Sifa hizi zikufanye ukajitegemee

Sifa hizi zikufanye ukajitegemee

Mangwea1900

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2025
Posts
2,485
Reaction score
3,224
Inatia aibu na fedheha kijana umeshamaliza shule kwa ngazi yoyote na bado unakaza chogo na komwe nyumbani kwa wazazi wako. Kwa sifa hizi beba begi au mfumo wa Jero ukapambane mbele kwa mbele;
1. Umefika umri wa miaka 25 na haupo shuleni kwa ngazi yoyote.
2. Unaona hali ya familia haiwezi kukuendeleza kwa elimu yoyote.
3. Wazazi wako umri umeenda na uwepo wako unakuwa ni mzigo kwao, fungua macho na masikio utaona unavyowalemea.
4. Una afya njema na hauna ulemavu wa akili wala kimwili.
5. Kwa sababu yoyote umezalia nyumbani au umetupiwa mtoto/watoto na mwanamke/wanawake zako.
USIKAE NYUMBANI UTALEMAA AKILI NA MWILI, USIOE KWENYE NYUMBA AMBAYO WAZAZI WAKO WANAISHI HAPO.
OMBI LANGU KWA WAZAZI WOTE KAMA UNA MTOTO UNAONA HATAKI KWENDA KUJITEGEMEA NIPE TAARIFA NITAKUJA KUKUSAUDIA AU KUKUPA MBINU ZA KUMFUKUZA.
 
Mbona wahindi huko mijini hawaondokagi na wanaishi TU!
Wazazi wana jumba kubwa ukahangaike kwenda kupanga huko kwa shida zipi!
Unasaka maisha jioni unarudi home 😁
Huku juu nyumba ni nyingi kiasi kwamba wazee huomba watoto wa ndugu waje wakaenao 🤔
 
Mbona wahindi huko mijini hawaondokagi na wanaishi TU!
Wazazi wana jumba kubwa ukahangaike kwenda kupanga huko kwa shida zipi!
Unasaka maisha jioni unarudi home 😁
Huku juu nyumba ni nyingi kiasi kwamba wazee huomba watoto wa ndugu waje wakaenao 🤔
Umeshasema wahindi tabia za watoto wao ni tofauti kabisa.Mitoto ya kiafrika kazi kuiba na kutapanya mali za nyumbani. Mnatakiwa mkanitegemee ukitoka kazini unaelekea ghetoni kwako
 
Sie Wengine wazazi wetu hawataki tukajitegemee, ko tunatimiza matakwa yao kwa kubaki home.
 
Back
Top Bottom