Siendi Arusha

Siendi Arusha

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Tumepokea ujumbe toka Makao Makuu ya CCM kuwa tunatakiwa kwenda Arusha kuhakikisha kuwa Wagombea wetu wa Udiwani katika Kata zinazorudia uchaguzi hapo Juni 16 wanaibuka na ushindi. Eti,tutoke hapa Dodoma mapema ili tuwahi Arusha kuanza 'kuwalisha sumu' wapigakura wa Arusha katika Kata husika. Eti,chama chetu kimejipanga kuibuka washindi dhidi ya wapinzani wetu hasa CHADEMA.

Mimi siendi Arusha. Tumeshashindwa kabisa uchaguzi huo wa Madiwani Arusha. Arusha CCM haiuziki,haiaminiki. Tulijitahidi kuwalaghai Madiwani wa zamani wa Kata hizo ili wahamie CCM. Wakakataa kuhama lakini wakaahidi kuwa 'kiburi' kwa CHADEMA. Wakafanya kweli.Wakafukuzwa. Sasa wanajiandaa kuhamia rasmi CCM na kusimamishwa kama Wagombea wetu.

Hatahivyo, siendi Arusha. Hao Madiwani wote wa zamani sasa hawaaminiki Arusha.Ni wasaliti kwa CHADEMA na wapigakura wao. Hawataweza kuiepusha aibu ya CCM pale Arusha. Nani atapambana jukwaani na Lema? Nani atamzidi kete Mawazo wa Sombetini? Sipo tayari kwenda kujidhalilisha. Arusha si mahali pa kwenda.

Pamoja na Tume ya Uchaguzi kupanga uchaguzi mwezi wa sita ili 'kuwazuia' akina-Lema Bungeni,bado niwajuavyo CHADEMA,wana timu kabambe ya kampeni hata bila Lema wa Arusha. Kwa hili la kwenda Arusha kusimamia harakati za uchaguzi wa Madiwani,nipo tayari kulaumiwa.Mimi siendi. Nitabaki hapa Dodoma kushuhudia 'vituko' vya Wabunge wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nieleweke kuwa: Arusha siendi.

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)
 
Mkuu neenda katusaidie kwa interejensia...huuo mziki hata mwenyekiti taifa wa maCCM atakuwa hataki kwenda,
makamanda Mungi Arushaone na webgine anzeni kujipanga...kata26 ila za Arusha zina mvuto wake...
 
Last edited by a moderator:
Umesema kweli hawo watu wameshatupiwa nyanya ,wametemewa mate,wamenyimwa kununua bidhaa madukani,wamezomewa sana mahakamani mpaka wakaacha kwenda,wamelipa fedha za faini mahakamani,utawauzaje watu hao,ina maana hawana kabisa watu wengine wakuwasimamisha nani atakayepita kati ya hao wanaozomewa mpaka leo wakipita barabarani wako kwenye tinted sio vibaya ukienda kuandalia vituko,
 
Hivi bado CCM wanasimamisha tu wagombea huko Arusha!!
 
Mkuu neenda katusaidie kwa interejensia...huuo mziki hata mwenyekiti taifa wa maCCM atakuwa hataki kwenda,
makamanda Mungi Arushaone na webgine anzeni kujipanga...kata26 ila za Arusha zina mvuto wake...

Mkuu POMPO huku usipate shida........................... ni kama unamsukuma mlevi.......
Kumbuka kata ya Daraja II ccm yote ilihamia kule, ukizingatia ilikuwa kata yao, lakini baada ya matokeo walikimbia kila moja njia yake.
 
Last edited by a moderator:
waende makomredi,NCHEMBA
LUSINDE
NKAMIA
SERUKAMBA.
wakipiga matusi kidogo tu CHADEMA chaliii!!!
 
Back
Top Bottom