Sielewi dhamira ya huyu dada kwangu

Sielewi dhamira ya huyu dada kwangu

Wakuu,mimi kuna nyumba moja nimepanga huku kitaani kwetu ni nyumba quality sana miongoni mwa nyumba za namna hii chache hapa mtaani kiasi kwamba mandhari yake yapo safi sana pametulia wapangaji tupo wawili tuu na hawo wenye nyumba kwa upande wao wanasehemu yao kulingana na mtindo wa nyumba hii ulivyo,sasa lengo langu si kueleza nyumba hii ila ni haya yanayonikuta.

Nimehamia nyumba hii,huu ni mwezi wa pili sasa tokea nihamie mwezi wa tano mwishoni,hapa kuna mama mwenye nyumba anayejiweza kiuchumi kwan anamiliki maduka ya nguo na ana hospitali yake ndogo hivi.Huyu mama huwa hashindi sana nyumbani kutokana na hizo shughuli zake anazosimamia kwahivyo unaweza ukaonana naye mara mbili au tatu kwa wiki na smtmz huwa anasafiri kabisa,sasa hapa nyumbani kuna binti yake wa kwanza yupo na mdogo wake anayesoma sekondari moja hivi japokuwa mara nyingi anayeshinda nyumbani ni huyu dada na housegirl tuu.Huyu dada anafanyia kazi kwenye hospital ile ya mamaake kwahivyo kapewa kitengo pale.

Shida iliyopo huyu dada simuelewi kabisa ndugu zanguni vijana wa siku hizi huwa wanasema HASOMEKI,yaani nimeshindwa kumsoma kabisa.kuna vituko na mambo ambayo huwa nayaona hata sipati picha mantiki yake.Huyu dada huwa ananichukia chukia tuu,akiniona nimetoka kazini tu punde ataanza kujifanya anaanzisha stori na yule housegirl wataanza kuongea majungu kwa sauti na ukitafsiri utagundua yanakulenga moja kwa moja.Utakuta wanasema tabia za kabila langu huku wakicheka,mara idara nayofanyia kazi wanaikashfu kwa vicheko japo hawanitaji mimi.Sometimes tukionana hivi anapenda nianze kumsalimia na mara nyingi mimi huwa namuanza na nikimsalimia anaitikia sauti kama yupo shimoni tena kwa madoido hivi.

Kuna siku nimetoka kazini niko ubao nawaza kuanza kukiwasha kigae nifanye harakati za chakula akamtuma housegirl msosi kwenye hot pot kukiwa ni ndizi na samaki tena inaonyesha viliandaliwa special to somebody,mimi kwasababu nilkrahisishiwa process nikakila huku nikifikiria mara mbili mbili hivi.Baada ya kula,nikaenda kumgongea mlango hakufungua yeye akamtuma yule housegirl kwa niaba yake zaidi nikamwambia yule housegirl nashukuruni baasi.Jana umeme uliisha sasa huwa kuna uraratibu wa kulipa ilibidi nilipe mimi sasa sikuwepo nikakuta amelipa kwa niaba yangu tena akazidisha kiwango ambacho huwa kila mpangaji anatakiwa kununua na akanunua umeme,Nilishangas sana kwani sielewi.Lakini kinachonishangaza ni kila tunapoonana yaani ananiangalia kwa chuki flani hivi anachange sura(kama anataka kusonya) na hajawahipiga stori na mimi hata siku moja

Hivi kwa namna hii huyu mtu mnamkadiriaje.sijui dhamira yake kwangu nashindwa kutabiri malengo yake kwangu wakuu(huyu dada kanizidi miaka 2 tuu).

Ni hilo tuu,mawazo yenu wataalamu wa saikolojia za wanadamu.
Kwa hili andiko wewe ndio haueleweki, kwa maana nyingine nyuki wa ..............
 
leta demu kutoka kitaa siku moja hapo nyumbani kichaa chake kitapona siku hiyo hiyo
 
Inaonekana aura zenu haziendani.


Ila kwa kichekesho tu, subiri housegirl wao akiondoka mvizie uingie jikoni kwao kamata kopo la chumvi kaza kabisa alafu rudi chumbani kwako kulala
Nakuhakikishia lazima atakuja mwenyewe kukuonba ukamfungulie
hahahaha ni nomaaa
 
Tangaza nia uone sio kuletewa chakula na kulipiwa luku tu na kodi utasamehewa ukae kwa mkwe bure haa haaaaaa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu umetisha,inaonesha unapenda sana fairness dadeek
 
baada ya kununua umeme badala yako hivi pesa yake ulimrudishia?
 
jaribu kufuata kanuni na taratibu za uandishi, umeandika hovyo hovyo mno, haivutii kusoma, fanya editing then rudi tukupe ushauri.

NB; kwani upo kidato cha ngapi?
Nyinyi ndiyo mabongo lala wenyewe, ukishajua kidato chake itakusaidia nini?

Humu hatupo kukaguana kanuni za uandishi, ukielewa toa ushauri usipoelewa kaa kimya tu. Kama ingekuwa kinaangaliwa hiko, mods wangekuwa wanaapprove uzi kwanza kabla ya kusoma kwa kila jukwaa.

Ukiona hakuna hiko tambua kila mmoja ana namna ya kuandika ilimradi havunji kanuni za mtandao, hebu acha dharau zako hizo.
 
Mleta uzi nina ushauri ninahitaji kukupa ila nina wasiwasi utaweza kukuharibia kabisa mkachukiana
 
Inaonyesha wewe ni mshamba fulani wanahaki ya kukudharau maana kwa uandishi huu dah
 
Nyinyi ndiyo mabongo lala wenyewe, ukishajua kidato chake itakusaidia nini?

Humu hatupo kukaguana kanuni za uandishi, ukielewa toa ushauri usipoelewa kaa kimya tu. Kama ingekuwa kinaangaliwa hiko, mods wangekuwa wanaapprove uzi kwanza kabla ya kusoma kwa kila jukwaa.

Ukiona hakuna hiko tambua kila mmoja ana namna ya kuandika ilimradi havunji kanuni za mtandao, hebu acha dharau zako hizo.
pole sana mkuu,naona imeingia sana na imekuumiza kweli kweli, ila tambua kwamba lengo langu lilikuwa zuri tu, ajifunze namna ya uandishi, sifikiri km ni sahihi kumuona mtu anakosea then umuache aendelee kukosea.,

NB; pole kwa kuguswa na kuumizwa na ushauri usio kuhusu.
 
Inaonekana aura zenu haziendani.


Ila kwa kichekesho tu, subiri housegirl wao akiondoka mvizie uingie jikoni kwao kamata kopo la chumvi kaza kabisa alafu rudi chumbani kwako kulala
Nakuhakikishia lazima atakuja mwenyewe kukuonba ukamfungulie
Yaan nimecheka mpaka nimeshindwa kuendelea kusoma zingine. Umewaza nin jomba
 
Back
Top Bottom