Siendi Arusha

Siendi Arusha

Huko ni kukariri, watu wanatia timu. CCM haitishiwi simba wa kuchora. Ushindi unapatikana uwanjani sio mezani.
 
Hamia CCM Mkuu najua wewe ni mwana Chadomo unaogopa magaidi wenzako.Kuwapa Magaidi Arusha kutapunguza Utalii na maendeleo kwa ujumla wa mji wa Arusha.

KINANA images.jpg PEMBE ZA NDOVU..jpg KINANA.jpg PEMBEZA NDOVU.jpg
 
Mkuu usiende wanataka kukufanya chambo bora umeshituka mapema MATOKEO YA ARUSHA YANAJULIKANA BILA KUFANYA KAMPENI!!!!!!!!!!!!!
 
mkuu matusi kwenu imekua ndo sera ya chama au
Lema kachuja, the so called makamanda wameshamchoka na vituko vyake, wanadai kachemka sana, CCM ina nafasi ya kushinda Arusha, hata Lema akiwepo, mbowe, kibabu na wengineo, mje wote, ili tushinde fair and square, tutakuwepo sisi, chama si mtu mmoja, na haijawahi tokea hivyo,
 
Tumepokea ujumbe toka Makao Makuu ya CCM kuwa tunatakiwa kwenda Arusha kuhakikisha kuwa Wagombea wetu wa Udiwani katika Kata zinazorudia uchaguzi hapo Juni 16 wanaibuka na ushindi. Eti,tutoke hapa Dodoma mapema ili tuwahi Arusha kuanza 'kuwalisha sumu' wapigakura wa Arusha katika Kata husika. Eti,chama chetu kimejipanga kuibuka washindi dhidi ya wapinzani wetu hasa CHADEMA.

Mimi siendi Arusha. Tumeshashindwa kabisa uchaguzi huo wa Madiwani Arusha. Arusha CCM haiuziki,haiaminiki. Tulijitahidi kuwalaghai Madiwani wa zamani wa Kata hizo ili wahamie CCM. Wakakataa kuhama lakini wakaahidi kuwa 'kiburi' kwa CHADEMA. Wakafanya kweli.Wakafukuzwa. Sasa wanajiandaa kuhamia rasmi CCM na kusimamishwa kama Wagombea wetu.

Hatahivyo, siendi Arusha. Hao Madiwani wote wa zamani sasa hawaaminiki Arusha.Ni wasaliti kwa CHADEMA na wapigakura wao. Hawataweza kuiepusha aibu ya CCM pale Arusha. Nani atapambana jukwaani na Lema? Nani atamzidi kete Mawazo wa Sombetini? Sipo tayari kwenda kujidhalilisha. Arusha si mahali pa kwenda.

Pamoja na Tume ya Uchaguzi kupanga uchaguzi mwezi wa sita ili 'kuwazuia' akina-Lema Bungeni,bado niwajuavyo CHADEMA,wana timu kabambe ya kampeni hata bila Lema wa Arusha. Kwa hili la kwenda Arusha kusimamia harakati za uchaguzi wa Madiwani,nipo tayari kulaumiwa.Mimi siendi. Nitabaki hapa Dodoma kushuhudia 'vituko' vya Wabunge wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nieleweke kuwa: Arusha siendi.

VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam(sasa Dodoma)

Mkuu, kwani huko hakuna Posho, kwanini usiende tu, we nenda, Tafuta Lodge ya Maana, tafuta Mtoto wa Kimasai Kula Maisha, Ndani Mwanzo mwisho
 
Nimevutiwa sana na style yako ya uandishi...!!! Pia nakusisitizia, Usiende Arusha!
 
Siku zote habari za VUTA NKUVUTE hua naziaminia sana,usiende kiongozi waache Magamba wakaumbuliwe.
 
Mkuu nakushauri uende, kama unabaki dodoma ili kuangalia vituko vya wabunge sasa ni muda wa kubadili aina ya vituko, unaachana na vituko vya lusinde,nchemba unaenda kushuhudia vya nape na kinana.
 
waende makomredi,NCHEMBA
LUSINDE
NKAMIA
SERUKAMBA.
wakipiga matusi kidogo tu CHADEMA chaliii!!!
Hamuwatakii mema hao wawakilishi wa wananchi wao? Nina wasiwasi Arusha bado wana kumbukumbu za matusi ya Lusinde kule Arumeru.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mimi na familia yangu tunakwenda kukiadhibu chama cha mapinduzi kwa kuhakikisha CHADEMA inashinda kata zote tano ikiwemo kata yangu.

Nashukuru mungu kina mama, kina baba, vijana na wote wenye vigezo vya kupiga kura wanajua kuwa CCM ni chama cha kiharamia na mkombozi pekee ni CHADEMA.

Tumejiandaa vema kuwatandika ccm na baada ya hapo meya wa kichina tunamtoa kwa kura na halmashauri inarejeshwa kwenye mikono salama ya CHADEMA.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mkuu POMPO huku usipate shida........................... ni kama unamsukuma mlevi.......
Kumbuka kata ya Daraja II ccm yote ilihamia kule, ukizingatia ilikuwa kata yao, lakini baada ya matokeo walikimbia kila moja njia yake.

Hawakuamin walichokiona,kama Arumeru kwa Nasari vile.,HAKIKA KASKASNI CCM WASAHAU.,Edo yupo pale kwa heshima ya wasee.
 
Last edited by a moderator:
Hakiamungu nawaapia ya kwamba siasa ni mchezo mgumu lakini katika kurudi uchaguzi huu wa sehemu zote zilizowazi nawaakikishieni ya kwamba mafisadi ccm hawatanyakua hata jimbo moja! Hata CDM wasipofanya kampeni nawaambia majimbo yote yako wazi! Hapa A town nawasihi mafisadi wakajaribu bahati yao kwingine na nawapa pole ya kinafiki!
 
Huwa nakukubali mkuu VUTA-NKUVUTE, goma kwenda bwana yanini kujitia aibu huko?
 
Last edited by a moderator:
Ni sehemu ya utalii na kukuza kipato pia sio uchaguzi tu, subiri utakapoona majukwaa ya wasanii na viongozi wa kitaifa na V8 zao kule huku mvua za Takrima zikinyesha vitakavyoshuhudiwa, Halafu Mzungu akisema .... Kuhusu rushwa Tunataka kuandamana kwa kumdhalilisha mkuu wetu.
 
Arusha hata Nape hatapoteza muda kuchungulia, ataishia Moshi.

Nina hamu kubwa na Mwigulu na Lusinde waje Arusha, wataaibika vilivyo.

Jamani hii si nzuri make itaturejesha kwenye kumbukumbu ya majonzi ya USA river RIP kamanda!
 
Back
Top Bottom