Siasa za Ulaya mtu kusema uongo tu hiyo ni sababu tosha ya kuachishwa nafasi yake, wakati huku kwetu hicho ndicho kinachompaisha mwanasiasa

paul sylvester

JF-Expert Member
Mar 18, 2020
3,436
2,000
Wakati kina Zitto, Sarungi, kina Lissu n.k wakiendelea kusambaza uongo juu ya nchi yao na hali ya kisiasa nchini, kule kwa wenzetu Ulaya, Amerika na sehemu zingine zilizostarabika na kuheshimiana, kusema uongo tu ni sababu tosha ya kuwajibishwa kisiasa na hata kutolewa katika nafasi mtu aliyonayo.

Ni muhimu sasa hasa Waziri wa mambo ya nje Mh. Palamagamba Kabudi kuieleza Dunia jinsi ambavyo ilivyo tofauti ya siasa za Ulaya, Amerika na huku kwetu Afrika na Tanzania.

Mambo mengi ambayo yanasambazwa na hao wenzetu, ni ya uwongo na hayana hata chembe ndoogo ya ukweli.

Tofauti ya siasa zetu na Ulaya, ni uongo!
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,135
2,000
EU wametoa hoja zao ambazo ni i.kukosekana demokrasia kwenye uchaguzi mkuu.
ii. polisi kuhujumu uchaguzi.
iii. kupokea pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona. Hizi ndio hoja ambazo kabidi anashindwa kujibu.

Lakini tujiulize je madai ya EU ni ya uongo?
1. Je, vyombo vya dola havikutumika kuvuruga uchaguzi?
2. Je, watu hawakukamatwa?
3. Je, hakuna walioripotiwa kuuawa?
4. Je, hatukuchukua pesa za corona?

Kwanza kuchukua pesa za Corona wakati tulisema hatuna Corona ni utapeli. Serikali imejipatia pesa kwa njia za udanganyifu. HII NI JINAI NA UHUJUMU UCHUMI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom