Kuna dada alileta mada hapa jukwaani akisema bikira ni overrated, na moja ya sababu zake ni kuhoji mwanaume anaanzaje kuoa mwanamke wa kijijini kisa tu ni bikira, akiamini kuwa hamtaendana kwenye kiwango cha kufikiri (thinking level). Pia, aligusia suala la bikira kuwa ni maumbile tu yanayoweza kubadilika au kuchoka, huku akionyesha kuwa mwanamke msomi mwenye exposure ndiye bora akimaanisha mtu aliyetembea na wanaume wengi na kupitia mahusiano mengi ndiye mwenye akili za maisha na uelewa.
Hoja yake hii imejaa dharau ya kifikra (class elitism) na upotoshaji wa wazi. Kwanza kabisa, bikira sio suala la maumbile au bahati mbaya; ni maadili, nidhamu, na maamuzi ya heshima anayochukua mtu kujitunza. Kutunza bikira ni uthibitisho wa uwezo mkubwa wa kujicontrol na kusimamia misingi ya maadili, jambo ambalo ni nguzo kuu na ya msingi sana katika kujenga ndoa imara na yenye kuaminika.
Pia, kudai kuwa mwanamke wa kijijini hana akili au kwamba uzoefu wa kutembea na wanaume wengi (body count) ndio "exposure" na uelevu wa maisha ni mtego wa kifikra (emotional fallacy). Idadi ya mahusiano au kuishi mjini haimfanyi mtu kuwa na akili za maisha au ukomavu wa ndoa. Mwanamke aliyejitunza na mwenye maadili ana thamani kubwa na uwezo wa juu wa kuwa mwanandoa bora kuliko mtu anayetumia kashfa za kijinga kuhalalisha ukosefu wa nidhamu na maadili.
vipi bibi yako mzaa baba yako au mama yako ni Gen Z?
kama sio manake ni wale watu wa vijijini je naye unamchukulia poa alishindwa kuendesha familia yake kwa kukosa hizo exposure? mbona umepatikana na watu wa ukoo mzima mnagangania mali za urithi unadhani babu yako mlevi pekee kijijini ndo alikuwa bora kifikra.