commander, Iringa, kabla ya kupelekwa Mkoa wa Ziwa Magharibi (West Lake Region) ambao sasa ni Kagera. Nakumbuka picha yake ilipochapishwa magazetini hapa nchini, 1972, baada ya kuuawa na askari wa Amin waliomteka Mutukula.
Katika picha ile, mwili wake ulivimba sana. Amin alisema jeshi letu lilikuwa na Wachina na Hans Pope ulikuwa ndiyo ushahidi huo. Hans Pope alikuwa na damu ya Kijerumani, siyo ya Kichaina, ingawa sura yake katika picha ile ilikuwa kama ya "Kichaina" kwa sababu ya kuvimba sana. Naikumbuka sana picha ile. Ilikuwa ukurasa wa kwanza magazetini.
Watoto wake ndiyo hao wawili Zacharia na Harry waliohusika na mpango wa kumpindua Nyerere, 1982, pamoja na wanajeshi wengine.
Zacharia alikuwa captain kikosi cha mabomu na Harry (RIP) alikuwa rubani wa Airwing. Walishawishiwa kuingia kwenye uhaini kwa hisia kuwa Nyerere kumsababisha kifo cha baba yao kwa kumpeleka kuwa RPC Wes Lake Region .